Wakati wa Nyerere na Mwinyi waandamanaji walifika Ikulu na hakuna aliyeuawa

Mjadala huu umeanza safi sana halafu kitaaluma kabisa!
KUELEKEA KUFUNGA MWAKA, HUU NDO MJADALA SAFI NA KUNA CHA KUJIFUNZA HUSUSUSANI POST KUMI ZA MWANZO
 
Nilivyosema ni kweli huko nyuma watu waliandamana na maandamano yalipoonekana yatahatarisha amani na usalama yakazimwa na polisi - kama ilivyofanyika MO29 na waandamanaji hawakuiba wala hawakuharibu mali. Hii hukuisoma?
Akina Warioba wakachapwa fimbo ikulu na mwenyewe Nyerere. Hapa hukunifahamu? Vijana wa leo wanajifanya wanajua lakini hawajui chochote. Ni mihemko tu. Jee nawe umo?

..sasa kuchapwa viboko unalinganisha na vijana kuchapwa risasi tena wengine wakiwa majumbani kwao?

.
 
Wananchi unamaanisha hao vibaka waliopigwa risasi au unamaanisha wale watiifu kwa sheria za nchi?.

..hata kibaka hastahili kuuwawa.

..Polisi wetu wamefundishwa namna ya kukamata vibaka, pamoja na kuwatawanya.

..pia wako wako wananchi waliouwawa wakiwa majumbani.

..haiwezekani Polisi wetu wenyewe wafanye mauaji makubwa kuliko wakati wa vita tuliyovamiwa na majeshi toka nje.

..Hii nchi ni yetu sote. Tusikubali maisha ya Watanzania wenzetu yatolewe thamani kiasi hiki.
 
Ndio maana tunasema yake hayakuwa maandamano ilikuwa vurugu yenye kutaka kuiangusha serikali, wangepoteza umakini siku ya pili serikali ingeangushwa.

Vita haina macho inapoanza, yale maisha tuliyoishi kwa siku mbili tu, kule DRC huwa utaratibu waliokwisha kuuzoea.

Huko Goma na Kivu kuna sehemu ukikatiza inabidi vidole vya mikono viwe mbele ya pua, unakutana na harufu za maiti zinazoharibika.
 
..Samia na genge lake ndio waliofikisha nchi kwenye machafuko.

..walishauriwa kwa muda mrefu,na kubembelezwa, wafanye marekebisho ktk mifumo ya uchaguzi lakini wakapuuza.

..matokeo yake ni joto la kisiasa kupanda nchini na kupelekea wananchi kufanya vurugu siku ya uchaguzi.

..lawama kubwa zaidi ni jinsi walivyotumia nguvu iliyopitiliza kudhibiti maandamano. Waandamanaji hawakuwa na silaha za moto hivyo hakuna uhalali wowote ule kuwatawanya kwa kutumia risasi na bunduki za kivita.
 
hv maandamano na kuchoma vitu vina uhusiano gan ?
Mwl wako wa uraia akiona hii atalia sn

Kwasas adui wa taifa ni ujinga wenu
mbona swali lako hata haliendani na nilichokiandika

anyway, chunga sana usijekuwa mjinga unayeona wenzako ndio wajinga ni mbaya sana.

maana umeandika pumba sijui mwalimu wangu wa uraia mara uhusiano wa maandamano na kuchoma vitu, sijui hata umejibu reply ya nani
 
..sasa kuchapwa viboko unalinganisha na vijana kuchapwa risasi tena wengine wakiwa majumbani kwao?

.
Huelewi kinachozungumzwa. Sijui umeona kichwa cha habari hii tunayoijadili na kukielewa? Kwa taarifa tu, mimi najadili hili bandiko.

Nimesema wakati wa Nyerere na Mwinyi kulikuwa na maandamano nayo yakazimwa kama yalivyozimwa yale ya MO29, ila katika maandamano hayo waandamanaji hawakuiba, hawakuharibu mali wala kuua askari.

Pamoja na yote hayo, bado yalizimwa na polisi baada ya kuonekana uwezekano wa kutokea fujo na uharibifu seuze yale yaliyofanywa kwa kushiriki katika wizi, uharibifu wa mali na mauaji ya askari.

Risasi zilikuwa ni matokeo ya uuaji wa askari, wizi na uharibifu wa mali.
 
Tarehe 29 October hapakuwa na maandamano mnajaribu kuweka urembo kwenye tukio la wizi na uasi dhidi ya serikali.
Hivi inawazekanaje kukawa na ''organized crime'' nchi nzima? Yaani wezi kuanzia Mbeya, Mwanza, Dar, Dodoma etc
Kilichotakiwa ni kulinda Waandamanaji na kukamata wahalifu
Kwa mwaka mzima Polisi walipita mitaani kwa kutisha si kusoma mazingira. Serikali ilinunua magari ya deraya si kutafuta sukuhu ya tatizo.
Suala la Nyerere umeandika uongo, maandamano aliyapokea yeye mwenyewe pale Ikulu, alitaka kupinduliwa mwaka 1964, maandamano aliyapokea mwaka 1966 Samuel Sitta akachapwa viboko na Mwalimu Nyerere mbele ya hadhara.
Nyerere hakuua ! waliopigwa viboko kwa ultimatum ni pamoja na akina Warioba ambao baadaye walikuwa washauri wa Mwalimu na leo ni Wazee wenye heshima katika Taifa.

Maadamano yale ya Mwinyi kutoka Wanafunzi wa UDSM mmoja wao alikuwa James Mbatia, yupo hai hakukuuawa na ni kiongozi anayeheshimika pia

Mwaka 1964 ilikuwa ''army mutiny' washiriki wakiwa askari . Hakuna Raia aliyeshiriki .
Kilichotokea MO29 ni ''mass uprising' kwa maana yake halisi ikifanywa na Raia

Kutenganisha mambo hayo mawili ni muhimu!

JokaKuu
 
Huelewi kinachozungumzwa. Sijui umeona kichwa cha habari hii tunayoijadili na kukielewa? Kwa taarifa tu, mimi najadili hili bandiko.

Nimesema wakati wa Nyerere na Mwinyi kulikuwa na maandamano nayo yakazimwa kama yalivyozimwa yale ya MO29, ila katika maandamano hayo waandamanaji hawakuiba, hawakuharibu mali wala kuua askari.

Pamoja na yote hayo, bado yalizimwa na polisi baada ya kuonekana uwezekano wa kutokea fujo na uharibifu seuze yale yaliyofanywa kwa kushiriki katika wizi, uharibifu wa mali na mauaji ya askari.

Risasi zilikuwa ni matokeo ya uuaji wa askari, wizi na uharibifu wa mali.

..askari wangapi walikufa?

..maana tukijua idadi ya askari waliouwawa, na namna walivyouwawa, tutaweza kujua kama nguvu iliyotumika ilikuwa sahihi au la.

..sasa umewahi kujiuliza kwanini idadi ya askari Polisi waliouwawa haitajwi?
 
Kipindi cha Mwalimu Nyerere, tena yeye alishanusurika kupinduliwa na wanajeshi, wasomi wa chuo kikuu waliandamana mpaka Ikulu.

Kipindi cha Mzee Mwinyi waandamanaji walifika Ikulu upande ule ilipo Ofisi ya Waziri Mkuu na hakuna aliyeuwawa.
Muuaji ni Muuaji tu hakuna namna ya kumsafisha...
 
1766710592886.jpg
 
Kuna dhana inaenezwa na wazalendo uchwara kwamba kuandamana kwenda Ikulu ni kutaka kufanya mapinduzi, au uhaini.

Wazalendo uchwara wanakwenda mbali na kudai kwamba yeyote anayepanga maandamano kwenda Ikulu anastahili kuuwawa hapo alipo.

Ukweli ni kwamba ktk jamhuri yetu maandamano yamewahi kwenda Ikulu na vyombo vyetu havikuamrishwa kuuwa waandamanaji.

Kipindi cha Mwalimu Nyerere, tena yeye alishanusurika kupinduliwa na wanajeshi, wasomi wa chuo kikuu waliandamana mpaka Ikulu.

Kipindi cha Mzee Mwinyi waandamanaji walifika Ikulu upande ule ilipo Ofisi ya Waziri Mkuu na hakuna aliyeuwawa.
Acha uzwazwa we mkongwe hapa hawakuharibu chochote wala kuiba chochote na hoja zao zilisikilizwa zikafumbuliwa.
 
Kuna dhana inaenezwa na wazalendo uchwara kwamba kuandamana kwenda Ikulu ni kutaka kufanya mapinduzi, au uhaini.

Wazalendo uchwara wanakwenda mbali na kudai kwamba yeyote anayepanga maandamano kwenda Ikulu anastahili kuuwawa hapo alipo.

Ukweli ni kwamba ktk jamhuri yetu maandamano yamewahi kwenda Ikulu na vyombo vyetu havikuamrishwa kuuwa waandamanaji.

Kipindi cha Mwalimu Nyerere, tena yeye alishanusurika kupinduliwa na wanajeshi, wasomi wa chuo kikuu waliandamana mpaka Ikulu.

Kipindi cha Mzee Mwinyi waandamanaji walifika Ikulu upande ule ilipo Ofisi ya Waziri Mkuu na hakuna aliyeuwawa.

Sasa Maza yuko KIZIMKAZI au Dodoma lakini anaogopa maandamano ya kuelekea Magogoni.
 
..askari wangapi walikufa?

..maana tukijua idadi ya askari waliouwawa, na namna walivyouwawa, tutaweza kujua kama nguvu iliyotumika ilikuwa sahihi au la.

..sasa umewahi kujiuliza kwanini idadi ya askari Polisi waliouwawa haitajwi?
Sijui idadi ya askari waliouwawa kama ambavyo sijui, nawe hujui idadi ya waliokufa. Idadi inayotolewa ni ya uongo. Hoja yangu ilikuwa kwamba maandamano yaligeuka kuwa uharamia wa kuiba, kuharibu mali na kuua. Hii ni kwasababu vijana wa leo hamuna hekima wala ustaarabu kwa kukosa elimu - siyo taaluma.
 
..kuiba, na kuharibu mali, hakuna anayebisha.

..tatizo liko kwenye vifo. Sina uhakika kama kuficha vifo vilivyotokea kutasaidia kupata suluhisho ya yaliyotokea.

..kwa mfano, tutajuaje kama Polisi walitumia nguvu stahiki au la, ikiwa hatujui idadi ya vifo, jinsi vifo hivyo vilivyotokea, na wapi vilitokea?
 
Vijana wa leo wanajifanya wanajua lakini hawajui chochote. Ni mihemko tu. Jee nawe umo?
Kweli kabisa. Hawajui chochote ila wanajiona wao wana akili mnoo. Yumkini kuna shida kwa maprofesa huko vyuoni huenda nao wamekuwa wanaharakati. Haiwezekani graduates wakawa wajinga kwa kiwango hiki.
 
Back
Top Bottom