Wakati wa Nyerere na Mwinyi waandamanaji walifika Ikulu na hakuna aliyeuawa

Kwahiyo nchi hii haina polis na mahakama ?

Shabikien tu ila hiko kikombe atakinywa kila mtu sio Zenj wala Bara mpk mkipata akil ya kuungana kukemea
Tungekuwa na nguvu kubwa ya kukemea endapo ule ujinga wa wanaojiita waandamanaji usingefanyika, kitendo cha kuchoma mali za watu, kuharibu miundombinu na wizi lilileta mgawanyiko kwa raia.

Sidhani kama hayo yasingefanyika kuna mtu hata mmoja angeuawa

Kwa hiyo usijione wewe ndiye unayejua kukemea na kutoa vitisho, kuna raia wenye hasira zetu pia tunawasubiri siku mjae kwenye mfumo mrudie ule ujinga wenu
 
Huko chuo cha Moshi na kwingineko, polisi hamfundishwi namna ya kudeal na waandamanaji hata wenye fujo??
FFU kazi yao pakitokea fujo na watu kuvunja mali za umma ni kupiga risasi za vichwa tena kwa kuwafata watu nyumbani???Au mnawafanya watu wajinga???
Polisi waliingia kwa lengo la kuua dhamira ilikua inaonekana kwenye matendo yenu - hatukuona kwamba mlitumia maji ya kuwasha au other means ambazo tunaamini mlimfundishwa.Kama training yenu ndo ile kuwa pakitokea fujo pigeni risasi za vichwa tena kwa kuchomoa watu majumbani, basi tuna hasara kubwa sana kama taifa.
Mali na uhai wapi na wapi??Tungesikia au kuona kuwa waandamanaji wameua wananchi kadhaa...na wanaendelea kuua..tungesema kweli, lkn waandamanaji wanaoiba mitungi ya gesi, wanaenda kwenye kituo cha mafuta, wanaacha kuchoma kisima cha mafuta, wanachoma pump, wangekua ni magaidi kama mnavyowaelezea mnafikiri walikua wanashindwa kuchoma yale mavisima ya mafuta vituoni?na kutengeneza mabomu ambapo watu wengi wangekufa????Hamuoni kuwa hao ni watu walikua wanapeleka ujumbe aggressivelly lkn pia walikua wanachukua caution..thus hawakuwa magaidi wale..You killed them in cold blood
Vurugu zilianza saa nne, hayo mauaji unayosema (nafikiri uliyaona na si kuhadithiwa tu na maria au Mzee aliyejichokea warioba) yalianza saa ngapi?!!!!!! Kabla ya hapa, mabomu ya machozi hayakupigwa?!!!! Vyombo vya ulinzi havikutoa Rai ya kutulia?!!!!! Kiongozi (msemaji (mbeba ujumbe mkuu)) katika maandamano Yale alikuwa nani na kituo Cha maandamano Yale kilikuwa wapi?!!! Au Kila mahali penye Mali za wasanii wasiomchukia Samia kama waandamanaji walivyoonekana wakisema walipotoka kuharibu Mali za bill nenga na shishi?!!!

Wapiga kura waliokatwa vidole unawazungumziaje?!!! Polisi kadhaa waliouawa na hao 'waandamanaji' unawazungumziaje (au mmekubaliana hili mlipinge)'?!!!! Una ufahamu wowote wa masuala ya kiusalama au ndo wale wa kuambiwa tu na kina lema na maria?!!!!!
Hapo unaposema hawakuwa na Nia ya kichoma visima vya mafuta sheli umesema ukiwa na akili timamu au labda Bado umelala?!!! Ulibahatika kuwa karibu na walipokuwa wanapita na kufanya uharibifu hao watu wenu?!!!! Mi nilikuwepo na nikibahatika kuona 'maajbu ya dunia' so usitukumbushe kwa kutukera kuhusu dhulma mlizokuwa mnajifanya katika "maandamano" yenu.
 
Hayo yote yasingefanyika hakuna hata mtu mmoja angeuawa, usitegemee kufanya ujinga ukijua kuwa utalindwa never! too bad iliongeza mgawanyiko kwa wananchi sahv wapo pia wanaoungana na serikali kupinga zile vurugu wakati mwanzo hakukuwa na wananchi waliokuwa na mwelekeo wa kupinga maandamano
 
Kipindi cha Mwalimu Nyerere, tena yeye alishanusurika kupinduliwa na wanajeshi, wasomi wa chuo kikuu waliandamana mpaka Ikulu.
Ni kweli, hata wengine akina Joseph Sinde Warioba, wakapigwa fimbo na Nyerere pale Ikulu, lakini hao waandamanaji hawakuiba, hawakuharibu mali za umma wala za watu binafsi.

Nikukumbushe tu mwaka 1977 maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam
yalimalizia Manzese kwa kuzimwa na Polisi. Huenda hili umelisahau. Hakuna serikali inayozembea inapoona kuna uvunjifu wa amani au tishio la uharibifu.
Kipindi cha Mzee Mwinyi waandamanaji walifika Ikulu upande ule ilipo Ofisi ya Waziri Mkuu na hakuna aliyeuwawa.
Ni kweli, siyo maandamano tu bali hata matusi ya nguoni dhidi ya mzee Mwinyi pale UDSM lakini hakuna aliyeharibu mali au kuiba. Kizazi cha leo hakijitambua halafu kinajifanya kinajua!
 
..kwanini watu wanataka kumuondoa Raisi kwa maandamano, na sio uchaguzi?
..kuna mahali waandamanaji wamekosea.
Uchaguzi ndio njia ya kuweka na kuondoa viongozi, lakini, kama haupo tutegemee nini? Maadamano ya mtaani ni hitimisho tu ! watu waliandamana mioyoni siku nyingi. Tunafanya uchaguzi unaibiwa , unaharibiw. Waliochafua wanatumia mbinu za maridhiano. Ukichanganya na hisia nyingine utaona kwanini ilitokea!
..kuna mahali Rais amekosea na kupelekea kuwepo na hisia na hamasa za maandamano.
..Nini kifanyiwe marekebisho ili maafa yasijirudie?
Nyerere alipoona kuna ''tension' kati ya Mrema wa NCCR na CCM akashauri watu waachwe wambebe.
Watu walimbeba Mrema mpaka wakachoka .

Kuanzia mwaka jana kuna kauli za vyombo vya ulinzi kulinda amani! yaani kuviandaa kwa tatizo
Tukaona askari Polisi na Wanajeshi wakifanya mazoezi mitaani na deraya za kijeshi, mbio na nyimbo za kejeli

Yote hayo yakatengeneza 'tension' tukijua Wananchi walikuwa na ya moyoni. MO29 Polisi wangelinda maandamano kusingetokea uvunjifu wa amani, hawakuweza kwasababu waliandaliwa kushambulia kisaikolojia na kwa zana. Wananchi nao waka react kwasababu zile zile za kuona misuli mitaani na maderaya.
 
Ni kweli, hata wengine akina Joseph Sinde Warioba, wakapigwa fimbo na Nyerere pale Ikulu, lakini hao waandamanaji hawakuiba, hawakuharibu mali za umma wala za watu binafsi.

Nikukumbushe tu mwaka 1977 maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam
yalimalizia Manzese kwa kuzimwa na Polisi. Huenda hili umelisahau. Hakuna serikali inayozembea inapoona kuna uvunjifu wa amani au tishio la uharibifu.

Ni kweli, siyo maandamano tu bali hata matusi ya nguoni dhidi ya mzee Mwinyi pale UDSM lakini hakuna aliyeharibu mali au kuiba. Kizazi cha leo hakijitambua halafu kinajifanya kinajua!

..kwa hiyo unakubali kwamba kuna upotoshaji kuhusisha maandamano na uhaini.

.. Au kudai kwamba anayetaka kuandamana kwenda Ikulu lazima atakuwa mhaini.
 
Kuna dhana inaenezwa na wazalendo uchwara kwamba kuandamana kwenda Ikulu ni kutaka kufanya mapinduzi, au uhaini.

Wazalendo uchwara wanakwenda mbali na kudai kwamba yeyote anayepanga maandamano kwenda Ikulu anastahili kuuwawa hapo alipo.

Ukweli ni kwamba ktk jamhuri yetu maandamano yamewahi kwenda Ikulu na vyombo vyetu havikuamrishwa kuuwa waandamanaji.

Kipindi cha Mwalimu Nyerere, tena yeye alishanusurika kupinduliwa na wanajeshi, wasomi wa chuo kikuu waliandamana mpaka Ikulu.

Kipindi cha Mzee Mwinyi waandamanaji walifika Ikulu upande ule ilipo Ofisi ya Waziri Mkuu na hakuna aliyeuwawa.

..
Tarehe 29 October hapakuwa na maandamano mnajaribu kuweka urembo kwenye tukio la wizi na uasi dhidi ya serikali.

Suala la Nyerere umeandika uongo, maandamano aliyapokea yeye mwenyewe pale Ikulu, alitaka kupinduliwa mwaka 1964, maandamano aliyapokea mwaka 1966 Samuel Sitta akachapwa viboko na Mwalimu Nyerere mbele ya hadhara.
 
..kwa hiyo unakubali kwamba kuna upotoshaji kuhusisha maandamano na uhaini.

.. Au kudai kwamba anayetaka kuandamana kwenda Ikulu lazima atakuwa mhaini.
Kitendo cha waandamanaji kutaka kulipua matenki ya mafuta kule bandarini kinaingia kwenye uhaini.

Kitendo cha kuchoma mabasi ya watu pamoja na vituo vya mafuta ni uhujumu uchumi,

Maandamano yanaruhusiwa yakiwa ya amani, ukishaanza kusema yatakuwa ni ya mfululizo mpaka Rais atoke ikulu huo ni uhaini.
 
Ungetukumbusha na tarehe kamili za maandano yaliyofanywa siku za uchaguzi mkuu na kwamba waandamanaji walichoma miundombinu ya umma na binafsi na kuiba mali za watu wakati wa uongozi wa Nyerere au Mwinyi ungetusaidia sana ndugu Joka Kuu.
Vijana wa Gen Z walikuwa hawajui majeshi yanafanya vipi kazi, tukio la october 29 litakuwa limewazindua, hawatakuja kucheza na mapolisi au wanajeshi katika maisha yao yaliyobakia duniani.
 
Tungekuwa na nguvu kubwa ya kukemea endapo ule ujinga wa wanaojiita waandamanaji usingefanyika, kitendo cha kuchoma mali za watu, kuharibu miundombinu na wizi lilileta mgawanyiko kwa raia.

Sidhani kama hayo yasingefanyika kuna mtu hata mmoja angeuawa

Kwa hiyo usijione wewe ndiye unayejua kukemea na kutoa vitisho, kuna raia wenye hasira zetu pia tunawasubiri siku mjae kwenye mfumo mrudie ule ujinga wenu
Vijana wana akili za kudeka hawajui hisia za mtu mwingine zinakuwa vipi.

Hawajui kwamba wapo raia ambao wana hasira na ule ujinga wa kuingia barabarani na kuanza kuharibu mali za watu.
 
Vurugu zilianza saa nne, hayo mauaji unayosema (nafikiri uliyaona na si kuhadithiwa tu na maria au Mzee aliyejichokea warioba) yalianza saa ngapi?!!!!!! Kabla ya hapa, mabomu ya machozi hayakupigwa?!!!! Vyombo vya ulinzi havikutoa Rai ya kutulia?!!!!! Kiongozi (msemaji (mbeba ujumbe mkuu)) katika maandamano Yale alikuwa nani na kituo Cha maandamano Yale kilikuwa wapi?!!! Au Kila mahali penye Mali za wasanii wasiomchukia Samia kama waandamanaji walivyoonekana wakisema walipotoka kuharibu Mali za bill nenga na shishi?!!!

Wapiga kura waliokatwa vidole unawazungumziaje?!!! Polisi kadhaa waliouawa na hao 'waandamanaji' unawazungumziaje (au mmekubaliana hili mlipinge)'?!!!! Una ufahamu wowote wa masuala ya kiusalama au ndo wale wa kuambiwa tu na kina lema na maria?!!!!!
Hapo unaposema hawakuwa na Nia ya kichoma visima vya mafuta sheli umesema ukiwa na akili timamu au labda Bado umelala?!!! Ulibahatika kuwa karibu na walipokuwa wanapita na kufanya uharibifu hao watu wenu?!!!! Mi nilikuwepo na nikibahatika kuona 'maajbu ya dunia' so usitukumbushe kwa kutukera kuhusu dhulma mlizokuwa mnajifanya katika "maandamano" yenu.
Vijana waliingizwa mkenge na kina Mange na Maria wakakutana na cha moto.

Walitaka wachekewe wakati wao walishajitambulisha kwa shari waliyoianzisha, watakuwa wamejifunza kwa namna ngumu sana hawawezi tena kuja kurudia ule ujinga.
 
..kwa hiyo unakubali kwamba kuna upotoshaji kuhusisha maandamano na uhaini.

.. Au kudai kwamba anayetaka kuandamana kwenda Ikulu lazima atakuwa mhaini.
Nilivyosema ni kweli huko nyuma watu waliandamana na maandamano yalipoonekana yatahatarisha amani na usalama yakazimwa na polisi - kama ilivyofanyika MO29 na waandamanaji hawakuiba wala hawakuharibu mali. Hii hukuisoma?
Akina Warioba wakachapwa fimbo ikulu na mwenyewe Nyerere. Hapa hukunifahamu? Vijana wa leo wanajifanya wanajua lakini hawajui chochote. Ni mihemko tu. Jee nawe umo?
 
Gen Z wajinga kupita maelezo.
 
Tungekuwa na nguvu kubwa ya kukemea endapo ule ujinga wa wanaojiita waandamanaji usingefanyika, kitendo cha kuchoma mali za watu, kuharibu miundombinu na wizi lilileta mgawanyiko kwa raia.

Sidhani kama hayo yasingefanyika kuna mtu hata mmoja angeuawa

Kwa hiyo usijione wewe ndiye unayejua kukemea na kutoa vitisho, kuna raia wenye hasira zetu pia tunawasubiri siku mjae kwenye mfumo mrudie ule ujinga wenu
hv maandamano na kuchoma vitu vina uhusiano gan ?
Mwl wako wa uraia akiona hii atalia sn

Kwasas adui wa taifa ni ujinga wenu tu
 
Nakumbuka enzi ya Mtikila pale Jangwani, baada mkutano kwisha watu walikuwa wanaandamana nae na kupita maeneo yote ya mjini bila kuharibu wala kuiba kitu
Ila hawa Okt29, hawakuwa na dhamira ya maandamano, walitaka waachiwe waende mpaka Kariakoo huku wakiharibu na kupora mali za watu mpaka kule mjini kati wangechoma, walidhibitiwa kulingana na matukio yao
 
Back
Top Bottom