chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Profesa Ibrahim Hamis Juma anastaafu mwaka huu, 2023. Jaji Mkuu alipata mamlaka hayo kipindi cha awamu ya tano, na kimsingi, ilikuwa ni mahala pa yeye kutenda alichohubiri madarasani kwa maisha yake yote ya kitaaluma kuhusu mgawanyo wa madaraka.
Ni wakati wa uongozi wake JPM aliteua Jaji wa Rufani jukwaani bila kufuata utaratibu wa kisheria wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Na Kuna Hakimu aliteuliwa na JPM kuwa Jaji kisa tu kambana mfanyabiashara kule Kahama, na baada ya JPM kumteua, hukumu alizokuwa anaandika ni sawa na wale kuku wenye manyoya yaliyocharuka
Ni wakati wa utawala wake, mahakama ilitumika kama bomba la maji, wale wasiotakiwa na awamu ya tano, harakaharaka walikimbizwa mahakamani, na mahakama ikawa inaimbiwa chorus za upelelezi unaendelalea, na mahakama ikishaambiwa hivyo, inabaki kama nyuki wa mashineni.
Ni kwa mara ya kwanza wakati Prof Juma akiwa Jaji Mkuu, wagombea wote wa uchaguzi 2020 hawakupeleka shauri lolote mahakamani.
Mahakama ilitambulika kama moja ya vifaa vya jiwe alivyotumia kuwaumiza watu ambao hawapendi.
Mpaka Prof Juma anaondoka madarakani mwaka huu, mahakama haijatoa maamuzi mazito yaliyotingisha jamii na tasnia ya sheria, tofauti na enzi ya kina Jaji Nyalali, Sammata na Ramadhani.
Ni mahakama ya Prof Juma ambayo, udhaifu wake, ndio umefanya hata SSH aunde Tume ya Kupitia mfumo wa haki jinai.
Mahakama ya Prof Juma ilikuwa dhaifu sana kuliko mahakama chini ya majaji wakuu wengine.
Ukiacha majengo yanayojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, mahakama ili-fail katika core function zake, utoaji haki. Haki hata itolewe chini ya mti, ndicho anachotaka mwananchi.
Mawakili walikuwa wanakamatwa au kutishiwa kukamatwa kwa sababu tu wanawakilisha wateja wao mahakamani.
Mahakimu walikuwa wanapewa zawadi ya Ujaji kwa kutoa hukumu za kidhalimu, mfano mzuri kesi ya Sugu mbeya.
Kwa ambao hawajui, kulitokea wimbi kubwa la mahakimu kushindana kufanya udhalimu anaoupenda Jiwe, ili Jiwe asikie, awape Ujaji.
Mahakama pia ihakikishe katika mapitio ya mfumo wa haki jinai, na yenyewe iwasilishe hoja zake, hasa zinazohusu waendesha mashtaka. Wanafanya wanavyotaka, na mahakama inaonekana hamna lolote, na kimsingi, wanaonekana Wana nguvu kuliko mahakama. In most cases, wananchi wanaona Bora umuite mwendesha mashtaka, mmalizane, aandike Nolle, au muingine katika plea bargaining, kuliko kusubiri mahakama.
Kwa heri Prof. Juma.