Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 9,830
- 20,686
Mungu wa kweli anaye abudiwa, Alishindwaje kuumba Dunia yenye usawa kwa binadamu wote?Mungu si kwa ajili ya Wazungu bali binadamu wote na viumbe vyote pamoja na Waafrika.Kama Wazungu hawamwamini Mungu na kuamini katika sayansi zao acha Waafrika maskini wamwabudu Mungu wa kweli.
Mathayo 5:1-11
Mathayo 11:23-27
Mungu wa kweli, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na Uovu wala mabaya?
Mungu wa kweli, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasioweza kutenda mabaya?
Mungu wa kweli, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na majanga ya Asili kama radi, mafuriko, matetemeko ya ardhi, vimbunga yanayo ua na yaliyo ua maelfu ya binadamu?
Mungu wa kweli, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na magonjwa na mateso?
Huyo Mungu ana ukweli gani?
Huyo Mungu yupo kweli?