Ni tofauti na unavyodhani. Mbowe anacheza chess wakati wengi wanacheza checkers. Hayuko emotional. Kwa kukubali maridhiano aliwaweka CCM mahali ambapo ilibidi walegeze kamba. Approach ya Lissu ingewapa kisingizio cha kutolegeza mahali popote. Wangesema tutafanya nini wakati mwenzetu hataki kukaa mezani na sisi! CDM waneonekana unreasonable.
Amandla...
Kwenye maridhiano hayo ndipo kwenye mtihani, wamemtangaza hadi BBC kuwa ni gaidi a very serious crime. Wakatengeneza kesi wakabumba kwenye ushahidi kwa aibu wanakimbilia kwenye maridhiano. USA walijadiliana na Osama?
Kuwakamata na kuwabambikizia kesi CHADEMA, kuzuia haki ya kufanya siasa kinyume cha sheria, kuwafilisi viongozi wa CHADEMA ni suala la mjadala wa mwaka mzima? Si haki yao? Kwa nini kwenye maridhiano hawakuzungumzia mfumo unaowapa mamlaka ya kuamua kuwakamata na kuzuia tena haki zao? Ambao ni katiba.
Unataka wote tushawishike kwamba maridhiano ni favour ya CCM kwa CHADEMA? Kuwaruhusu kufanya siasa kwa matakwa ya CCM? Kwa hiyo Mbowe ni gaidi au la? Aliyemsafisha ni nani ni mahakama au maridhiano? Nini kitakachomzuia Samia kesho kuamua kumtangenezea tena kesi ya uhaini yeye au mwingine tena?
Uhaini na ugaidi wa Mbowe umefutwa kwa maridhiano? Hakuna chochote behind the scene? Kama wana dhamira nzuri ya maridhiano uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita umefanywa na watu wenye dhamira ya maridhiano?
Mtu kama Lissu ambaye tangu awali alishtukia huu mtego na akasema wazi wahafidhina na CCM wanajua huyu hawawezi kumdhibiti labda kumuua ndio mnakuja na dhana ya kuwa emotional. Kwa unataka tuamini kwamba siasa za Tanzania kufanya ni FAVOUR ya CCM siyo RIGHTS za wapinzani?
Nini mafanikio ya maridhiano? Waonekame reasonable lakini kwenye uchaguzi wanaibiwa wanaporwa wanatekwa na kuuliwa na wauaji wanaenda scot free?
Kwa nini CCM wote na makada wao hata humu jukwaani mnamsifia Mbowe? Miaka zaidi ya 20 madarakani haitakiwi changes? CCM mnanufaika na nini kwa Mbowe kama siyo mnammiliki na yupo kwa maslahi yenu?
Lissu ni mbaya kwa CCM sababu alisema wazi kuwa mapendekezo yao CCM waliyakataa yote na Mbowe kimya maana katulizwa