Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Kila siku, Kanisa Katoliki hutumia Biblia kwenye Masifu, Misa na sala zingine sasa sijui unaelewa unachoongea ? injili husomwa kila siku
 
Bikra Maria alibarikiwa na Mungu ili uzao utakatifu upitie kwake. Kwa hiyo ni Roho inaishi unaweza kuisujudia na ikakusaidia.
Yesu Kristo - ni Roho katika ule utatu na inaishi ambayo tunakombolewa nayo kwa Damu iliyomwagika pale msalabani.
 
Biblia inasema mungu hana baba wala mama hana mwanzo wa siku wala mwisho wa miaka
Sasa huyu mungu unaemuongelea sio yehova muumbaji
Huyu mungu aliezaliwa ni wakipagani upo sahihi
Wewe ni mkristo? Tunaamini Yesu ni Mungu? Bibilia ipi unasoma wewe?🤣
 
Wewe huna lolote unalojua. Mvivu wa kufuatilia. Eti vimeongezwa. Yani watu wavikate vitabu miaka 1500 baadae ndio useme tumeongeza? Kweli waprotestanti mna funza kichwani.😂 Ukimuamsha mtu wa mwaka 1200 huko akiona kipande cha bibilia mnachosoma atawashangaa sana. Nani alimpa mamlaka Luther kukata vitabu? Paulo , na wengine wote vitabu vyao vikikuwa vinajitegemea, ndio kanisa kwa kuvuviwa na Roho wa Mungu likavikusanya alafu mnajikuta mnajua.
 
Shida yako ni kumwomba Maria au kutaka kujua anaishi nchi gani? Maana naweza kuwa najibu swali ambalo hujaniuliza.
Mwanzo nilikuuliza kama yupo hai ukajibu yupo hai na anaishi. Sasa niambie anaishi nchi gani mkuu.
 
Mwanzo nilikuuliza kama yupo hai ukajibu yupo hai na anaishi. Sasa niambie anaishi nchi gani mkuu.
Nilisema hivi, Yesu anayemwamini hata kama atakufa, ataishi (ataendea kuishi kiroho). Kwa mantiki hii hata yeye ataendelea kuishi, si kimwili, bali kiroho. Sasa kama huamini achana na hii submission.
 
Sasa hapa umeandika nini mkuu? Unataka kutuaminisha kuwa bikra Maria ni mmoja wa malaika wa Mungu?
 
Mkuu umemaliza kila kitu; uzi ufungwe.
 
Bikra Maria alibarikiwa na Mungu ili uzao utakatifu upitie kwake. Kwa hiyo ni Roho inaishi unaweza kuisujudia na ikakusaidia.
Yesu Kristo - ni Roho katika ule utatu na inaishi ambayo tunakombolewa nayo kwa Damu iliyomwagika pale msalabani.
Kwa hiyo bikra Maria na Yesu wana hadhi sawa mkuu? Unaweza ukaamua ama kumuomba Maria au Yesu?
 
Kuna haja gani ya kupitisha maombi yetu kwa Maria wakati Yesu alishasema maombi yote yaende kwake moja kwa moja na atayapokea na kuyajibu?
 
Kuna haja gani ya kupitisha maombi yetu kwa Maria wakati Yesu alishasema maombi yote yaende kwake moja kwa moja na atayapokea na kuyajibu?
Na kuna ubaya gani kupitisha maombi yetu kwa Mama Maria kisha akafikisha kwa Yesu? Zote ni njia cha muhimu maombi yafike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…