Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Mroman yupo tayari asikilize vyoote kutoka kwako isipokuwa tuu injili.
Hapo ndipo utaiona sura yake halisi.
Yeye stori za kutungwa na madogma yupo tayari kuamini isipokuwa neno la mungu tuu.

Wakristo waliuwawa kwa kupinga uromani,wafia imani mamilioni kwa mamilion ya wakristo.
Martin,columbus,irenios,luther na wengine wengi walikumbana na hayo.
Soma wafia imani waliuwawa na katoliki,kanisa likajifanya kutubu na kuwaita majina yao majina ya makanisa yao.

Waromani ni Mafarisayo wa wakati huu,ukiwaona ni kama wema na wapole ila ndani mwao ni mbwa mwitu.
Uwezo mkubwa wa ibilisi wa sasa ni kuweza kuigizia ukristo na mambo ya kiungu.

Mathayo 23:27-30
[27]Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote.

[28]Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.

[29]Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki,

[30]na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.
Kila siku, Kanisa Katoliki hutumia Biblia kwenye Masifu, Misa na sala zingine sasa sijui unaelewa unachoongea ? injili husomwa kila siku
 
Bikra Maria alibarikiwa na Mungu ili uzao utakatifu upitie kwake. Kwa hiyo ni Roho inaishi unaweza kuisujudia na ikakusaidia.
Yesu Kristo - ni Roho katika ule utatu na inaishi ambayo tunakombolewa nayo kwa Damu iliyomwagika pale msalabani.
 
Biblia inasema mungu hana baba wala mama hana mwanzo wa siku wala mwisho wa miaka
Sasa huyu mungu unaemuongelea sio yehova muumbaji
Huyu mungu aliezaliwa ni wakipagani upo sahihi
Wewe ni mkristo? Tunaamini Yesu ni Mungu? Bibilia ipi unasoma wewe?🤣
 
Miaka 400bk 500bk mnaleta vitabu vya vilivyotungwa na walevi mnavupachika kwenye biblia takatifu.
Vitabu vimetungwa na wanawake.

Mungu alifunga kitabu chake kwa paulo.
Hao ndio waliotokewa na Mungu moja kwa Moja kukiandika,pamoja nawale walioshuhudia maisha ya kristo yesu.

Ukitunga kitabu chako lazima kikubaliane na msingi wa ukristo ,ukiweka kitabu kinapingana na hao mashahidi basi jua alikupa ibilisi.

Hvyo viyabu viliingizwa kwa hila kusapot upagani wa rumi.
Na Mungu aliwaaibisha,watoto wa Mungu wamedumu na biblia ya kweli ya asili tangu mitume.
Wewe huna lolote unalojua. Mvivu wa kufuatilia. Eti vimeongezwa. Yani watu wavikate vitabu miaka 1500 baadae ndio useme tumeongeza? Kweli waprotestanti mna funza kichwani.😂 Ukimuamsha mtu wa mwaka 1200 huko akiona kipande cha bibilia mnachosoma atawashangaa sana. Nani alimpa mamlaka Luther kukata vitabu? Paulo , na wengine wote vitabu vyao vikikuwa vinajitegemea, ndio kanisa kwa kuvuviwa na Roho wa Mungu likavikusanya alafu mnajikuta mnajua.
 
Shida yako ni kumwomba Maria au kutaka kujua anaishi nchi gani? Maana naweza kuwa najibu swali ambalo hujaniuliza.
Mwanzo nilikuuliza kama yupo hai ukajibu yupo hai na anaishi. Sasa niambie anaishi nchi gani mkuu.
 
Mwanzo nilikuuliza kama yupo hai ukajibu yupo hai na anaishi. Sasa niambie anaishi nchi gani mkuu.
Nilisema hivi, Yesu anayemwamini hata kama atakufa, ataishi (ataendea kuishi kiroho). Kwa mantiki hii hata yeye ataendelea kuishi, si kimwili, bali kiroho. Sasa kama huamini achana na hii submission.
 
  • Ufunuo 5:8: "Na alipoitwaa kile kitabu, wale wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vikombe vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambazo ni maombi ya watakatifu."
  • Ufunuo 8:3-4: "Na malaika mwingine akaja, akasimama mbele ya madhabahu, akiwa na chetezo cha dhahabu; naye akapewa uvumba mwingi, ili aufanye pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi. Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu kutoka mkononi mwa malaika."
Sasa hapa umeandika nini mkuu? Unataka kutuaminisha kuwa bikra Maria ni mmoja wa malaika wa Mungu?
 
Waroman hawana majibu ya kimaandiko.
Maana maisha mazima ya uroman ni upagani.
Na waumini wanaburuzwa wakiangamuzwa kwakukosa maarifa.
MARIAMU si bikira tenaa baada ya kumzaa yesu, tena alizaa na mtoto mwingine kama yohana.
Mariamu ilimbidi akafunge nakuomba moaka siku ya pentekost ili apokee roho mtakatifu. Laa hata kuwepo mbinguni.
Mariamu hakutoa chembe yoyote ile kwenye utungaji wa mimba ya yesu

YESU kamwe hakuwahi kumuita mariamu mama maisha yake yote,alimuita mwanamke kwisha.
Biblia inasema hakuna wakukuombea utapeleka maombi yako mwenyewe mbele za Munguu.
Na ndio sababu ya pazia la hekalu kupasuka alipokata roho

Roman inaibada za kishetani za mapapa waliokufa,wakiisujudu mifupa yao nakuomba wawaombee

Mariamu yupo akisubiri ufufuo wa wafu siku ya mwisho.
Unaomba mtu ambae amelala kwa tumaini tu.
Wao wamemtoa roho mtakatifu wakaweka mariamu nafasi yake

Hivi unaombaje mariamu badala ya kuomba Mungu moja kwa moja.
Yesu alisema ombeni lolote kwa jina langu sio la mariamu
Mkuu umemaliza kila kitu; uzi ufungwe.
 
Bikra Maria alibarikiwa na Mungu ili uzao utakatifu upitie kwake. Kwa hiyo ni Roho inaishi unaweza kuisujudia na ikakusaidia.
Yesu Kristo - ni Roho katika ule utatu na inaishi ambayo tunakombolewa nayo kwa Damu iliyomwagika pale msalabani.
Kwa hiyo bikra Maria na Yesu wana hadhi sawa mkuu? Unaweza ukaamua ama kumuomba Maria au Yesu?
 
Wewe hauwezi kuzungumza na Mama akamueleze Baba kama unahitaji jambo fulani? Bikira Maria ndiye alimzaa Yesu, anamjua mwanaye na aliumia hata wakati anateswa msalabani, Anamfahamu vyema mwanae.Kwenye Harusi ya Kana baada ya Divai kuisha mbona hawakumuendea Yesu moja kwa moja bali walienda kwa mama yake ili akawaombee? Kuna ubaya gani kupitisha maombi yako kwa mama ili yamfikie Baba? Hususan kama una makosa fulani uliyatenda yanayokufanya mpaka unaogopa kwenda kwa Baba.Kuhusu kufa na kufufuka mbona wapo watakatifu wengi tu ambao walikufa miili ila roho zao zi hai, Na wanatuombea kila siku, mfano Yesu alipokuwa mlimani alitokewa na Manabii Musa na Eliya ambao walishakufa zamani, Mifano ni mingi ila kwa leo ngoja tuishie hapa.
Kuna haja gani ya kupitisha maombi yetu kwa Maria wakati Yesu alishasema maombi yote yaende kwake moja kwa moja na atayapokea na kuyajibu?
 
Kuna haja gani ya kupitisha maombi yetu kwa Maria wakati Yesu alishasema maombi yote yaende kwake moja kwa moja na atayapokea na kuyajibu?
Na kuna ubaya gani kupitisha maombi yetu kwa Mama Maria kisha akafikisha kwa Yesu? Zote ni njia cha muhimu maombi yafike
 
Back
Top Bottom