Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto.
Hapa unawaambia nini ambao huamini kua Yesu ni Mungu? kwa mujibu wa andiko lako hapa ni kua Yesu na Mungu ni vitu viwili tofauti,

Ufafanuzi tafadhali.
 
Wewe hauwezi kuzungumza na Mama akamueleze Baba kama unahitaji jambo fulani? Kwenye Harusi ya Kana baada ya Divai kuisha mbona hawakumuendea Yesu moja kwa moja bali walienda kwa mama yake ili akawaombee? Kuna ubaya gani kupitisha maombi yako kwa mama ili yamfikie Baba? Hususan kama una makosa fulani uliyatenda yanayokufanya mpaka unaogopa kwenda kwa Baba.Kuhusu kufa na kufufuka mbona wapo watakatifu wengi tu ambao walikufa miili ila roho zao zi hai, Na wanatuombea kila siku, mfano Yesu alipokuwa mlimani alitokewa na Manabii Musa na Eliya ambao walishakufa zamani, Mifano ni mingi ila kwa leo ngoja tuishie hapa.
Kwani bikra Maria alipaishwa mbinguni kama Yesu mkuu? Hebu tupe kifungu kwenye biblia kinachothibitisha hili.

Naomba pia utupe mistari ya biblia inayoonesha Yesu kutokewa na manabii waliokufa siku nyingi mkuu.
 
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipatke kufunguka macho.

Asanteni sana.

Kule Makha Bikira Maria anajulikana kwa Majina haya👇🏽👇🏽👇🏽
Maryam
مَرْيَم
Mary
Titleal-Qānitah (the Woman who submits to God)
al-Sājidah (the Woman who prostrates to God)
al-Rāki’ah (the Woman who bows to God)
al-Ṣa’ima (the Woman who fasts)
al-Ṭāhirah (the Purified)
al-Ṣiddīqah (the Truthful)
al-Mustafia (the Chosen)
 
Attachments

  • msikie dr sule akisema mama yake yesu ndo mwanamke bora na mzur.mp4
    1.2 MB
Wakatoliki wanaamini katika kanisa moja lenye muunganiko kiroho wa waliohai duniani, wafu walio toharani na Watakatifu walio mbinguni. Hawa watakatifu huwaombea walio hai na miongoni mwa watakatifu hao, Bikira Maria/Mariamu ni mwenye daraja ya juu. Maria alikufa kifo cha kawaida ila wanaamini hakuoza mwili kaburini, bali alipalizwa mbinguni. Fundisho la Maria kuwaombea watu limetokana na kisa katika Biblia ambapo Maria na Yesu walipokuwa katika harusi huko Kana, Maria aliwaombea watu divai na kwa kumtii mamaye Yesu alifanya muujiza wa kugeuza maji kuwa divai (Yohana 2: 1-25).
Kimsingi haya ni mambo ya kiimani hayambani mtu hasa asiye Mkatoliki. Kiimani, kama 'mtu' ambaye ni Mchungaji au Askofu anaweza 'kuombea' watu; sembuse Mama wa Yesu?
Ya Wakatoliki tuwaachie Wakatoliki.
 
Kwa nini hamumthamini mama wa Yesu Kristo?Mnadhani katika wananawake wote kwa nini Mungu alimchagua yeye na sio mwanamke mwingine.Mnadhani Yesu hamdhamini mama yake kama ambavyo nyinyi hamumdhamini? Unakuta mtu anasali anasema anamwamini Yesu lakini ni mtu huyohuyo utamkuta anaongea vibaya kuhusu mama yake Yesu.Kama ambavyo na nyinyi mnathamini mama zenu ni hivyo hivyo na Mungu mwana anamheshimu na kumsikiliza mama yake.Kasomeni Ufunuo Bikira Maria ametajwa katika ufunuo,tatizo hamsomi biblia na hata mkisoma hamtaki kuielewa!
 
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipatke kufunguka macho.

Asanteni sana.

Yesu hana mama biblia inasema yesu alikuwako tangu mwanzo wa misingi ya ulimwengu kilicho fanyika pale ni yesu kuuvaa ubinadamu ili adhihirishe upendo wake kwa wanadamu, leo hii watu wengi wanasema mungu anatupenda ukiuliza alitufanyia nini tulianguka dhambini lakini bado yupo pamoja nasi hakutuacha hata akaja kutoka mbinguni kukaa nasi hivyo yeye hana mama alikuwako.

Je wewe mungu wako anaupendo? Je kama anaupendo tuambie alikufanyia nini? Au unasema tu unaupendo alafu hakuna kitu alicho kufanyia, lakini yesu anatupenda alituumba kwa mfano wake na hata baada ya sisi kuingia dhambini hakutuacha alikuja kukaa nasi na ame ahidi anaebda kuandaa makao ili alipo sisi tuwako.

Nina ndugu zangu wengi na marafiki zangu wengi ni wakatoliki lakini katika uhalisia ukatoliki umetengeneza vitu vingi vya uzushi ambavyo hata katika historia ya yesu na mitume wake kwenye biblia hawakuvifanya.

Yesu haku muabudu maria wala mitume, yesu hakutengeneza sanamu ya maria wala mitume, pia kanisa hili limetafuta sanamu bandia za muigizaji wa uhusika wa yesu na kuzifanya kama huyo ndio yesu yule halisi, vile vile kanisa hilo limefanya na kwa maria pia limechukua sanamu za muigizaji na kuanza kuliabudu haya yote ni uzushi na upotoshaji mkubwa wa wawtu wa mungu.
 
Wewe hauwezi kuzungumza na Mama akamueleze Baba kama unahitaji jambo fulani? Bikira Maria ndiye alimzaa Yesu, anamjua mwanaye na aliumia hata wakati anateswa msalabani, Anamfahamu vyema mwanae.Kwenye Harusi ya Kana baada ya Divai kuisha mbona hawakumuendea Yesu moja kwa moja bali walienda kwa mama yake ili akawaombee? Kuna ubaya gani kupitisha maombi yako kwa mama ili yamfikie Baba? Hususan kama una makosa fulani uliyatenda yanayokufanya mpaka unaogopa kwenda kwa Baba.Kuhusu kufa na kufufuka mbona wapo watakatifu wengi tu ambao walikufa miili ila roho zao zi hai, Na wanatuombea kila siku, mfano Yesu alipokuwa mlimani alitokewa na Manabii Musa na Eliya ambao walishakufa zamani, Mifano ni mingi ila kwa leo ngoja tuishie hapa.
Yesu hana mama yeye alikuwako tangu kabla ya maria,
 
Haya masuala nadhani mngetuachia sisi wenyewe Wakatoliki. Maana hayakuhusu/hayawahusu. Ok?
Mkuu mimi pia ni mkristo kama walivyo wakatoliki na sote tunatumia biblia moja. Naomba utufumbue macho ili tuijue kweli na tuiishi badala ya kutususia kwa kusema eti haya mambo hayatuhusu. Haya mambo yanatuhusu sana tu.
 
MRembo unatumia Biblia ipi ambayo haina jina la Maria ?
Nimekuweka andiko na wewe weka andiko toka Biblia ya Kiswahili.
Maneno ya Kashfa yanatoka katika Kichwa cha Mpumbavu tu.

Mathayo (Mat) 1:18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu
 
Kwa nini hamumthamini mama wa Yesu Kristo?Mnadhani katika wananawake wote kwa nini Mungu alimchagua yeye na sio mwanamke mwingine.Mnadhani Yesu hamdhamini mama yake kama ambavyo nyinyi hamumdhamini? Unakuta mtu anasali anasema anamwamini Yesu lakini ni mtu huyohuyo utamkuta anaongea vibaya kuhusu mama yake Yesu.Kama ambavyo na nyinyi mnathamini mama zenu ni hivyo hivyo na Mungu mwana anamheshimu na kumsikiliza mama yake.Kasomeni Ufunuo Bikira Maria ametajwa katika ufunuo,tatizo hamsomi biblia na hata mkisoma hamtaki kuielewa!
Hatu mthamini Kwasababu yesu alikuwako tangu zamani kabla ya maria yesu alikawako yeye hana mama ndivyo alivyo sema kwenye biblia "mimi msinione hivi nilikuwako tangu kuwekwa msingi ya dunia"
 
Hapa unawaambia nini ambao huamini kua Yesu ni Mungu? kwa mujibu wa andiko lako hapa ni kua Yesu na Mungu ni vitu viwili tofauti,

Ufafanuzi tafadhali.
Bila shaka hawa watakuwa wale wenzetu wavaa vibagharashia. Mimi leo siko huko mkuu. Yesu na Mungu ni roho mbili tofauti; sio kitu kimoja mkuu.
 
Kwani bikra Maria alipaishwa mbinguni kama Yesu mkuu? Hebu tupe kifungu kwenye biblia kinachothibitisha hili.

Naomba pia utupe mistari ya biblia inayoonesha Yesu kutokewa na manabii waliokufa siku nyingi mkuu.
Tuanze na wewe kwa kunionyesha kwamba hakupaishwa! Tupe kifungu kwamba hakupaishwa.

(Marko 9:2-13; Luka 9:28-36)
Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga. Mose na Elia wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.
 
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipatke kufunguka macho.

Asanteni sana.

Vipi nitapata mtoto hali hajanigusa mwanaume yeyote, wala mimi si mwasherati?" (Qur'an 19:20)
Malaika alimjibu kwamba hilo lilikuwa amri ya Mungu na rahma yake.
 
Kule Makha Bikira Maria anajulikana kwa Majina haya👇🏽👇🏽👇🏽
Maryam
مَرْيَم
Mary
Titleal-Qānitah (the Woman who submits to God)
al-Sājidah (the Woman who prostrates to God)
al-Rāki’ah (the Woman who bows to God)
al-Ṣa’ima (the Woman who fasts)
al-Ṭāhirah (the Purified)
al-Ṣiddīqah (the Truthful)
al-Mustafia (the Chosen)
Huyu shehe wenzake wakimsikia watamuua....anatakuza ukafir.
 
Tuanze na wewe kwa kunionyesha kwamba hakupaishwa! Tupe kifungu kwamba hakupaishwa.

(Marko 9:2-13; Luka 9:28-36)
Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga. Mose na Elia wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.
Tukio la Kusingiziwa

Baada ya Maryam kurudi kwa watu wake akiwa amembeba mtoto mchanga (Isa), watu walistaajabu na kumlaumu kwa kuwa na mtoto bila ya ndoa. Walisema:

"Ewe Maryam! Hakika umeleta jambo kubwa la ajabu. Ewe dada yake Haruni! Baba yako hakuwa mtu mbaya, wala mama yako hakuwa mwasherati."
(Qur'an 19:27-28)

Hapa, kaumu yake walikuwa wakimshutumu kwa uzinifu kwa sababu hawakuweza kuelewa jinsi alivyopata mtoto bila ya mwanaume.

Utetezi wa Maryam

Maryam hakuweza kujitetea kwa maneno yake. Badala yake, alimfuata amri ya Mungu ya kunyamaza na kuwaonyesha mtoto mchanga, Nabii Isa, ambaye kwa miujiza alianza kuzungumza ili kumtetea mama yake:

"[Mtoto] alisema: Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu na amenifanya Nabii."
(Qur'an 19:30)

Hili lilikuwa ni ushahidi wa wazi kwa watu kwamba Maryam hakufanya dhambi yoyote, na mtoto wake alikuwa muujiza wa Mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom