Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
NdioWewe ni mkatoliki muhishimiwa?
Mama wa Yesu jina lake ni Mariamu na sio Maria.
Hata Qurani inatambua hivyo
Na ina sura ya Mariamu
mama yake Isa.
Isa Bin Mariam.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NdioWewe ni mkatoliki muhishimiwa?
Kama unasema mungu ananguvu nyingi alafu awe na nafsi moja basi huyo mungu hana nguvu, kiumbe chenye nafsi moj6ni mwadamu mungu yeye sio mwadamu kama sisi na tunasema kuwa ananguvu nyingi kwanini jambo la nafsi tatu lishindikane mbele zake.Bila shaka hawa watakuwa wale wenzetu wavaa vibagharashia. Mimi leo siko huko mkuu. Yesu na Mungu ni roho mbili tofauti; sio kitu kimoja mkuu.
Hivi huwa hawana mawazo mengine zaidi ya kuua makafir?Huyu shehe wenzake wakimsikia watamuua....anatakuza ukafir.
Maria na Yosefu ni wazazi walezi/walishi wa Yesu, walimlea tangu utoto wake, Hata Yesu mwenyewe anawathamini, wewe ni nani usiwape thamani yao? Mungu ndiye aliwapa heshima ya kutimiza Unabii wake kupitia wao.Yesu hana mama yeye alikuwako tangu kabla ya maria,
Kifungu kinachothibitisha kuwa bikra Maria alipaishwa sina mkuu. Kama wewe unacho, unaweza kukiweka hapa kwa faida ya wengi. Kama huna, tusubiri wenyewe waje mkuu.Tuanze na wewe kwa kunionyesha kwamba hakupaishwa! Tupe kifungu kwamba hakupaishwa.
Kwa hiyo shida yako hasa ni nini?Je,unapenda uitwe "she mitoga/che mittoga/sha mititioga?Ndio
Mama wa Yesu jina lake ni Mariamu na sio Maria.
Hata Qurani inatambua hivyo
Na ina sura ya Mariamu.
Hakuna kifungu kinacho onesha kuwa alipaishwa na hakuna kifungu kinacho oneshwa kuwa hakupaishwa, je wewe unaamini alipaishwa kwa kifungu kipi?Tuanze na wewe kwa kunionyesha kwamba hakupaishwa! Tupe kifungu kwamba hakupaishwa.
(Marko 9:2-13; Luka 9:28-36)
Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga. Mose na Elia wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.
Kifungu unachopaswa kupewa mkuu ni cha kifungo cha miezi sita na viboko saba vya shingoni.Kifungu kinachothibitisha kuwa bikra Maria alipaishwa sina mkuu. Kama wewe unacho, unaweza kukiweka hapa kwa faida ya wengi. Kama huna, tusubiri wenyewe waje mkuu.
Je maria alikuwako tangu kuwekwa misingi ya dunia kabla ya yesu?Rudi "sandeskuli"!You've got an empty pumpkin!
Point na suala ni moja tu; Baada ya hayo yote, Je, Maryamu/Maria anastahili/hastahili HESHIMA kwa kuwa sehemu ya utimilifu wa Unabii wa MUNGU?Tukio la Kusingiziwa
Baada ya Maryam kurudi kwa watu wake akiwa amembeba mtoto mchanga (Isa), watu walistaajabu na kumlaumu kwa kuwa na mtoto bila ya ndoa. Walisema:
(Qur'an 19:27-28)
Hapa, kaumu yake walikuwa wakimshutumu kwa uzinifu kwa sababu hawakuweza kuelewa jinsi alivyopata mtoto bila ya mwanaume.
Utetezi wa Maryam
Maryam hakuweza kujitetea kwa maneno yake. Badala yake, alimfuata amri ya Mungu ya kunyamaza na kuwaonyesha mtoto mchanga, Nabii Isa, ambaye kwa miujiza alianza kuzungumza ili kumtetea mama yake:
(Qur'an 19:30)
Hili lilikuwa ni ushahidi wa wazi kwa watu kwamba Maryam hakufanya dhambi yoyote, na mtoto wake alikuwa muujiza wa Mwenyezi Mungu.
Hicho ndicho kinafanya awe hajazaliwa na Maria ili umdharau?Je maria alikuwako tangu kuwekwa misingi ya dunia kabla ya yesu?
Yesu hana mama Kwasababu alikuwako kabla ya maria, je hatakuwepoje kabla ya maria alafu tuseme anamama ambaye yeye alimuumba mwanzo wa uumbaji?Yesu hana mama?
Na wewe hauamini kama alipaishwa kwa kifungu kipi?Hakuna kifungu kinacho onesha kuwa alipaishwa na hakuna kifungu kinacho oneshwa kuwa hakupaishwa, je wewe unaamini alipaishwa kwa kifungu kipi?
Luka 1
29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?
30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?
35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
(Maria mnamtoa wapi ?)
1. Nani hamthamini bikra Maria mkuu?Kwa nini hamumthamini mama wa Yesu Kristo?Mnadhani katika wananawake wote kwa nini Mungu alimchagua yeye na sio mwanamke mwingine.Mnadhani Yesu hamdhamini mama yake kama ambavyo nyinyi hamumdhamini? Unakuta mtu anasali anasema anamwamini Yesu lakini ni mtu huyohuyo utamkuta anaongea vibaya kuhusu mama yake Yesu.Kama ambavyo na nyinyi mnathamini mama zenu ni hivyo hivyo na Mungu mwana anamheshimu na kumsikiliza mama yake.Kasomeni Ufunuo Bikira Maria ametajwa katika ufunuo,tatizo hamsomi biblia na hata mkisoma hamtaki kuielewa!
Piganeni tu 🤣 🤣.Hakuna jina la Maria kwenye Biblia.
Acheni kuwapotosha watu.
Mathayo (Mat) 1:18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Huwa wanatafuta mstari mmoja ulio tata kwenye biblia ili waanzishie kanisa la kupata maokoto.Pure conmen!Mnanishangaza sana Waislamu wanamtambua Bikira Maria ila nyinyi protestants hamumtambui?Hizo dini mlinazo zote zilitoka Roma.Baada ya Luther na wengineo kuondoka ndio mkapata haya makanisa yote yaliyopo sasa.Mungu ni mmoja tunaheshimu ila pia msidhihaki vitu ambavyo hamvijui kuna mengi sana ambayo protestants hamyajui.Mimi ni shuhuda wa miujiza ya Bikira Maria na ninasema hapa wakristo tunamheshimu kwa sababu ni mama wa Mungu wetu na msaada wetu katika shida.Utakapokufa Yesu mwenyewe hawezi kumpokea mtu anayemdharau mama yake, kW maneno ya kumdhihaki.Mungu ajakuambia wewe udhihaki dini au imani za watu wengine kitu ambacho hukifahamu sio vyema kukiongelea