Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Luka 1
29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?

30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?

35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

(Maria mnamtoa wapi ?)
Tatizo lako ni kumtoa wapi Maria au ni hiyo "m" wa mwisho kwenye Mariam?
 
Hakuna jina la Maria kwenye Biblia.
Acheni kuwapotosha watu.

Mathayo (Mat) 1:18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Kwanza kuwa mpole unapotaka kujua au kuuliza kitu usichofahamu au usichokuwa na uhakika nacho. Hilo ni jina tu halimbadilishi mtajwa kuwa mtu tofauti. Maeneo, makabila au hata mila tofauti zinaweza kutamka jina hilo hilo katika mazingira yao. Maria ni huyo huyo Mariamu, au Yosefu ni huyo huyo Yusufu, au Moses ni huyo huyo Musa. Abdul ndiyo huyo Abdool, Karim ndiyo huyo Kareem, Saeed ndiyo huyo Said. Inategemea wewe ni Mwarabu, au Mhindi au Mzungu au Myahudi au Mwafrika, maana hata sasa wewe unajiita Che Mittoga badala ya Mitoga!
 
Imani ni ufunuo kwa ajili ya watu fulani

Kama wakatoliki ndo wamefunuliwa hivyo na wewe hujafunuliwa bado hayo , basi yaache

Hata Neema ya ukristo tumefunuliwa wachache na ambao hawajafunuliwa hutuona sisi machizi kwahiyo usikonde

Mariam ni mama wa KRISTO YESU hivyo anaweza kweli kukuombea kwa mwanae amini Amin amin
Mkuu hapo ni mama au mwana?
Yesu hana mama biblia inasema yesu alikuwako tangu mwanzo wa misingi ya ulimwengu kilicho fanyika pale ni yesu kuuvaa ubinadamu ili adhihirishe upendo wake kwa wanadamu, leo hii watu wengi wanasema mungu anatupenda ukiuliza alitufanyia nini tulianguka dhambini lakini bado yupo pamoja nasi hakutuacha hata akaja kutoka mbinguni kukaa nasi hivyo yeye hana mama alikuwako.

Je wewe mungu wako anaupendo? Je kama anaupendo tuambie alikufanyia nini? Au unasema tu unaupendo alafu hakuna kitu alicho kufanyia, lakini yesu anatupenda alituumba kwa mfano wake na hata baada ya sisi kuingia dhambini hakutuacha alikuja kukaa nasi na ame ahidi anaebda kuandaa makao ili alipo sisi tuwako.


Nina ndugu zangu wengi na marafiki zangu wengi ni wakatoliki lakini katika uhalisia ukatoliki umetengeneza vitu vingi vya uzushi ambavyo hata katika historia ya yesu na mitume wake kwenye biblia hawakuvifanya.


Yesu haku muabudu maria wala mitume, yesu hakutengeneza sanamu ya maria wala mitume, pia kanisa hili limetafuta sanamu bandia za muigizaji wa uhusika wa yesu na kuzifanya kama huyo ndio yesu yule halisi, vile vile kanisa hilo limefanya na kwa maria pia limechukua sanamu za muigizaji na kuanza kuliabudu haya yote ni uzushi na upotoshaji mkubwa wa wawtu wa mungu.
Weka vifungu vya bible
 
Back
Top Bottom