Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?
View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.
Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?
Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipate kufunguka macho.
Asanteni sana.
Maria ni mwanadamu wa kawaida, hana hadhi kuongea mbele za Mungu kwa ajili ya wanadamu wengine kwa sababu hakulipa deni lolote. Yesu Kristo pekee (ambaye ni Mungu) ndiye kafara ambalo Mungu alijifanyia yeye mwenyewe kwa ajili ya wanadamu kupitia kwa maombi, na chochote kama kiunganishi. Yesu Kristo ni Mungu aliyeuvaa mwili hivyo ni Mungu yule yule, na alipofanyika kafara ni kwamba alikuwa anatengeneza kafara yeye mwenyewe ili wanadamu wapitie kwa maombi, kwa wokovu na kwa kila communication. kwa maana hiyo, maraia hana hadhi pia kumwambia Yesu chochote kwa niaba ya wanadamu wengine kwa sababu Yesu ni Mungu. Maria alikuwa anamwambia hivyo Yesu akiwa katika mwili hapa duniani, mwili alioufanya wa kibinadamu, na alikuwa mama kwa kibinadamu na siku Yesu alipokufa na kupaa mbinguni baada ya kufufuka ndio mwisho wa ubinadamu wa Yesu hivyo maria hana hadhi.
kwanini tunasema maria hana hadhi? kwa sababu hakufanyika kafara, hakufa kwa ajili ya wanadamu, hakumwaga damu hata ya kujikwaa kidoleni tu kwa ajili ya wanadamu, hivyo ni ujinga mkubwa sana kumfanya mwombezi wakati hana mandate kumsogeza mwanadamu yeyote mbele za Mungu.
YOHANA 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi
MATENDO 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana
hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa
wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
YOHANA 14:13 Nanyi
mkiomba lo lote
kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote
kwa jina langu, nitalifanya.
hii ni mistari michache tu ambayo Yesu mwenyewe aliagiza kwamba hatuwezi kupata chochote tusipoomba kwa Jina lake, sasa wakatoliki wanamdharau Yesu wanaona bora waombe kwa maria. wanajilisha upepo.
MUNGU ametupatia wanadamu njia ya kuwasiliana naye, namna ya kufika kwake, shetani akaingiza njia anayoijua yeye ili wanadamu wapoteze muda mwingi kuomba bila majibu, na ndio maana hakuna mkatoliki mwenye uwezo kufukuza hata mchawi au pepo, na majority wanategemea waganga, wachawi na washirikika na bado wanaomba kwa maria wao, ninyi wenyewe mashahidi, mnajijua hamna Mungu moyoni, hamjawahi kumwona wala kuhisi, mnamsikia tu. wala Roho wake Mtakatifu hamjawahi kujaa, kanisa la kwanza matendo ya mitume walijaa Roho Mtakatifu na waliweka mikono juu ya watu waliookoka wakajawa na Roho Mtakatifu. ninyi sio tu kwamba mmeukataa wokovu, bali mmemkataa Roho Mtakatifu ambaye Yesu alisema bila huyo hatuwezi kufanya lolote, mnaamua muongozwe kwa mapokeo yaliyokufa na yasiyookoa. Mungu awasaidie.