Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipate kufunguka macho.

Asanteni sana.
 
Hakuna jina la Maria kwenye Biblia.
Acheni kuwapotosha watu.

Mathayo (Mat) 1:18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
 
Imani ni ufunuo kwa ajili ya watu fulani

Kama wakatoliki ndo wamefunuliwa hivyo na wewe hujafunuliwa bado hayo , basi yaache

Hata Neema ya ukristo tumefunuliwa wachache na ambao hawajafunuliwa hutuona sisi machizi kwahiyo usikonde

Mariam ni mama wa KRISTO YESU hivyo anaweza kweli kukuombea kwa mwanae amini Amin amin
 
Hii logic ya kukaa aidha upande wa kuume au hata mkono wa kushoto ipoje ?
Kwamba roho au miili ya wahusika haibadilli positions zao ? Kwamba wa kulia siku zote anabaki mkono wa kulia na wa kushoto hali kadhalika ?
Watu walioandika biblia kuna makosa mengi sana ya kiufundi walifanya.

Mfano: Huwezi kusema Mungu ni roho, halafu wakati huo huo ana MKONO WA KUUME na wa kushoto. Huo mkono unatokea wapi tena? Roho zina mikono?
 
Hakuna jina la Maria kwenye Biblia.
Acheni kuwapotosha watu.

Mathayo (Mat) 1:18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Maria ndiye Mariamu mkuu. Haya sasa turejee kwenye mada. Huyu Mariamu anayewaombea wakatoliki kwa mwanaye Yesu, yu wapi? Je, bado yupo hai?
 
Imani ni ufunuo kwa ajili ya watu fulani

Kama wakatoliki ndo wamefunuliwa hivyo na wewe hujafunuliwa bado hayo , basi yaache

Hata Neema ya ukristo tumefunuliwa wachache na ambao hawajafunuliwa hutuona sisi machizi kwahiyo usikonde

Mariam ni mama wa KRISTO YESU hivyo anaweza kweli kukuombea kwa mwanae amini Amin amin
Kwa hiyo mkuu hapa inabidi tuamini tu bila kuhoji kama vile wapagani wanavyoamini tunguli za sangoma?
 
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipatke kufunguka macho.

Asanteni sana.

Ni Yeye kawashika Kweli Kweli 😂🔥
 
Kuna imani zingine za kijinga sana unaweza ukacheka mpaka ukabubujikwa na machozi 😂😂😂

Maria na Yesu ni mizimu ya kiyahudi.

Cc: johnthebaptist Lucas Mwashambwa

KANISA MOJA TAKATIFU LA MITUME LA ASKOFU PENGO
Hakunaga Imani ya kijinga ila Mjinga ni yule anayejihusisha na Imani isiyomuhusu kabisa 😂😂😂
 
Wewe hauwezi kuzungumza na Mama akamueleze Baba kama unahitaji jambo fulani? Bikira Maria ndiye alimzaa Yesu, anamjua mwanaye na aliumia hata wakati anateswa msalabani, Anamfahamu vyema mwanae.Kwenye Harusi ya Kana baada ya Divai kuisha mbona hawakumuendea Yesu moja kwa moja bali walienda kwa mama yake ili akawaombee? Kuna ubaya gani kupitisha maombi yako kwa mama ili yamfikie Baba? Hususan kama una makosa fulani uliyatenda yanayokufanya mpaka unaogopa kwenda kwa Baba.Kuhusu kufa na kufufuka mbona wapo watakatifu wengi tu ambao walikufa miili ila roho zao zi hai, Na wanatuombea kila siku, mfano Yesu alipokuwa mlimani alitokewa na Manabii Musa na Eliya ambao walishakufa zamani, Mifano ni mingi ila kwa leo ngoja tuishie hapa.
 
Hakuna jina la Maria kwenye Biblia.
Acheni kuwapotosha watu.

Mathayo (Mat) 1:18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Mimi kwenye bible yangu hakuna Mathayo bali Mathew.Sijajua kama Maria si Mariamu/Mariam/Maryamu/Maria/Mary au vinginevyo.Je,nimeuziwa "baibl" fekero?
 
Back
Top Bottom