Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Yesu Kristo, kulingana na mafundisho ya Biblia, ni njia ya pekee ya kufikia Mungu Baba ,hakuna cha Maria wala mtakatifu yeyote. Katika Yohana 14:6, Yesu anasema:
"Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."
Hii inaonyesha kwamba Yesu ni mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu, akiunganisha uhusiano uliovunjika na dhambi.

Ni kweli kwamba Yesu mara nyingi aliwafundisha wafuasi wake kumwabudu na kumuomba Mungu Baba moja kwa moja. Kwa mfano:

Katika Mathayo 6:9, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake Sala ya Baba Yetu

"Basi, ninyi salini hivi, Baba yetu uliye mbinguni..."
Hii inaonyesha kwamba maombi yanaweza kuelekezwa kwa Baba moja kwa moja.

Katika Yohana 4:23, Yesu anaeleza kwamba waabuduo wa kweli watamwabudu Baba katika roho na kweli. Hii inaonyesha umuhimu wa uhusiano wa moja kwa moja kati ya muumini na Mungu Baba.

Yesu pia anafahamika kama Kuhani Mkuu wa agano jipya. Katika Waebrania 4:14-16, Yesu anatajwa kama Kuhani Mkuu ambaye anatuwezesha kupata neema mbele za Mungu. Hii inamaanisha kwamba ingawa waumini wanaweza kumuomba Baba moja kwa moja, Yesu ndiye anayefanikisha upatanisho huo.

Katika Yohana 10:30, Yesu anasema:
"Mimi na Baba tu umoja."
Maneno haya yanaonyesha kwamba kumuomba Yesu au Baba ni sawa kwa sababu wana uhusiano wa karibu kabisa. Kwa hivyo, wakati Wakristo wanapomuomba Mungu kupitia Yesu, hawampuuzilii Mungu Baba, bali wanaheshimu jukumu la Yesu kama mpatanishi.

Aya ni nyingi sana zipo
Hii itakuwa theolojia ya akina Mwamposa na Mzee wa Upako!
 
Wewe hauwezi kuzungumza na Mama akamueleze Baba kama unahitaji jambo fulani? Bikira Maria ndiye alimzaa Yesu, anamjua mwanaye na aliumia hata wakati anateswa msalabani, Anamfahamu vyema mwanae.Kwenye Harusi ya Kana baada ya Divai kuisha mbona hawakumuendea Yesu moja kwa moja bali walienda kwa mama yake ili akawaombee? Kuna ubaya gani kupitisha maombi yako kwa mama ili yamfikie Baba? Hususan kama una makosa fulani uliyatenda yanayokufanya mpaka unaogopa kwenda kwa Baba.Kuhusu kufa na kufufuka mbona wapo watakatifu wengi tu ambao walikufa miili ila roho zao zi hai, Na wanatuombea kila siku, mfano Yesu alipokuwa mlimani alitokewa na Manabii Musa na Eliya ambao walishakufa zamani, Mifano ni mingi ila kwa leo ngoja tuishie hapa.
Ila hiz imani hiz, ko Mungu Yesu hana neno mbele ya mama ake,
Haya bhan ngoja tuwa achie wenyewe
 
1. Kuna kifungu chochote kwenye biblia kinacholazimisha kuongea na Yesu kupitia kwa roho ya bikra Maria badala ya kuongea na Yesu moja kwa moja?

2. Tupe kifungu kwenye biblia kinachoidhinisha roho za wafu kutumika kuwaombea walio hai.
Kwani Tajiri alivyokuwa akimuomba Ibrahimu amtume Lazaro amtume kwake amburudishe maji kidogo alikuwa hai mwenye mwili? Je haijandikwa kwenye biblia ili hali walishafariki?Biblia inasema mambo yasiyoonekana ni dhahiri kuliko yanayo onekana
 
Watu wa dini mnapaswa kutambua kitu kimoja usidhihaki imani ya mtu mwingine Mungu hapendi na hajakutuma kufanya hivyo.Mimi siwezi kumdhihaki maombi ya walokole najua kuna watu wameombewa na wachungaji wa kilokole na wakapona,hivyo hivyo kwa Lutheran,Sabato na mengineyo. Maria ni mtumishi wa Mungu na Mungu alimchagua kwa kusudi hilo ,Mungu hajakuita wewe kudharau watumishi wake,au kuwahukumu kwa namna yeyote ile,hata kwa wenzetu waislamu Mungu hajakutuma wewe kuwadhika au kuwasema .Sababu Mungu ni Mungu wa watu wote
Hakuna Mkristo mwenye akili timamu anaweza mdharau Bikra Maria. Ila wengi tunachosema ni kuwa Bikra Maria hana uwezo wa kumwombea mtu kwa Yesu. Bikra Maria. Alipomzaa Yesu alimaliza jukumu lake. Alitumika kupitishia kuzaliwa Yesu. Baada ya hapo akabaki kama mama tu. Ndo maana huoni akizungumziwa tena katika Injili. Anywhere. Hajazungumziwa hata kidogo. Why? Alimaliza kazi yake.
 
Bikira Maria aliniombea mimi kwa Yesu na nikapata mahitaji yangu.Sijawahi kuomba kwake ombi langu likashindikana,mimi na akili zangu timamu narudia kusema.BIKIRA MARIA ALINIOMBEA KWA YESU KWA NA MAOMBI YANGU YAKAPATA KIBALI.Sishuhudii shuhuda ya mtu mwingine na shuhudia miujiza yangu niliyotendewa mimi mwenyewe
 
Yohana 14:13
Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
 
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc

Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipate kufunguka macho.

Asanteni sana.

Kwenye tourati hakuna popote neno BIKRA limetajwa huo ni uzushi wa Agano jipya.
Kwa wasiojua limetajwa YOUNG WOMAN
 
Unalazimisha ku u-define ukatoliki kwa kutumia ulokole. Hau-ujui undani wa ukatoliki.

Pia sio kazi yetu sisi wakatoliki kukufundusha kitu ambacho hauko tayari kukipokea; ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
kwa bahati nzuri, niujue au nisiujue ukatoliki haiongezi thamani yeyote ya maisha yangu, ila nikiujua ukristo halisi, ule wa Kitabu cha matendo ya mitume (ambao wakatoliki wako mbali nao kabisa) hapo ndio ningefaidika. kwa kukusaidia, mfano wa kukusaidie iwe ni kanisa la kwanza, lile limeandikwa kitabu cha matendo. JIfunze kwa Petro, YOhana, Mathayo, Marko, Paulo, stephano, filipo na wengine. usiangalie jengo, angalia theme ya ukristo wa kwanza ungekuwaje. kwa sababu kama ni jengo najua utakuja na hoja kwamba st.Peter pale vatican ilijengwa na aidha Petro au Paulo kwa hiyo kwa sababu mabaki ya jengo bado yapo basi katoliki ni kanisa la kwanza. mnajidanganya na kujilisha upepo. wakatoliki sio wakristo kabisa, kwa sababu zifuatazo ambazo ndio character halisi ya Mkristo.

1. Wakatoliki (sambamba na wasabato) hawaamini kuokoka. Lakini Yesu alikuja kuleta wokovu. ukisoma MATENDO 2:47 SUV ... wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. KUMBE, kanisa la kwanza watu walikuwa wakiokolewa, ila wakatoliki hamuokoki, mnaabudu dini.

2. Kanisa la kwanza lilijawa na Nguvu za Roho Mtakatifu. kanisa katoliki wanapinga ujazo wa Roho Mtakatifu. ukisoma Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. ukisoma pia MATENDO 19:3-6 3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. 5 Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.

3. WAKATOLIKI wanaomba kwa bikira maria na wafu. Yesu aliseme yeye peke yake ndiye njia kweli na uzima, na tukiomba tupitie JIna lake tu ndio maombi yetu yatafika.

4. Kanisa la kwanza, waliombea wagonjwa na wenye shida wakapona. Kanisa katoliki na hata wasabato, hata pepo tu hawawezi kuombea, kwa sababu hawana Nguvu za Mungu kufukuza pepo. kitu pekee ukiwaletea pepo watatoa sababu nyingi kujitetea na kuonyesha siku hizi sio za maombezi. (ijulikane, maombezi ninayoongelea hapa ni yale ya kitabu cha matendo ya mitume, sio haya maombezi ya manabii wa uongo na wauza maji na mafuta, matapeli wakubwa).

kuna mengi sana ambayo yananifanya niamini katoliki sio wakristo, kwa sababu hawana Kristo. mtu ataitwa Kristo kama akimpokea Kristo.

kwa sababu hizo na nyingi, kumfanya maria ni kitu chochote ni kujilisha upepo na kupoteza muda wakati shetani anakushtukiza akuchinje mwende wote motoni.
 
Upo nje ya mada kabisa, hizi ni chuki za wazi wazi
 
1. Kuna kifungu chochote kwenye biblia kinacholazimisha kuongea na Yesu kupitia kwa roho ya bikra Maria badala ya kuongea na Yesu moja kwa moja?

2. Tupe kifungu kwenye biblia kinachoidhinisha roho za wafu kutumika kuwaombea walio hai.
Hii ya mambo ya kifungu kifungu wakati wakatoliki wanayo mapokeo pia, hapo ndipo mnapoteana
 
Ugumu walio nao ni wakutengenezwa tangu wakiwa watoto wadogo. Kuchomoka kwenye hicho kifungo sio rahisi!
Noma sn
Hata waliochomoka ni Neema ya Mungu tu

Hapa ndo utaelewa ile wakorinto inayoongelea ,kutekwa nyara fikra,kuzungushiwa ngome ya elimu iliyojiinua kinyume na elimu ya Mungu
 
1. Kuna kifungu chochote kwenye biblia kinacholazimisha kuongea na Yesu kupitia kwa roho ya bikra Maria badala ya kuongea na Yesu moja kwa moja?

2. Tupe kifungu kwenye biblia kinachoidhinisha roho za wafu kutumika kuwaombea walio hai.
  • Ufunuo 5:8: "Na alipoitwaa kile kitabu, wale wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vikombe vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambazo ni maombi ya watakatifu."
  • Ufunuo 8:3-4: "Na malaika mwingine akaja, akasimama mbele ya madhabahu, akiwa na chetezo cha dhahabu; naye akapewa uvumba mwingi, ili aufanye pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi. Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu kutoka mkononi mwa malaika."
 
Noma sn
Hata waliochomoka ni Neema ya Mungu tu

Hapa ndo utaelewa ile wakorinto inayoongelea ,kutekwa nyara fikra,kuzungushiwa ngome ya elimu iliyojiinua kinyume na elimu ya Mungu
Haswaa Mimi ni miongoni mwa watu ambao Yesu aliingilia Kati kuning'oa kutoka kwenye huo utumwa. Nafurahia Uhuru ndani ya Kristo lakini kwa upande mwingine nikitafakari namna watu walivyoshikwa 'masikio' furaha inaingia shubiri😭
 
Back
Top Bottom