Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

Sio lazima wafanye promo za kuwaita waumini. Yako mambo mengi wanayoweza kuandaa vijana kupitia redio na tv na yakavuta wengi. Hata kama ibada inarushwa, basi audio na video ziwe na ubora unaofaa. Wakati mwingine ibada za mubashara sauti ni shida sana.

Kikubwa kanisa liwekeze kwenye ubora wa content kupitia media.
 
Liturugia imewahi kusaidia nini labda
 
nijikite kwenye ukongwe hapo, hakuna wakongwe kwenye dini kama Wayahudi, wao wamekuwa waaminifu kwenye dini mno, lakini dini haijawaokoa, wanakufa na wanaenda motoni kwasababu ni kwa kutumia dini hiyohiyo walimsumbua sana Yesu na waliwauwa mitume waliosambaza hata huu ukristo. Cha msingi, tuishi tukijua kwamba, dini haiokoi, Biblia inasema tunatakiwa kuokoka. kwa kua ukimkiri Yesu kwa kinywa chako na kuamini moyoni kwamba Mungu alimfufua katika wafu utaokoka, kwa moyo mtu huamini na kwa kinywa hukiri. tunatakiwa kuokoka, hizi dini ni NGOs tu ambazo tena zimesajiliwa kabisa kwenye secular government hiihii na zinaweza kufutwa au kurekebishwa, ila njia ya wokovu kwa Yesu Kristo ni moja tu, kuokoka ni lazima.
 
Unajua, binadamu tukiachwa bila mifumo hatutaweza kuwa sawa. Hivyo hizi taasisi za kiimani ni muhimu zikawepo. Tatizo serikali zinaruhusu usajili kila leo. Ifike muda taasisi zilizopo ziangaliwe upya na zipunguzwe ikibidi. Kisha pasiongezeke zingine. Na zitakazobaki ziwe na uhalisia katika kutumikia waumini wake.
 
sheria zipo, taasisi zinazokiuka sheria, zishughulikiwe. ni ngumu hata hivyo kucontol hizi taasisi, kama unawapa vibali waganga wa kienyeji na wapagani wafanye upagani wao wapendavyo (labda kwa sababu ndiko wanaend akuchukua tunguli wakati wa uchaguzi na kwenye vyeo vyao), utakuwa na sauti kuzuia mlipuko wa dini kweli?
 
Binafsi naona nje ya ibada za live, hivi vituo vya dini hazina maudhui mengine zaidi ya nyimbo aka videos. Labda uniambie Kuhani Musa, Mwamposa na hao wengine huonesha vipindi Gani vingine vya kijamii au tofauti nje ya kuhubiri neno na kucheza gospel music? Mimi nawashangaa TU wameshindwa kurusha matangazo yao Startimes!?
 
Bila shaka ni taasisi 2 tofauti zinazitoa vibali, maana uganga na dini havichangamani
 
Siyo maneno yangu mkuu.

Luka 9:23
Akawaambia wote, "mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate."
Sipingi neno la Mungu.Hata kwa madhehebu mengine pia huo msalaba ndio nguzo kuu na chanzo cha wokovu.Una lingine? Hamna content kubalini tu
 
ASizungumzii biashara bali namna gani Katoliki tumesongwa na vishawishi.

Sizungumzii biashara bali namna gani Katoliki tumesongwa na vishawishi.
Acha udhehebu hao wote ni wakristo mbona mimi ni mluther ila nikikosa kanisa karibu kama nipo mkoa au nchi nyingine naingia catolic safii kabisa, ok nikusaidie tu tumia azam kifurushi utakutana na chanel kibao za catolik ingawa mimi mpenzi wa dstv, ila jifunze kubadilika udhehebu aufai kwa dunia ya sasa sote ni wakristo
Sizungumzii biashara bali namna gani Katoliki tumesongwa na vishawishi.
 
‭‭Yohana 2:23
[23] Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya.

Kama ungeendelea kidogo katika somo tulilosoma leo ungekutana na huo mstari.

Ishara na miujiza inazalisha imani usibishe kitu usichokijua.

Kuhusu kujitangaza ni kama swali la mleta mada. Je? tutajitangaza katika lipi? Katika kulinadi kanisa au kumhubiri Kristo. Lazima tukubali kwamba kanisa limetulea lakini jukumu letu sio kumlinda papa Bali kumtangaza Kristo, kilele cha imani yetu lazima iwe wokovu maana yake Kristo alikufa kisha akafufuka katika hilo tumekombolewa na tuu warithi wa neema pamoja nayeye hivyo hatuna vifungo vya dogma wala kanisa tu watumwa wa Kristo katika kazi ya kuokoa mioyo iliyopotea.
 
Wakati wanaanzisha redio maria waliwavuta wasikilizaji wake kwa kuweka nyimbo za walokole, mwisho wakazitupilia mbali wakawa wawasikilizia nyimbo za kikatoliki na sala zao. Sasa redio haina wasikilizaji wengi
Acha uongo sidhan kama kuna Radio kwa sasa yenye Masafa mengi kwa sasa kama radio Maria.
 
Ni kweli, hakuna content za ajabu sana ila zilizo
Wakristo wengine vimeo sana. Wapotoshaji na wapigaji wa wazi. Mbali na upigaji ni matapeli wa kiimani na waumizao wale wanaowaendea kupata huduma zao. Sasa unaanzaje kuchangamana na hawa?
 
Wewe ukitaka kuhama, hama! Ila siyo kulazimisha Kanisa Katoliki liishi kama makanisa/madhehebu mengine.

Kama ni hayo mahubiri, huwa yanarushwa mara nyingi tu na Mafrateli na Mashemasi wa seminari kuu mbalimbali; Mapadre mfano Padre Titus Amigu wamekuwa wana vipindi vingi vya mafundisho ya Kanisa; na hata Maaskofu huwa wanatoa mafunzo ya Kanisa kupitia redio na pia television! Mfano mzuri ni Askofu mstaafu Kilaini, Askofu Mstaafu Lebulu, na wengineo wengi!

Ni bahati mbaya tu umekariri muda wote ni sala. Na bila shaka unataka na Kanisa Katoliki nalo liwe na wakina Mwamposa wake, ili baadaye waote mapembe; na hivyo kuleta mvurugano kwenye Kanisa! Kwa hilo, sahau.
 
Waebrania 11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.


Kama imani yako inajengwa juu ya ishara na miujiza, unahitaji kuomba sana msaada wa Mungu akufunulie kweli yake.

Yohana 20:29
Yesu akamwambia, "Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.


Sidhani kama kuna haja ya kumwongelea Papa, lakini kama Mkristu Mkatoliki unapaswa kujua Papa ni khalifa (successor) wa Mtume Petro.

Kanisa lina vyanzo vitatu vya mafundisho:
  • Maandiko Matakatifu (Holy Scriptures)
  • Mapokeo Matakatifu (Holy Traditions)
  • Kiti cha Mtume Petro (Papacy).
Sijui hata unaelewa ulichokiandika. Anyway...

Bwana awe nasi sote.
 
Uinjilishaji pia kutembeza sanamu ya bikira Maria.
 
Mbona hayo madhehehu mengine unayosema yana ubunifu hayatembezi msalaba na hujawashauri nao watembeze msalaba na sanamu ya bikira Maria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…