Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

Bila shaka ni taasisi 2 tofauti zinazitoa vibali, maana uganga na dini havichangamani
yaani hoja ni kwamba, serikali hiyo hiyo hata kama ina taasisi mbalimbali zenye kutoa vibali, lakini ni serikali hiyohiyo. inaruhusu mtu kuamua kuwa mpagani, mganga wa kienyeji kabisa na inampa leseni ya uganga wa kichawi, sasa kama inatoa hadi leseni kwa waganga, je? itatumia hoja gani kuzuia watu kufungua taasisi za kidini hata kama ni za ajabuajabu? serikali imeshakuwa mtumwa.
 
Sizungumzii biashara bali namna gani Katoliki tumesongwa na vishawishi.
Ondoka katoliki,Huku hakuna kubembeleza wewe nenda kwa mwamposa

Katoliki hawamfuati padri au askofu kanisani

Watu wanaenda kusali na yeyote Padri anasalisha
 
Achana na dini,njoo kwa Yesu kuna neema ajabu.
 
Hii ni sawa na kusema serikali isipobadirika shule za serikali zitakosa wanafunzi.
 
Ondoka katoliki,Huku hakuna kubembeleza wewe nenda kwa mwamposa

Katoliki hawamfuati padri au askofu kanisani

Watu wanaenda kusali na yeyote Padri anasalisha
Kanisa linajua kuwa waumini wake wanapotelea huko makanisa yanayojiita ya kiroho. Sidhani kama wako kimya. Kwa wao kutokuwa kimya haimaanishi tusiendelee kuwakumbusha
 
Liturugia imewahi kusaidia nini labda
liturugia ni mfumo wa uendeshaji wa ibada mmoja, kwamba leo kanisa lilipo sehemu a na lililopo sehemu b na c wote sala na mafundisho yatakuwa ya namna moja.
kwangu imekuwa msaada wq urahisi wa kuabudu na kujifunza kwa urahisi mafundisho juu ya Mungu.
 
Waumini wakitoroka msiwalaumu.
Kama kuna mtu 'anatoroka' just kwa sababu ya kuona TV, basi nadhani atoroke tu. Uzuri Ukatoliki hauamini sana katika mashindano bali unafundishwa imani ya Kanisa na unaongozwa namna ya kuiishi, kuitumikia na kudumu katika imani hiyo. TV ni njia ya kiteknolojia ya kutekeleza hayo, lakini haiondoi nafasi ya muumini kulitumikia Kanisa hata katika mazingira ambayo teknolojia hiyo haifiki. Sasa ukiwa unatetereshwa na TV, basi hakuna njia ya kukusaidia zaidi ya kukuombea
 
Kwa kuwa hutaki kujua matumizi ya teknolojia hata katika imani, basi wewe ndio wa kuombewa. Fikiria pasingekuwepo na kipaza sauti tu
 
Kwenye radio maria mwenyewe nashangaaga sana, like how mtu afungulie radio ili asali,
Kama nataka kusali nazima kila kitu nakaa comfortable alone nasali sio nianze kusikiliza radio mara mitambo iingilia niahirishe,

Wajaribu kujikita kwenye kuufundisha ukatoliki, na kutoa neno kwa kufuata ukatoliki ,
Wapunguze unnecessary sala kwa radio, hakuna anaesikiliza
 
Wakati wanaanzisha redio maria waliwavuta wasikilizaji wake kwa kuweka nyimbo za walokole, mwisho wakazitupilia mbali wakawa wawasikilizia nyimbo za kikatoliki na sala zao. Sasa redio haina wasikilizaji wengi
Wewe wasema
 
Nafarijika sana ninapotazama EWTN na kusikiliza na kusali rozari na radio maria fm
 
Kwa hiyo unataka Radio Maria watangaze vipindi gani kwa mfano?
 
Utakuwa hujafuatilia kwa undani au umesikia kwa jirani tu! Tumaini TV mbona iko vizuri sana tu! Umeshawahi kufuatilia EWTN (Eternal Word Television Network)?
 
Kuna mashindano ?

Anyway kama umeona kuna uhitaji / gap in the market unaweza kuanzisha station / kipindi chenye hayo maudhui
 
Kwa kuwa hutaki kujua matumizi ya teknolojia hata katika imani, basi wewe ndio wa kuombewa. Fikiria pasingekuwepo na kipaza sauti tu
Wamisionari hawakutumia vipaza sauti na bado walifikisha Injili hadi Karema mkoani Katavi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…