ndugu yangu, wala sisemi mimi, nimeweka mistari ya Biblia hapo, nakuwekea tena ili ubishane nayo.
Wagalatia 6:5 inasema kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe na Warumi 14:12 inasema Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.
Anaposema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe manake kila mtu atakuwa accountable kwa dhambi zake mwenyewe zile ambazo amekaidi kama wengi wanavyofanya, hajataka kutubu. Yesu alikuja kulipa garama ya dhambi, na kwa kufanya hivyo Yesu haimaanishi basi dunia yote imeshasamehewa, hapana, yule tu anayezipeleka dhambi zake kwa Yesu ndiye anasamehewa, ndio hukumu yake ya dhambi inafutwa, wale wenye shingo ngumu wanabaki na dhambi zao na watakuwa accountable personally. na hii ndio sababu Yesu alisema kwamba hiii ndio itakuwa hukumu kwamba Nuru imekuja duniani lakini watu wanaikimbia nuru wanapenda giza.
nakuonea huruma sana unapoujali sana huu mwili, unasema suala la ibada ya wafu sio masihara? hiki ndicho kifungo ambacho nilikuwa nasema wakatoliki mmefungwa, ni kifungo kikubwa kuamini kwamba siku ile utakapokufa padre atakuombea na utasamehewa dhambi zako, pambana na mistari nimekuwekea hapo juu, naw ewe kama unayo kinzani niwekee, haujaweka hata mmoja, why? unasema mtu akifa hata kidole tu kitachukuliwa aombewe au azikwe, na kama msipokipata manake nini? wale waliopotea na ndege ya malaysia mmeshapata kidole hata kimoja? mtu akiliwa na mamba mamba akaenda zake kwenye kina cha maji huko mtamfanya nini au mtasubiri ajisaidie haja kubwa ili mchukue kinyesi cha mamba mkakizike?
hiki ndicho kifungo watu wengi wamefungwa, na hakipo kwenye Biblia. ninyi mnaosoma hapa jueni kuwa,
1. Yesu Kristo alikufa, akalipa deni la dhambi, ukitubu anazifuta, usipotubu unabaki nazo.
2. Mungu ameweka nafasi ya mtu kuishi, ukiwa hai tengeneza mambo yako na Mungu,ukifa ndio deadline yako ya kutubu, huko utakakoenda badala ya Yesu Kristo kubeba dhambi zako utakuwa umeshachelewa utazibeba wewe mwenyewe na utakuwa accountable personally kwasababu aliyekuja azichukue haukumpatia mizigo yako hiyo.
3. Huu mwili ni udongo tu, roho ndio itiayo uzima mwili haufai kitu. ukifa unaoza unakuwa udongo tu, kinachotafutwa kuokolewa ni roho yako, huko ndiko kwenye dhambi, na huko ndiyo kwa kusafishwa dhambi, huko rohoni ndiko kunakotubu, ukitubu dhambi na kuziacha roho inakuwa safi, na hata ukifa hapa utaoza ila roho yako itapona. ukifa na dhambi, ni hasara.
4. Kumwombea mtu akiwa amekufa kwamba asamehewe dhambi haipo kwenye Neno la Mungu, Mitume hawajawahi kufanya hivyo, na Yesu hakuagiza hivyo, ni kitu tu kimetungwa na wanadamu, kama vile tu papa anavyotaka kuingiza kuombea mashoga, miaka ijayo hili nalo mtakuwa nalo kwenye ibada zenu.
5. unaweza kumwombea mtu akiwa hai kama ametenda dhambi, Mungu akamsamehe na kumponya ugonjwa wake, ila ni pale atakapotubu yeye na kukiri, msamaha wa dhambi unatokana na kukiri kuwa umetenda dhambi, ukifa huwezi kukiri, imeisha hiyo.
6. wengi hamtaelewa hili hadi siku mtakapofunguka macho na kukimbia kuabudu hiyo dini. Mungu awasaidie.