Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

ndugu yangu, wala sisemi mimi, nimeweka mistari ya Biblia hapo, nakuwekea tena ili ubishane nayo.

Wagalatia 6:5 inasema kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe na Warumi 14:12 inasema Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Anaposema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe manake kila mtu atakuwa accountable kwa dhambi zake mwenyewe zile ambazo amekaidi kama wengi wanavyofanya, hajataka kutubu. Yesu alikuja kulipa garama ya dhambi, na kwa kufanya hivyo Yesu haimaanishi basi dunia yote imeshasamehewa, hapana, yule tu anayezipeleka dhambi zake kwa Yesu ndiye anasamehewa, ndio hukumu yake ya dhambi inafutwa, wale wenye shingo ngumu wanabaki na dhambi zao na watakuwa accountable personally. na hii ndio sababu Yesu alisema kwamba hiii ndio itakuwa hukumu kwamba Nuru imekuja duniani lakini watu wanaikimbia nuru wanapenda giza.

nakuonea huruma sana unapoujali sana huu mwili, unasema suala la ibada ya wafu sio masihara? hiki ndicho kifungo ambacho nilikuwa nasema wakatoliki mmefungwa, ni kifungo kikubwa kuamini kwamba siku ile utakapokufa padre atakuombea na utasamehewa dhambi zako, pambana na mistari nimekuwekea hapo juu, naw ewe kama unayo kinzani niwekee, haujaweka hata mmoja, why? unasema mtu akifa hata kidole tu kitachukuliwa aombewe au azikwe, na kama msipokipata manake nini? wale waliopotea na ndege ya malaysia mmeshapata kidole hata kimoja? mtu akiliwa na mamba mamba akaenda zake kwenye kina cha maji huko mtamfanya nini au mtasubiri ajisaidie haja kubwa ili mchukue kinyesi cha mamba mkakizike?

hiki ndicho kifungo watu wengi wamefungwa, na hakipo kwenye Biblia. ninyi mnaosoma hapa jueni kuwa,

1. Yesu Kristo alikufa, akalipa deni la dhambi, ukitubu anazifuta, usipotubu unabaki nazo.

2. Mungu ameweka nafasi ya mtu kuishi, ukiwa hai tengeneza mambo yako na Mungu,ukifa ndio deadline yako ya kutubu, huko utakakoenda badala ya Yesu Kristo kubeba dhambi zako utakuwa umeshachelewa utazibeba wewe mwenyewe na utakuwa accountable personally kwasababu aliyekuja azichukue haukumpatia mizigo yako hiyo.

3. Huu mwili ni udongo tu, roho ndio itiayo uzima mwili haufai kitu. ukifa unaoza unakuwa udongo tu, kinachotafutwa kuokolewa ni roho yako, huko ndiko kwenye dhambi, na huko ndiyo kwa kusafishwa dhambi, huko rohoni ndiko kunakotubu, ukitubu dhambi na kuziacha roho inakuwa safi, na hata ukifa hapa utaoza ila roho yako itapona. ukifa na dhambi, ni hasara.

4. Kumwombea mtu akiwa amekufa kwamba asamehewe dhambi haipo kwenye Neno la Mungu, Mitume hawajawahi kufanya hivyo, na Yesu hakuagiza hivyo, ni kitu tu kimetungwa na wanadamu, kama vile tu papa anavyotaka kuingiza kuombea mashoga, miaka ijayo hili nalo mtakuwa nalo kwenye ibada zenu.

5. unaweza kumwombea mtu akiwa hai kama ametenda dhambi, Mungu akamsamehe na kumponya ugonjwa wake, ila ni pale atakapotubu yeye na kukiri, msamaha wa dhambi unatokana na kukiri kuwa umetenda dhambi, ukifa huwezi kukiri, imeisha hiyo.

6. wengi hamtaelewa hili hadi siku mtakapofunguka macho na kukimbia kuabudu hiyo dini. Mungu awasaidie.
Kumbuka unaandika haya yote kwa kunukuu Biblia iliyoandaliwa na Wakatoliki 😁
 
Wakati Katoliki inaandaa biblia, ilijua yote hayo unayoshikia bango. Nakushauri ukaungane na waamini wenzio kutafuta biblia yenu mpya kisha uje na hoja zako.
Pia kama hauna heshima kwa mwili hauwezi kuwa na roho yenye heshima. Mwili hubeba roho na nafsi. Hivyo wakati wa kutamatisha safari ya mwanadamu, kilichohifadhi roho na nafsi nacho kipewe heshima
ndugu yangu, hata kama yeyote yule aliandika Biblia, kama kweli yupo, naamini atakuwa alitumika tu kama chombo, na ingemsaidia sana kama angeihifadhi na kuifuata basi, kuliko kuiandika na akawa wa kwanza kutupwa. yote katika yote, uandishi wa Biblia au hata kusoma uwe na degree zote, kama hauna Roho Mtakatifu wa kukusaidia kuitafsiri, hamna kitu kabisa. na hii ndio maana kila dhehebu lina watu waliosoma ila kwa mlengo wa dhehebu lao tu, wana phd na hawafiki muafaka mmoja kwasababu determinant factor ni uwepo wa Roho Mtakatifu, yeye sio tu anaweza kukutafsiria hiyo Biblia ukaelewa bali hata yale yasiyoandikwa anaweza akakuambia kipi dhambi na kipi sio dhambi.

ni ajabu kwamba, kiburi kwamba ninyi ndio mliandika Biblia ndicho kinachowafanya msiokoke, bila kusahau kuwa Biblia kiuhalisia aliiandika Mungu mwenyewe kutumia watu wake, wakatoliki kama waliandika waliokota tu yale yaliyokwisha aandikwa na kian Paulo, petro na mitume wengine, na agano la kale kuchukua yale yaliyoko kwenye uyahudi ambayo yapo hadi leo vilevile, sasa sijui nini mliandika nini cha kujivunia.
 
Kumbuka unaandika haya yote kwa kunukuu Biblia iliyoandaliwa na Wakatoliki 😁
nijuavyo, Biblia ilikuwepo kabla ya ukatoliki, na hata kama wakatoliki waliokoteza na kuweka pamoja, Mungu anaweza kumtumia yeyote hata mwovu kufanikisha mambo yake, kwahiyo hicho hakitakuwa kitu cha ajabu. ninachokushaurini, hata kama tuseme mlitumiwa kuviweka pamoja (though viliexist before you existed) basi yafuateni hayo yaliyoandikwa ndio yatawasaidia. kuliko wageni kuja kuponea hayo maandiko ninyi mkabaki vilevile.

pia, Kitabu cha Isaya mfano, unaposema ninyi mlikiandika, unamaana gani (kama mfano tu), najua hicho ni kitabu cha manabii, wayahudi awali walikuwa wanafuata torati na manabii, na Isaya kilikuwa kimojawapo ya kitabu cha Manabii,kimekuwepo hata kabla ya Yesu, sasa ninyi kuja kukichukua na kukihifadhi, unamaana mlikibadilisha mkaandika chenu au ni kile kile ambacho hata wayahudi walihifadhi kitabu hicho kama mojawapo ya vitabu vya manabii? kama jibu ni negative, mna nini cha kujivunia sasa?
 
Unaelewa tofauti kati ya 'kuandaliwa' na hiyo 'kuandikwa' uliyoichomekea? Ndio maana nasisitiza kwamba ili tuelewane ni lazima kuwepo na standard fulani ya elimu. Mapadri wa Katoliki wanasoma miaka minne ya Falsafa na miaka mitatu au minne ya Theolojia. Anakuja mtu hata hajasoma, amekaririshwa mstari ila anaelezea utadhani ametunga Biblia yeye
 
ndugu yangu, hata kama yeyote yule aliandika Biblia, kama kweli yupo, naamini atakuwa alitumika tu kama chombo, na ingemsaidia sana kama angeihifadhi na kuifuata basi, kuliko kuiandika na akawa wa kwanza kutupwa. yote katika yote, uandishi wa Biblia au hata kusoma uwe na degree zote, kama hauna Roho Mtakatifu wa kukusaidia kuitafsiri, hamna kitu kabisa.
Uwe mpole hivyo hivyo maana ni dhahiri hujui hata historia ya Biblia. Mdadisi mchungaji wako walau aliyesoma Diploma ya Theolojia, tena umsisitize akueleze ukweli
 
Unaelewa tofauti kati ya 'kuandaliwa' na hiyo 'kuandikwa' uliyoichomekea? Ndio maana nasisitiza kwamba ili tuelewane ni lazima kuwepo na standard fulani ya elimu. Mapadri wa Katoliki wanasoma miaka minne ya Falsafa na miaka mitatu au minne ya Theolojia. Anakuja mtu hata hajasoma, amekaririshwa mstari ila anaelezea utadhani ametunga Biblia yeye
ndugu yangu, kama nini hamkuandika, bali mliandaa, vyovyote vile, ninavyojua ni kwamba, kabla ya Yesu Kristo, wayahudi walikuwa wanatumia torati na manabii, manabii maana yake kulikuwa na vitabu vingi tu vya manabii tunavyovijua leo (Yeremia, isaya, zaburi n.k) walikuwa wanatumia.

baada ya Yesu kupaa, kanisa likazaliwa, mitume waliandika hizo injili, hilo unalijua. wakati injili hizo zinaandikwa, kiukweli ni kwamba Kanisa lilikuwa zuri sana, kabla uharibifu haijaingia.

shida ilikuja miaka mia kadhaa baada ya mitume hao wote kufariki, kanisa lilipoingiliwa, ndipo mkaingiza mambo mengi ya kibinadamu, hata hivyo mitume walionya sana kuhusu hilo, paulo hadi alilia kwamba kuna mbwamwitu watakuja kulirarua kanisa.

sasa, kama torati na manabii zilishakuwepo, na zipo vilevile hamkuwa na uwezo kuzibadilisha maandishi yake, na kama njili ilikuwepo hamkuandaa ninyi bali mliihifadhi tu au nisema mlicompile ninyi tu, kujisifu kwenu kuhusiana na theme yake kunatoka wapi? tunachotakiwa kufanya ni kumshukuru Mungu kwa kuwatumia ninyi kufanay compilation yakitu mlichokikuta, tu, hapo tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu, hata kama shida ni kwamba tunahuzunika kwamba Mungu alilitumia kanisa lenu kuhifadhi ila waliokuja kufaidika ni wengine,ninyi hata hamfuati yale mliyohifadhi.

I am aware na unachoandika, unalenga kwamba, yalishakuwepo maandiko mengi mno hasa huko kwenye injili na ninyi ndio mlichambua yapi muyahifadhi kwenye hii Bible na yepi msiyajumuishe. doubt kama hiyo imeexist sana, na hapo ndipo tunapomhitaji Roho Mtakatifu ambaye angeweza kumfunua Yesu Kristo kwetu kwa namna yeyote ambayo Mungu angeamua, hata ninyi msingefanya compilation wangefanya wangine, haustahili kabisa kuchukua hiyo kama credit, you do not own anything, Mungu ndiye ana own kila kitu, na usiwe na kiburi kwa ajili ya kazi waliyofanya wenzako ambao wameshakuwa mavumbi, fanya wewe sasaivi ili kujisifu kwako kutokane na yale uliyoyafanya wewe binafsi.
 
baada ya Yesu kupaa, kanisa likazaliwa, mitume waliandika hizo injili, hilo unalijua. wakati injili hizo zinaandikwa, kiukweli ni kwamba Kanisa lilikuwa zuri sana, kabla uharibifu haijaingia.
Nimebold hapo, Kanisa Katoliki ni Kanisa Takatifu la Mitume
Kwa hiyo upo sahihi kabisa kuwa mitume waliiandika hiyo injili. Mitume
 
Nimebold hapo, Kanisa Katoliki ni Kanisa Takatifu la Mitume
Kwa hiyo upo sahihi kabisa kuwa mitume waliiandika hiyo injili. Mitume
ndugu yangu, hivyo ndivyo mnavyojiita, lakini ukweli usemwe, jipime mwenyewe, mnasali kama vile mitume walivyokuwa wanasali? JIBU NI HAPANA. hapo awali nilikuwekea maeneo machache tu ya kuwalinganisha na kanisa la mitume, na hakuna hata kimoja mnacholingana nacho, nini ni kitu kingine kabisa, hamkai kwenye mzani wa kanisa takatifu la mitume. angalia hata kwenye suala moja tu la kuamini ujazo wa Roho mtakatifu, ninyi mnaukimbia, mitume walihubiri wokovu, ninyi mnapinga. angalia mfano haya ya Roho kama hata moja linatendeka kwenu kama walivyofanay kina PETRO, PAULO, YOHANA na wengine.

1. KUNENA KWA LUGHA. kila aliyejazwa Roho Mtakatifu kwenye kitabu cha Matendo ya mitume, alinena kwa Lugha, na wale ambao hawakunena waliwekewa mikono ili wanene. Marko 16:17-18 "Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya,..." sasa tuambie ni padre gani ulishawahi kumwona ananena kwa lugha? au mkatoliki gani anene kwa lugha kama hajafukuzwa ukatoliki siku hiyohiyo? why? MATENDO 19:1 -10 inasema, Ikawa Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso, akakutana na wanafunzi kadhaa wa kadhaa huko, akawauliza, je? mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini? wakamjibu la hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. akawauliza basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? wakasema kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, kyaani Yesu. waliosikia haya wakabatizwa kwa Jina la Bwana Yesu. na Paulo alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao, wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri. sasa tueleze, ulishawahi kuona wapi Padre ana dalili yeyote kama hii? tusijidanganye, bila kujazwa Roho kwa namna hii,hauna Mungu. na huwezi pata kama haujaokoka, na kama dini yako inabeza kuokoka manake wote kuanzia viongozi hadi muumini hamna Mungu, ila mna dini.

2. ROHO MTAKATIFU ANADHIHIRISHWA PIA KWA MATUNDA YAKE. ila hiyo haimaanishi kwamba hutakiwi kunena, unalazimika kujazwa ila tutajua kama bado amekaa ndani yako au ameshakuacha kwa kuangalia matunda yako. yapo Wagalatia 5:22.

3. Wakorintho 12 kuna karama za Roho Mtakatifu. 1Wakorintho 12, ndani yake tutajie ipi ulishawahi kuiona kwa padre yeyote, au mkatoliki yeyote (ukiondoa wale wachache karismatic).
 
Nimebold hapo, Kanisa Katoliki ni Kanisa Takatifu la Mitume
Kwa hiyo upo sahihi kabisa kuwa mitume waliiandika hiyo injili. Mitume
nikuulize kitu kimoja tu walichofanay mitume, au kilichofanyika kwenye kanisa la kwanza lile la mitume, wao waliombea watu, walinena kwa lugha, waliongozwa na Roho, ninyi wakatoliki wa leo mnayafanay hayo?

kwani, kanisa la mitume ni jengo lile lililojengwa pale vatican st.peter (mtakatifu petro) au ni kanisa la kiroho? kwa uelewa wako.
 
1. KUNENA KWA LUGHA. kila aliyejazwa Roho Mtakatifu kwenye kitabu cha Matendo ya mitume, alinena kwa Lugha, na wale ambao hawakunena waliwekewa mikono ili wanene.
Mitume walinena kwa lugha na watu wa mataifa tofauti kila mmoja akasikia kwa lugha yake na wakaelewa ujumbe. Kwa sasa walokole na waprotestant wengine mnachofanya ni kinyume chake, kwamba wanaopaswa kupata ujumbe hawaelewi mnachoongea 😁 😁😁

Mdo 2:7-11
7 Wakastaajabu sana, wakasema, “Hawa wote wanaozungumza ni Wagalilaya. 8 Imekuwaje basi tunawasikia wakinena lugha ya kila mmoja wetu? 9 Hapa kuna Waparthi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, 10 Frigia, Pom filia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi. 11 Watu wen gine wametoka Krete na Uarabuni. Sisi sote tunasikia watu hawa wakisema katika lugha zetu wenyewe mambo makuu ya ajabu aliyofa nya Mungu.”
 
nikuulize kitu kimoja tu walichofanay mitume, au kilichofanyika kwenye kanisa la kwanza lile la mitume, wao waliombea watu, walinena kwa lugha, waliongozwa na Roho, ninyi wakatoliki wa leo mnayafanay hayo?
Wakatoliki
1. Wanaombea watu
2. Wanaongozwa na Roho Mtakatifu
3. Hawaneni kwa lugha zisizoeleweka kwa walengwa. Wanafikisha ujumbe kwa lengo la kuuwezesha ufike kwa mlengwa
 
Wakatoliki
1. Wanaombea watu
2. Wanaongozwa na Roho Mtakatifu
3. Hawaneni kwa lugha zisizoeleweka kwa walengwa. Wanafikisha ujumbe kwa lengo la kuuwezesha ufike kwa mlengwa
nauliza hivii, wananena kwa lugha kama vile walivyofanya kanisa la kwanza? jibu hilo kwanza.
 
Mitume walinena kwa lugha na watu wa mataifa tofauti kila mmoja akasikia kwa lugha yake na wakaelewa ujumbe. Kwa sasa walokole na waprotestant wengine mnachofanya ni kinyume chake, kwamba wanaopaswa kupata ujumbe hawaelewi mnachoongea 😁 😁😁

Mdo 2:7-11
7 Wakastaajabu sana, wakasema, “Hawa wote wanaozungumza ni Wagalilaya. 8 Imekuwaje basi tunawasikia wakinena lugha ya kila mmoja wetu? 9 Hapa kuna Waparthi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, 10 Frigia, Pom filia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi. 11 Watu wen gine wametoka Krete na Uarabuni. Sisi sote tunasikia watu hawa wakisema katika lugha zetu wenyewe mambo makuu ya ajabu aliyofa nya Mungu.”
soma Matendo 19:1-10 halafu urudi uone kama unakijua unachoongea.
 
Ukweli ni kwamba nipo home naperuzi stesheni za TV. Ukija clouds unakutana na chomoza, ukurudi chanel ten yupo Mwamposa. TVE yupo kuhani Musa. Wasafi yupo tena Mwamposa. Naperuzi zaidi nakutana na Upendo TV ya walutheri. Sasa Jumapili natoka kanisani kazi yangu ni kutazama maudhui ya madhehebu mengine tu? TV tumaini mmeshindwa kuingia DStv? Hata hivyo content mnazo?

Ukirudi kwenye redio ni yaleyale. Usiku redio zote zimeshikwa na hawa walokole. Namaanisha almost zote, tena hadi alfajiri. Ukija redio Tumaini na redio Maria ni sala %80. Hivi, ni nani anakaa au yuko nyumbani aache kufanya pilika za nyumani atulie kufuatilia sala redioni? Hata hao wanaoongoza sala redioni wametulia sehemu. Badilikeni

Waumini wakitoroka msiwalaumu. Kanisa katoliki ni kongwe kweli ila ifike sehemu mabadiliko, hasa kwenye uinjilishaji yawepo. Watu/waumini wanataka content.

Kanisa halijakosa waumini wenye karama za kuhubiri. Kwa nini wasipewe nafasi kwenye media? Kanisa halijakosa waumini wenye uwezo bunifu kwenye vipindi/maudhui. Mnatengeneza mazingira gani kuwawezesha hawa.

Niishie hapa kwa leo.
Makatoliki tupo hivi;
Ukijisikia kuhamia ukatoliki, wewe mwenyewe tafuta kanisa lilipo na unajieleza nia yako, then utafuata taratibu za huko kwa kadiri utakavyoelekezwa. Hakuna mtu atakuhubiria njiani uhamie huko. The same to redio na TV, tunazo zetu, wewe mwenyewe tafuta king'amuzi chenye redio au TV za kikatoliki then hamia huko. Haya mambo ya kusema tukufuate wewe huko DSTV, maana yake ukatoliki ndo una imani na wewe, badala ya wewe kuwa na imani na ukatoliki..!!
 
Ukweli ni kwamba nipo home naperuzi stesheni za TV. Ukija clouds unakutana na chomoza, ukurudi chanel ten yupo Mwamposa. TVE yupo kuhani Musa. Wasafi yupo tena Mwamposa. Naperuzi zaidi nakutana na Upendo TV ya walutheri. Sasa Jumapili natoka kanisani kazi yangu ni kutazama maudhui ya madhehebu mengine tu? TV tumaini mmeshindwa kuingia DStv? Hata hivyo content mnazo?

Ukirudi kwenye redio ni yaleyale. Usiku redio zote zimeshikwa na hawa walokole. Namaanisha almost zote, tena hadi alfajiri. Ukija redio Tumaini na redio Maria ni sala %80. Hivi, ni nani anakaa au yuko nyumbani aache kufanya pilika za nyumani atulie kufuatilia sala redioni? Hata hao wanaoongoza sala redioni wametulia sehemu. Badilikeni

Waumini wakitoroka msiwalaumu. Kanisa katoliki ni kongwe kweli ila ifike sehemu mabadiliko, hasa kwenye uinjilishaji yawepo. Watu/waumini wanataka content.

Kanisa halijakosa waumini wenye karama za kuhubiri. Kwa nini wasipewe nafasi kwenye media? Kanisa halijakosa waumini wenye uwezo bunifu kwenye vipindi/maudhui. Mnatengeneza mazingira gani kuwawezesha hawa.

Niishie hapa kwa leo.
Usifananishe wakatoliki na dini za kitapeli/wajasiliamali
 
soma Matendo 19:1-10 halafu urudi uone kama unakijua unachoongea.
Mimi ninanukuu vifungu na kuviweka hapa ili wote waone hoja. Wewe unasema niende nikasome kifungu; kwani ukikiweka hapa ukajenga hoja kuna ubaya gani? 😁😁😁
 
Back
Top Bottom