Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

nauliza hivii, wananena kwa lugha kama vile walivyofanya kanisa la kwanza? jibu hilo kwanza.
Kwa sasa neno la Mungu limetafsiriwa kwa karibu lugha zote kubwa, kwa hiyo yeyote anayehitaji kulisikiliza hana kikwazo cha lugha. Mitume walinena kwa lugha ili kuwawezesha Waparthi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, Frigia, Pomfilia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi wapate kusikia na kufuata neno hilo. Inawezekana hauelewi lengo la kunena kwa lugha walikofanya Mitume, ndio maana kwa sasa unanena lugha ambayo wewe mnenaji na anayesikiliza wote hamuielewi na hamuelewi maudhui yake
 
Uinjilishaji siyo kuhubiri tu.

Yakiwemo mahubiri; imani hujengwa na vitu vingi: sala, kwaya, historia ya Kanisa, kuelezea mafundisho mbalimbali, kujifunza maisha ya Watakatifu, n.k.

Haya yote utayapata Kanisani, kwenye media za Kanisa, Jumuia Ndogondogo za Kikatoliki, n.k. Imani ya Ukatoliki, na Ukristu kwa ujumla, haikujengwa kwenye miujiza na matangazo.
Infact Kristu alipotenda miujiza, ukiacha ule aliowaambia wakajioneshe kwa viongozi wa dini, mara zote aliwasisitiza wasimuambie mtu. Maana imani haijengwi kwenye miujiza, bali msalaba.
Quest ya muulizaji ni kuhusu aagizo la Yesu mwenyewe hapa chini.
👇
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; ”
— Mathayo 28:19 (Biblia Takatifu)
 
Binafsi naona nje ya ibada za live, hivi vituo vya dini hazina maudhui mengine zaidi ya nyimbo aka videos. Labda uniambie Kuhani Musa, Mwamposa na hao wengine huonesha vipindi Gani vingine vya kijamii au tofauti nje ya kuhubiri neno na kucheza gospel music? Mimi nawashangaa TU wameshindwa kurusha matangazo yao Startimes!?
Kwa content za kiafya, mtindo wa maisha na kijamii...kama familia , malezi ya watoto! Fuatilia Hope channel TZ au morning star radio ya waadventista wasabato.
 
Jambo kubwa kwa sasa huko ni mambo ya kutoa baraka kwa upinde.
Mambo ya kuinjilisha wamewaacha walokole.
 
Quest ya muulizaji ni kuhusu aagizo la Yesu mwenyewe hapa chini.
👇
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; ”
— Mathayo 28:19 (Biblia Takatifu)
Hilo andiko umelielewaje?
 
Kwa sasa neno la Mungu limetafsiriwa kwa karibu lugha zote kubwa, kwa hiyo yeyote anayehitaji kulisikiliza hana kikwazo cha lugha. Mitume walinena kwa lugha ili kuwawezesha Waparthi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, Frigia, Pomfilia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi wapate kusikia na kufuata neno hilo. Inawezekana hauelewi lengo la kunena kwa lugha walikofanya Mitume, ndio maana kwa sasa unanena lugha ambayo wewe mnenaji na anayesikiliza wote hamuielewi na hamuelewi maudhui yake
sasa sikia, kwa kukusaidia, wala haipo kama unavyoamini. Roho Mtakatifu ni muhimu hata leo hii kwako kwa ajili ya Maombi, unahitaji unene kwa lugha katika maombi yako. siku ya pentecost ni kweli watu walisema kwa lugha mbalimbali kadiri Roho alivyowajalia, ila haimaanishi kama lengo lilikuwa ni kuwafanya watu wote wa pale Yerusalemu (siku ile ya pentecost) waelewe, Noo, kwasababu wote waliokuwepo pale walikuwa wanaelewana lugha. wawe wayahudi wa libya, ponto, arabuni au wowote wakiwa pale Yerusalem walikuwa wanaongea lugha ya pale, na walienda pale kuabudu, wakitumia lugha ya pale.

lakini hata tuseme pengine lugha zilitafsiriwa ili watu waelewe, kwanini sasa Matendo 19:1 na kuendelea niliyosema uisome ukakimbia, inaonyesha kwamba wale wote waliokuwa wamebatizwa na Apolo walikuwa watu wa lugha moja, na Pauli still aliwawekea mikono na Roho Mtakatifu akashuka wakaanza kunena? walikuwa wanamwambia nani sasa wakati wote walikuwa wa lugha moja?

Yesu alisema ishara hizi zitaambatana na wote waaminio, moja wapo ya ishara ni kusema kwa lugha mpya, sio kwa ajili ya kutafsiria mtu bali hiyo ni ishara kwamba umejazwa Roho. Ninyi wakatoliki hilo mmelitupa.

Mnachanganya Paulo alipoenda kwa waumini kuwatuliza baada ya kuona badala ya kuhutubu sasa wao wakifika kanisani wananena kwa lugha tuuu hakuna kuhubiri, akawa anawatuliza kwamba wanene ila na kuhutubu wahutubu ili wageni wakija waelewe kinachoendelea. pamoja na yote hakumaanisha kwamba wasinene kwa lugha manake aliwaambia kabisa kwamba "mimi nanena kwa lugha kuliko ninyi nyote". hilo nalo unasemaje?

1Korintho 14: 12 - 19, Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, jitahidini kusudi mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa. 13 Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri. 14 Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda. 15 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia. 16 Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika mahali pa mjinga ataitikaje, Amina, baada ya kushukuru kwako, akiwa hayajui usemayo? 17 Maana ni kweli, wewe washukuru vema, bali yule mwingine hajengwi. 18 Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote; 19 lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, kuliko kunena maneno elfu kumi kwa lugha.

NB: nimekuwekea mstari ambao utaupenda, hasa hapo anaposema awepo mtafsiri, usije kufikiri alisema basi usinene hadi awepo, kama hayupo usinene, ni kwamba kanisa lilikuwa linanena tu hawatafsiri wala kuhutubu akawa anawaambia kuwa kunena ni muhimu lakini na kuhutubu na kutafsiri ni muhimu pia. hapo amesisitiza kwamba nitaomba kwa akili na nitaomba kwa roho pia. sasa ninyi kwa roho huwa hamuombi? wakati ukiomba kwa roho ndio roho yako inaomba. jibu hili swali.

Warumi 8:26 - 28, Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. (swali, ninyi msionena kwa lugha, Roho huwa anawaombeaje?).

Wagalatia 4:6 - 7, Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu aliaye Aba, yaani BAba. kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena, bali u mwana, na kama u mwana basi u mrithi kwa Mungu. (swali, ninyi huwa hamneni, mna Roho? mu warithi sambamba na mstari huu?).

Warumi 8:9-17, Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili bali mwaifuata roho. lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo si wake. Na Kristo akiwa ndani yenu mwili wenu umekufa kwasababu ya dhambi bali roho yenu i hai, kwasababu ya haki. lakini ikiwa Roho yake yey ealiyemfufua Yesu katika watu anakaa ndani yenu yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. basi kama ni hivyo ndugu tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia Aba, yaani Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu, na kama tu watoto basi tu warithi warithi wa Mungu warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

SWALI: ninyi msiojazwa Roho, msionena, Roho wenu huwa anajidhihirishaje kwenu? kama hajawaku jidhihirisha manake ninyi hamuongozwi na Roho, hamsali kwa Roho, na sio watoto wa Mungu kwasababu wote wasio na Roho hao sio wake kama ilivyo kwenye mstari hapo juu. justifiation yenu ya kutoomba kwa Roho Mtakatifu ni nini?
 
Mimi ninanukuu vifungu na kuviweka hapa ili wote waone hoja. Wewe unasema niende nikasome kifungu; kwani ukikiweka hapa ukajenga hoja kuna ubaya gani? 😁😁😁
Matendo 19: 1 - 9, Wakati Apolo alikuwa Korintho, Paulo alipitia sehemu za kaskazini akafika Efeso. Huko aliwakuta wanafunzi kadhaa, 2 aka wauliza, “Mlipoamini mlipokea Roho Mtakatifu?” Wakajibu, “Hapana. Hatujawahi hata kusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.” 3 Ndipo Paulo akawauliza, “Mlibatizwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Ubatizo wa Yohana.” 4 Paulo akasema, “Yohana alipobatiza, aliwaambia watu watubu dhambi na kumwamini atakayekuja baada yake, yaani, Yesu.” 5 Waliposikia haya, wakabatizwa katika jina la Yesu. 6 Na Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia , wakasema kwa lugha mpya na kutabiri.

sasa soma hapo juu, halafu niambie baada ya Paulo kuwawekea mikono hawa watu, walifanya nini? walisema kwa lugha mpya na kutabiri. manake walinena kwa lugha. sasa niambie, lini ulishawahi kuona hata padre au hata papa amenena kwa lugha? tuseme ninyi mna Roho? kwa ishara gani mlizo nazo, wakati Yesu alisema na ishara hizi zitaambatana na wale watakaoamini, mojawapo ni kusema kwa lugha mpya...ninyi Roho Mtakatifu aliwakosea nini hadi msipende kunena kwa lugha yake?
 
Kwa sasa neno la Mungu limetafsiriwa kwa karibu lugha zote kubwa, kwa hiyo yeyote anayehitaji kulisikiliza hana kikwazo cha lugha. Mitume walinena kwa lugha ili kuwawezesha Waparthi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, Frigia, Pomfilia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi wapate kusikia na kufuata neno hilo. Inawezekana hauelewi lengo la kunena kwa lugha walikofanya Mitume, ndio maana kwa sasa unanena lugha ambayo wewe mnenaji na anayesikiliza wote hamuielewi na hamuelewi maudhui yake
JE? KUNENA KWA LUGHA NI LAZIMA KAMA ISHARA YA KUJAZWA NA ROHO?

Marko 1:8
, Yohana Mbatizaji alihubiri akiwaambia watu kwamba, “mimi nawabatiza kwa maji, bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.

Matendo 11:16, Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu. (hapa, Petro alikuwa anawaeleza wenzake yale maono ya kuchinja wanyama hata ambao kwa kiyahudi ni wachafu ale, story ya Kornelio, alipoondoka na wale waliotumwa na Kornelio kwenda kumchukua kule Yafa, akafika akaanza kuwafundisha, Roho Mtakatifu akashuka kwa wale watu wakaanza kunena, ndio anasema akalikumbuka lile neno alilosema Yesu, hapa kushuka na kunena kwa Roho manake walikuwa wanabatizwa kwa Roho. Swali, ninyi wakatoliki huwa mnabatizwa kweli kwa Roho? Padre yeyote alishawahi kubatizwa kwa Roho?

Matendo 1:4-5, Hata alipokuwa amekutana nao, aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. (SWALI: ninyi huwa mnabatizwa kwa Roho au la?, ishara yake ni ipi kama hamtaki kunena kwa lugha?).
 
... haimaanishi kama lengo lilikuwa ni kuwafanya watu wote wa pale Yerusalemu (siku ile ya pentecost) waelewe, Noo, kwasababu wote waliokuwepo pale walikuwa wanaelewana lugha. wawe wayahudi wa libya, ponto, arabuni au wowote wakiwa pale Yerusalem walikuwa wanaongea lugha ya pale, na walienda pale kuabudu, wakitumia lugha ya pale.
Kwa hiyo walinena kwa lugha ili kujifurahisha?
 
Papa yuko bize kujaribu kuhalalisha yale mambo ya kishetani. Kanisa kongwe la mitume!
Papa huwezi kumwelewa. Kama maaskofu wameshindwa kumwelewa ndio wewe? Kwa mtu wa upeo mdogo, kutafsiri na kuuishi upendo ni ndoto
 
Ni mpaka watapotokea walei wa invest kuweka maudhui ya Kikatoliki. Tuko slow mno na kutumia media kuinjilisha.

Hata TV maarufu duniani EWTN founder ni mother Angelica na inaendeshwa kupitia bodi maalum.
 
1. Maji
2. Mshumaa (Mwanga wa Roho Mtakatifu)
3. Kitambaa cheupe
hHAHAAAAAAA, Yesu alisema, Yohana mbatizaji alibatiza kwa maji, ila ubatizo wake yeye ni wa Roho Mtakatifu. lakini ninyi mnabatiza kwa mshumaa na kitambaa cheupe (ukiachilia pembeni hiyo ya maji ambayo ni desturi inayofuatwa na wengi), hauoni kama mmepotea? NIkuwekee tena mistari hii hapa chini halafu kuanzia leo muache kupotosha watu kufuata mapokeo ya wanadamu huku mkiacha Neno la Mungu, nawakemea kwa Jina la Yesu, hukumu hii mtainywa wakati ukifika kuanzia papa hadi mtu wa mwisho kabisa.

Marko 1:8, Yohana Mbatizaji alihubiri akiwaambia watu kwamba, “mimi nawabatiza kwa maji, bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu. (huu mstari huwa hamuuoni hadi mbatize watu kwa mshumaa?) Roho Mtakatifu sio mshumaa, ni nafsi halisi ya Mungu, inaongea, inaongoza, inafundisha, mshumaa wenu si ndio ibada ya sanamu hiyo? wakatoliki shtukeni, changamkeni, kimbieni mpo kwenye dini inayowapeleka motoni na katu hamtakuja kumwona Mungu, ndio maana kila sisi wenzenu tukishuhudia kuwa tumemwona Mungu, ninyi huwa hamuelewi, kwasababu mlivyojiposition sio rahisi Mungu kuonekana, mnamtafuta kwa njia potofu, na hataonekana kwenu. kwahiyo ukimbatiza mtu kwa mshumaa huwa ananena kama Yesu alivyosema au?

Matendo 11:16, Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu. (hapa, Petro alikuwa anawaeleza wenzake yale maono ya kuchinja wanyama hata ambao kwa kiyahudi ni wachafu ale, story ya Kornelio, alipoondoka na wale waliotumwa na Kornelio kwenda kumchukua kule Yafa, akafika akaanza kuwafundisha, Roho Mtakatifu akashuka kwa wale watu wakaanza kunena, ndio anasema akalikumbuka lile neno alilosema Yesu, hapa kushuka na kunena kwa Roho manake walikuwa wanabatizwa kwa Roho. Swali, ninyi wakatoliki huwa mnabatizwa kweli kwa Roho? Padre yeyote alishawahi kubatizwa kwa Roho?

Matendo 1:4-5, Hata alipokuwa amekutana nao, aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. (SWALI: ninyi huwa mnabatizwa kwa Roho au la?, ishara yake ni ipi kama hamtaki kunena kwa lugha?). tuambie, ndimi za moto zilizowakalia wale 120 pale upper room, na walivyonena kwa lugha, walibatiza kwa mshumaa na kitambaa?

siwahukumu, nawafafanulia halafu nawaombea kwa Mungu macho yenu yafumbuke, yatiwe nuru, kama Waefeso 1:18 inavyosema, Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo. dini imewafanya kuwa vipofi, jeuri na kiburi ya kutosikia ushauri wala Neno la Mungu vitawaangamiza.

Marko 7:8 Yesu aliwakemea washika dini kama wewe kwamba, Ninyi mwaiacha amri ya Mungu na kushika mapokeo ya wanadamu. (mmeacha Neno halisi la Mungu kama nilivyoliweka hapo Yesu alivyosisitiza, na mnashika mapokeo ya dini yenu).
 
Kwa hiyo walinena kwa lugha ili kujifurahisha?
Tatizo kubwa ni kwamba, huwezi fahamu experience ya Roho Mtakatifu kama haujawahi kujazwa, ndio maana tunapata shida kueleza, ni kitu ambacho huwezi kukijua hadi ujazwe. Ni Nguvu ya Mungu inayokaa ndani yako ambayo hakuna wa kuishinda, na akiongea kwa kutumia kinywa chako maneno yake yote yana impact. Ndio maana Petro aliyekuwa mvuvi tu hata kama alitembea na Yesu siku alipojazwa Roho Mtakatifu siku ya Pentecost, alipata Nguvu ya ujasiri akahubiri wayahudi wakachomwa mioyo wakaokoka siku moja watu 3,000.

unaponena kwa lugha, roho yako inakuwa inaomba: 1Korintho 14:14 - 15 "Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda" Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho, na pia nitaomba kwa akili yangu. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia " Roho Mtakatifu anaponena ndani yako, Roho yako inakuwa inaomba, kwa faida yako binafsi, anakusaidia kuomba, kwasababu ukiomba kwa akili pekee mwanadamu ni mdhaifu lazima tu hataomba sawasawa na mapenzi ya Mungu, cha kwanza ataanza kuomba mahitaji na tamaa za mwili badala ya kutaka karama za rohoni au hata kama ni za mwilini basi ziwe kwa mapenzi ya Mungu.

Pia, Unapoomba kwa Roho, kuna raha moyoni, raha ya utakatifu na amani ya Kristo ipitayo akili zote ambayo hata nikikueleza hapa hauwezi kuelewa kwasababu anayeijua hiyo amani ni yule tu ambaye alishawahi kuexperience.

sisi ni wadhaifu, hatuwezi kuomba ipasavyo: Rumi: 8:26 - 27, Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
 
Tatizo kubwa ni kwamba, huwezi fahamu experience ya Roho Mtakatifu kama haujawahi kujazwa, ndio maana tunapata shida kueleza, ni kitu ambacho huwezi kukijua hadi ujazwe.
Bado hujajibu swali kwamba kwa nini uongee lugha ambayo wewe huielewi na wala anayekusikia haielewi, wakati imeandikwa mitume walinena lugha ambayo watu wengine wa kutoka nchi mbalimbali waliielewa kila mtu kwa lugha yake. Sasa unasema unashindwa kuielezea hali inavyokuwa, tukisema ni illusion tutakosea?
Wakatoliki tunafuata maandiko matakatifu kwamba Roho Mtakatifu yupo popote na kwa yeyote, hahitaji kumjaza mtu. Ni kwa wato wote.
Yoeli 2:28
28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
 
Back
Top Bottom