Kwa sasa neno la Mungu limetafsiriwa kwa karibu lugha zote kubwa, kwa hiyo yeyote anayehitaji kulisikiliza hana kikwazo cha lugha. Mitume walinena kwa lugha ili kuwawezesha Waparthi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, Frigia, Pomfilia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi wapate kusikia na kufuata neno hilo. Inawezekana hauelewi lengo la kunena kwa lugha walikofanya Mitume, ndio maana kwa sasa unanena lugha ambayo wewe mnenaji na anayesikiliza wote hamuielewi na hamuelewi maudhui yake
sasa sikia, kwa kukusaidia, wala haipo kama unavyoamini. Roho Mtakatifu ni muhimu hata leo hii kwako kwa ajili ya Maombi, unahitaji unene kwa lugha katika maombi yako. siku ya pentecost ni kweli watu walisema kwa lugha mbalimbali kadiri Roho alivyowajalia, ila haimaanishi kama lengo lilikuwa ni kuwafanya watu wote wa pale Yerusalemu (siku ile ya pentecost) waelewe, Noo, kwasababu wote waliokuwepo pale walikuwa wanaelewana lugha. wawe wayahudi wa libya, ponto, arabuni au wowote wakiwa pale Yerusalem walikuwa wanaongea lugha ya pale, na walienda pale kuabudu, wakitumia lugha ya pale.
lakini hata tuseme pengine lugha zilitafsiriwa ili watu waelewe, kwanini sasa Matendo 19:1 na kuendelea niliyosema uisome ukakimbia, inaonyesha kwamba wale wote waliokuwa wamebatizwa na Apolo walikuwa watu wa lugha moja, na Pauli still aliwawekea mikono na Roho Mtakatifu akashuka wakaanza kunena? walikuwa wanamwambia nani sasa wakati wote walikuwa wa lugha moja?
Yesu alisema ishara hizi zitaambatana na wote waaminio, moja wapo ya ishara ni kusema kwa lugha mpya, sio kwa ajili ya kutafsiria mtu bali hiyo ni ishara kwamba umejazwa Roho. Ninyi wakatoliki hilo mmelitupa.
Mnachanganya Paulo alipoenda kwa waumini kuwatuliza baada ya kuona badala ya kuhutubu sasa wao wakifika kanisani wananena kwa lugha tuuu hakuna kuhubiri, akawa anawatuliza kwamba wanene ila na kuhutubu wahutubu ili wageni wakija waelewe kinachoendelea. pamoja na yote hakumaanisha kwamba wasinene kwa lugha manake aliwaambia kabisa kwamba "mimi nanena kwa lugha kuliko ninyi nyote". hilo nalo unasemaje?
1Korintho 14: 12 - 19, Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, jitahidini kusudi mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa. 13 Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri. 14
Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda. 15 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia. 16 Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika mahali pa mjinga ataitikaje, Amina, baada ya kushukuru kwako, akiwa hayajui usemayo? 17 Maana ni kweli, wewe washukuru vema, bali yule mwingine hajengwi. 18
Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote; 19 lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, kuliko kunena maneno elfu kumi kwa lugha.
NB: nimekuwekea mstari ambao utaupenda, hasa hapo anaposema awepo mtafsiri, usije kufikiri alisema basi usinene hadi awepo, kama hayupo usinene, ni kwamba kanisa lilikuwa linanena tu hawatafsiri wala kuhutubu akawa anawaambia kuwa kunena ni muhimu lakini na kuhutubu na kutafsiri ni muhimu pia. hapo amesisitiza kwamba nitaomba kwa akili na nitaomba kwa roho pia. sasa ninyi kwa roho huwa hamuombi? wakati ukiomba kwa roho ndio roho yako inaomba. jibu hili swali.
Warumi 8:26 - 28, Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. (swali, ninyi msionena kwa lugha, Roho huwa anawaombeaje?).
Wagalatia 4:6 - 7, Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu aliaye Aba, yaani BAba. kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena, bali u mwana, na kama u mwana basi u mrithi kwa Mungu. (swali, ninyi huwa hamneni, mna Roho? mu warithi sambamba na mstari huu?).
Warumi 8:9-17, Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili bali mwaifuata roho.
lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo si wake. Na Kristo akiwa ndani yenu mwili wenu umekufa kwasababu ya dhambi bali roho yenu i hai, kwasababu ya haki. lakini ikiwa Roho yake yey ealiyemfufua Yesu katika watu anakaa ndani yenu yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. basi kama ni hivyo ndugu tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho mtaishi.
Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo
twalia Aba, yaani Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu, na kama tu watoto basi tu warithi warithi wa Mungu warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
SWALI: ninyi msiojazwa Roho, msionena, Roho wenu huwa anajidhihirishaje kwenu? kama hajawaku jidhihirisha manake ninyi hamuongozwi na Roho, hamsali kwa Roho, na sio watoto wa Mungu kwasababu wote wasio na Roho hao sio wake kama ilivyo kwenye mstari hapo juu. justifiation yenu ya kutoomba kwa Roho Mtakatifu ni nini?