Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawatafanikiwa kwenye hili la kulazimisha mambo yawe wanavyotaka wao, tunaojitambua siku zote tutasimama na kulipigania Kanisa Katoliki bila hofu, aibu, wala uoga wowote, potelea mbali wajinga waendelee kutuona wafia dini ambao kwao kukaa kimya na kuficha ukweli ndio ujanja, kumbe ni unafiki.Chuki zenu dhidi ya Ukatoliki haziwezi kumtikisa Papa wala Kanisa. Vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vinavyounga mkono ushoga, wahafidhina wa Kiislamu na madhehebu ya kikiristo yenye upinzani na katoliki ndiyo yaliyoko busy kugeuza maana na msimamo wa Vatican kuhusu ushoga.
Kuna propaganda za wazi kabisa kwenye hili, kwa mfano kugeuzwa na kupotoshwa kwa makusudi kauli ya Papa alipokuwa akitoa majibu baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari kuhusu watu wanaojihusisha na ndoa za jinsia moja kwa maana ya ushoga na usagaji.
Aliulizwa yapo Mataifa yamepitisha sheria ya kuwauwa watu wanaojihusisha na ushoga na usagaji na pia yapo makanisa na jamii zimewatenga na hawaruhusiwi hata kusogelea Kanisa.
Papa akajibu,Hatutakiwi kuwauwa wala kuwatenga na akasema,inapotokea watu wanaojihusisha na usagaji,ushoga na usenge wameenda Kanisani wasifukuzwe wala kuadhibiwa kwa kuuliwa bali ni kazi ya Kanisa kuwapokea na kuwaombea ili wabadilike na kumrejea mwenyezi Mungu.
Papa alisema hayo kutokana na baadhi ya mataifa kuchukua uamuzi wa kuwauwa na kuwatenga.
Akasema kazi ya Kanisa siyo kuwauwa na Kuwatenga bali kuwapokea na kuwaombea.
Sijuhi chuki zenu dhidi ya Kanisa katoliki zina faida gani kwenu.
Na uzuri sisi Wakatoliki huwa tunamind our own business hatunaga muda wa kupigizana kelele na mamikutano ya hadhara.Mambo yetu ni kwenye Jumuiya ndogo ndogo na Kanisani tumemaliza.Hamna kuyumba, makelele yao yakizidi ni kuwapuuza tu na akili ndogo zao.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
- Hakuna popote nilipoandika mapadri au Papa sio binadamu, kufanya kosa sikatai wanaweza kukosea, lakini lazima kosa hilo liwe la ukweli, sio huu uongo unaoletwa na wenye nia ovu.Mkuu kuna jambo halipo sawa kwa viongozi wa katoliki huko juu hata kama hutaki. Ukumbuke wale ni binadamu.
Hapa unachosema ni mashoga wakubalike kama wanavyokubalika wezi na wenye dhambi wengine. Unasahau historia ya imani ya kikristo linapokuja suala la ushoga. Nakwambia kuna kitu hakipo sawa na ikiendelea hivi bila kupingwa watetezi watajikuta wameingia kwenye mfumo.
PAPA IS WRONG LINAPOKUJA SUALA LA KUBARIKI MASHOGA. HATA HIVYO MIBARAKA INAPASWA KUTOLEWA BAADA YA KUTUBU DHAMBI.
Kama suala ni kubariki mali bila kujali aina ya dhambi kwanini ushoga uwekewe upekee wa kutolewa waraka? Huoni kuna attention inayotafutwa kuhusu ushoga?
Kama wasiojulikana tabia na matendo yao na mashoga wapo ndani upekee ni wa nini wa kuutambua ushoga? Si haijulikani? Kwani kabla mashoga, wezi, hawakuwa wakibarikiwa? Special attention ya nini kwa mashoga? Kuna kitu hakipo sawa.
Hili ni suala simple sana, kuhubiria mashoga waache ushoga au jambazi aache ujambazi si hichi kinachofanyika. Hichi kinachofanyika ni kuuandaa ubongo kuukubali ushoga. Ni suala la muda huyu papa asipodhibitiwa basi ushoga utakuwa jambo la wazi na la kawaida.
Biblia yenyewe ni ya kijima, misingi yake ni ya kijima tangu uumbaji. Watu waachane na hayo mawazo watoke waende wapi? Mambo ya upo nyuma ya muda, acha ushamba, una mawazo ya kijima ni misemo ya mashoga wakitaka kuhalalisha hiyo tabia. Kuna jambo halipo sawa, Isipobadilika muda utasema.
Kwanini hatujawahi kuona waraka wa kuwabariki wazinzi? What is so special kwa hawa watenda dhambi wengine kwa jina la mashoga?Wazinzi mbna wanabarikiwa kila siku? Tena wengine wanabarikiwa na mimba iko tumboni, wee hujui au??
Yesu mwenyewe aliambiwa na viongozi wa kidini wa Kiyahudi kuwa ni rafiki wa makahaba na walevi, kisa tu alikuwa kuwatafuta wadhambi. Yesu aliwaambia, mzima hahitaji daktari Ila mgonjwa. Hawa wanaomlaumu Papa Paulo ni sawa na wale viongozi wa Kiyahudi waliokuwa hawataki wadhambi wawakaribie. Shoga ahubiriwe abadilike, ukimtenga ni sawa na kupelekwa dawa kwa mzima ukaacha kupelekwa kwa mgonjwa (shoga).Umepotosha kwa kiasi kikubwa, unaonekana hujasoma hata ule waraka wa Vatican, ulichofanya ni kuokoteza maneno kwa wengine na kuja kuanzisha huu uzi wako hapa, hujafanya uchunguzi wowote, sasa hiyo aibu aione nani?
- Kama hutaki mashoga wavumiliwe na kutambuliwa ndani ya Kanisa Katoliki, unataka wezi, waongo kama wewe, na wazinzi, wao pekee ndio waendelee kuvumiliwa? Kanisa Katoliki haliishi kwenye misingi ya kinafiki.
- Kwanini hutaki mashoga wapewe sakramenti kama waumini wengine? au wale wanaopewa ni watakatifu? hayupo yeyote miongoni mwao mwenye dhambi? Hapa unaonesha ulivyojaa ubinafsi, Papa yuko above your thinking capacity.
- Wapi umeona kwenye ule waraka wa Vatican pameandikwa Kanisa Katoliki litabariki mashoga? tuwekee hapa tupaone, kisha nami nitakuwekea pale palipoandikwa Kanisa Katoliki litabariki mali za mashoga, sio mashoga kama ulivyopotosha hapa.
Hii ni sawa na kubariki mali za wengine wasiojulikana tabia na matendo yao, hakuna yeyote anayejulikana kama ni mzinzi sababu hufanyia sirini, mwizi hufanyia sirini, kujaribu kuwatenga mashoga kama vile wao pekee ndio wenye dhambi ni unafiki na ubinafsi, Papa hataki huu unafiki.
Papa anajua miongoni mwetu hayupo aliyekamilika, Kanisa Katoliki pia linajua hivyo, tukianza kutazamana usoni na kutengana mwisho wa siku huko kanisani atabaki nani? injili atahubiriwa nani? hujui hata Yesu Kristu alikuja duniani ili kuwahubiria wenye dhambi wapate kuokoka?
Mna upeo mdogo sana kifikra, na thinking yenu ni ya kijima sana wakati Kanisa Katoliki lilishatoka huko.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ushoga na ulawiti umo ndani ya Quran 2:223 kwamba wanawake ni konde zenu zieendeeni konde zenu kama mpendavyo, tafsiri ya Kitabu Sabulus-Salam juzuu 3 ambapo Mtume alisema Aya hii imeteremshwa kwa ajili ya wanaume kuwaingilia wake zao tupu zao za nyuma.Wacha ushoga
Kama wanaweza kukosea basi wakikosea ni sawa kusimama na kupinga. Watu walipigana hadi na malaika mieleka sembuse papa. Mnafiki ni yule asiyehoji na kutetea kila kitu kutoka kwa viongozi. Shetani lipo na linaweza ingia hadi kanisani. Kama linaweza kwenda hadi mbinguni na kuzungumza na MUNGU mwenyewe namna ya kumtesa Ayubu hapo vatican inashindikana vipi?- Hakuna popote nilipoandika mapadri au Papa sio binadamu, kufanya kosa sikatai wanaweza kukosea, lakini lazima kosa hilo liwe la ukweli, sio huu uongo unaoletwa na wenye nia ovu.
Usasa miongozo yake ni ipi? Kuna miongozo ya kisasa zaidi ya biblia inachoagiza?- Kanisa Katoliki haliendeshwi kwa historia, linaendeshwa kwa usasa kulingana na mabadiliko yanayoendelea kutokea kwenye jamii ya waumini inalowaongoza, mambo ya historia yaache vitabuni huko.
Kama hakuna kwanini tupo hapa tukizungumza kuhusu waraka? Hili swali ni la kupuuza ila kwa heshima yako hapa JF nimelijibu kwa kukuuliza swali.- Wapi kwenye ule waraka Papa amesema anabariki mashoga? hebu tuoneshe hapa tupaone.
Hawa wajinga ni kuendelea kuwaamsha tu, hawayajui maandiko, wana upeo mdogo kifikra, wanaongozwa na chuki dhidi ya Kanisa Katoliki ikiambatana na ushabiki na mihemko ya kipuuzi.Yesu mwenyewe aliambiwa na viongozi wa kidini wa Kiyahudi kuwa ni rafiki wa makahaba na walevi, kisa tu alikuwa kuwatafuta wadhambi. Yesu aliwaambia, mzima hahitaji daktari Ila mgonjwa. Hawa wanaomlaumu Papa Paulo ni sawa na wale viongozi wa Kiyahudi waliokuwa hawataki wadhambi wawakaribie. Shoga ahubiriwe abadilike, ukimtenga ni sawa na kupelekwa dawa kwa mzima ukaacha kupelekwa kwa mgonjwa (shoga).
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Usitumie nguvu nyingi boss. Call a spade a spade. Papa amekosea. Shida uko wapi yeye ni mtu anayefanya excretion kama wewe kukosea na kutenda dhambi ni kawaidaupotoshaji wa mwendokasi.
Acha uongo,
mkatoliki hana muda wa kubishana wala kupambana na yeyote kuhusu hilo linalopotoshwa...
Mafundisho yao ni ya kiroho na kisaikolijia zaidi...
Wapi pametajwa uislam?MUNGU hayupo kwenye ukristo wala uislam, MUNGU yupo ndani yetu na wala si kwa papa wala shekhe kipozeo.
- Hilo kosa la Papa liko wapi? usilazimishe tu kila kitu kiwe kosa, haya ni mawazo ya kijinga, nimekwambia nipe ushahidi wapi kwenye ule waraka panasema Papa atabariki mashoga, umeshindwa kunionesha nakuona unaandika ngonjera zako tu hapa.Kama wanaweza kukosea basi wakikosea ni sawa kusimama na kupinga. Watu walipigana hadi na malaika mieleka sembuse papa. Mnafiki ni yule asiyehoji na kutetea kila kitu kutoka kwa viongozi. Shetani lipo na linaweza ingia hadi kanisani. Kama linaweza kwenda hadi mbinguni na kuzungumza na MUNGU mwenyewe namna ya kumtesa Ayubu hapo vatican inashindikana vipi?
Usasa miongozo yake ni ipi? Kuna miongozo ya kisasa zaidi ya biblia inachoagiza?
Kama hakuna kwanini tupo hapa tukizungumza kuhusu waraka? Hili swali ni la kupuuza ila kwa heshima yako hapa JF nimelijibu kwa kukuuliza swali.
Mkuu kitu usichokijua kuhusu Wakatoliki ni kuwa hawana muda kubishana na watu wenye uwezo mdogo wa kupambanua mambo,wanaitwa waabudu sanamu na sasa mnawaita mashoga lkn wao hawana haja ya kubishana na watu wasioijua imani yao.Siku hizi wale wanaoitwa wavaa Kobazi wamejihakikishia kuwaita Wakatoliki mashoga. Na hakuna wakupinga
Kanisa limekuwa likibariki mali za wenye dhambi, huu upekee wa kubariki mali za mashoga umetokana na nini?Miongozo ya usasa ndio kama hii Papa anabariki mali za mashoga mnaishia kumkasirikia, mnataka tuendelee kuishi kijima kama mlivyozoea.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Nimeshajibu hili swali lako kule juu karibia mara tatu, kama huna jibu sorry.Kanisa limekuwa likibariki mali za wenye dhambi, huu upekee wa kubariki mali za mashoga umetokana na nini?
mnavojua kuupamba uovu, hv ushoga umeanza leo? mpaka utolewa waraka wa kuukubali?Hawatafanikiwa kwenye hili la kulazimisha mambo yawe wanavyotaka wao, tunaojitambua siku zote tutasimama na kulipigania Kanisa Katoliki bila hofu, aibu, wala uoga wowote, potelea mbali wajinga waendelee kutuona wafia dini ambao kwao kukaa kimya na kuficha ukweli ndio ujanja, kumbe ni unafiki.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Wewe hujibu unahaha kuingia kwenye mfumo wa kubariki hizo unazoziita mali za mashoga. Na unateseka kweli maana ni kinyume na maadili yako ila akili yako inakataa kumpinga papa.Nimeshajibu hili swali lako kule juu karibia mara tatu, kama huna jibu sorry.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Jamaa anajikaza kanakwamba yeye ni mkatoliki kuliko wanaopinga hili suala. Kuna wakatoliki wanaomuelewa Papa zaidi yake na wamesimama against hilimnavojua kuupamba uovu, hv ushoga umeanza leo? mpaka utolewa waraka wa kuukubali?
Niwekee ushahidi wako hapa, nani amekwambia natania?Mkuu kuwa serious