Wakazi: Diamond Platnumz ni maarufu ila hajui kuimba, "ukweli unauma mpaka mnanipigia simu za vitisho"

Wakazi: Diamond Platnumz ni maarufu ila hajui kuimba, "ukweli unauma mpaka mnanipigia simu za vitisho"

Ukiwa critical thinker kwenye jamii ya watu wenye upeo mdogo kama kitenes unakua unaonekana wewe ndio mwehu
Wakaz yuko sahihi kabisa ila watu wamepofushwa na mahaba
Huwa nakuonea huruma sana kizazi Cha Tz kuanzia 2030+ ,kutakuwa ni ujinga mtupu maana umeanza kukua kila siku.........
 
Kuwa na mawazo hayo ni dhana mbaya sana ya kimasikini na yenye utabaka, kufikiria mwenye haki ya kukosolewa ni yule ambaye hana kitu, kuwa hata ukimkosea watu watasema ni sawa as long as hana kitu cha thamani cha kukufanya uonekane mkosoaji una wivu nacho

Kwamba mkosoaji amemuona Diamond kuwa ni tajiri sana kiasi cha kumonea wivu kuliko MO na Bakhresa ambao wako kwenye rank za matajiri Africa?
MO na Bakhresa siyo masuperstar Bali ni famous

Diamond ni superstar
 
Nafikiri wanamjibu maana naye aliwapa makavu sana
 
Wakazi yuko sahihi Diamond hata atoe ngoma ya dakika mbili halafu humo ndani awe anacheka mwanzo mwisho utaona ngoma hiyo itavyokuwa trend na usikute ikapewa na tuzo

Hayo yote yamerahisishwa kutokana na jina (umaarufu) na ndio maana hata hawa ma underground wana amini wakipata nafasi ya kufanya kazi kwenye lebel yao watatoka tu, kwasababu kitachowafanya wajulikane sio ubora wa kile wanachokiimba

Means hata kwa level zao za huku chini wanaamini hata wakaze msuli namna gani bado ubora wa nyimbo hautakuwa kigezo wao kutoka

Nakubaliana na Wakazi
Kuna moja inaitwa abeykhe sijui kama nimepatia jina, ameimbana mastercraft na mr flavor. Sijui waliwaza nn
 
True, Diamond hajuwi kuimba ila yuko famous. Diamond anaimba tune moja ile ile, wale wanaojuwa muziki watakubaliana nami.
 
Wakazi huwezi kumfananisha na nikki wa pili

Niki wapili alikiwa ni chawa, mlamba miguu, asskisser aliyepitiliza mpaka akapewa huo u DC

Tena umenikumbusha kati ya wasanii ambao nimekuwa nawaongelea negative basi hapa mtaiona nafuu ya diamond katika kuwakosoa wasanii

Kipindi cha magufuli ambapo tweeter ilipigwa ban, na kufanya access iwezekane kwa vpn tu, huyu jamaa alijitokeza na ku tweet kuwa watu wanaizushia serikali uwongo kwani yeye ameweza kuingia tweeter bila vpn na kwenda mbali kuwa watu wanafanya hivyo kumchafua magufuli tu

Baada ya hapo zikaja gharama kubwa za mabando, jamaa akasimamia ukucha kuwa wananchi wasilie lie kuhusu bando kwanj sio kitu necessary kama kula, ni jambo linaweza kuepukika tu kuliko kuisumbua serikali kuhusu kupunguziwa gharama za bando

Haya akaja tena kwenye tozo akaongea ujinga kibao just kuwa upande wa serikali

Sio huyo tu, hadi masanja naye ni wa type hiyo hiyo na anasemwa sana.

Lakini utofauti unavyokuja tukiwasema hawa hatutajwi kama watu wenye wivu wa mafanikio ya hao watu au haters kwasababu nikki wapili hajaweza kuwa na mashabiki wengi wakumtetea kama ilivyo kwa diamond na alikiba kila platfom kuna utimu

Kwa hiyo nasisitiza kuwa diamond kwenye ywezo wa kuimba bado sana, labda kama utanifananishia yule diamond wa "utanipenda" lakini huku kwa nyegezi ni ujinga na aibu kukubaliana na hoja hiyo kuwa mwana anaimba vizuri
Bro wewe mdau wa rap,nikikwambia unitajie rappers wako kumi Bora list yako itakua tofauti na Jay z, Mimi,Fid Q,ubishi wa kitoto kama huu ndio unakupunguzia points,Kusema fulani ni mwanamuziki mzuri kuliko fulani ni kitu "subjective"kila mtu ana maoni yake,na mkali wake ,usifanye mtazamo wako binafsi ndio FACT...

I respect your opinions tho,hata Mimi sijawahi kuona kama diamond muimbaji mzuri but sio suala la kushindana coz mziki ni suala la hisia na Mapenzi hiyo kujua au hajui kila mtu na maoni yake...mimi nampenda saaaaana Belle 9,sijui I'm lil biased coz natokea Moro,I don't know....mkali Nani??tutakesha Hakuna jibu
 
Back
Top Bottom