Wakazi wa Dar, ulishawahi kuitwa na kuingia kwenye mfumo wa huyu muuza juice pale Karume?

Wakazi wa Dar, ulishawahi kuitwa na kuingia kwenye mfumo wa huyu muuza juice pale Karume?

Hawa waizi,sijui matapeli huwa wanaangalia na watu wa kuwafanyia huo ujinga
 
View attachment 3063170

unatembea zako ghafla unaitwa,

zinaanza stori "vipi, bwana habar za siku nyingi, bado unaish pale pale au"... mda huo huelewi chochote kombe linajazwa juice basi inadhani ni ukarim...
Labda nikiri tu kuwa nilishawahi kuingia kwenye mfumo na hadi nainywa niliamini ananijua kweli. Lakini nilimlipa hela kwa mantiki kwamba namsapoti mtu anijuaye, anayehangaika kwa kujiajiri.

Hilo la kusema kwamba usipomlipa anatumia nguvu nilikuja kulisikia humu humu JF miezi kadhaa baadaye, sasa sijajua angefanyeje kama ningemwambia umenisimamisha na kunipa mwenyewe.

I wish nipite tena pale Karume
 
Dah oya mimi nikajuaga inanikutaga mimi tu, amenifanyia mara mbili mara ya mwisho nilikua na jamaa yangu juice mbaya kinyama sijui maji ya mtaroni alafu buku glasi, jamaa anajifanya kama anakufahamu mliishaonana huku anakupa juice unywe yupo na toroli kajaza jaba la juice
Kwa nini usikatae? Hivi unaanzaje kuparamia majuisi ya barabarani ambayo haujui yametengenezwaje?
 
Alijidai ananijua kabisa, na akataja had nnapokaa, kwenye story akaniwekea juisi nikanywa, nilivyomalza nikamuaga akaanza kuniambia nilipie nikamwambia sina kitu nikaondoka zangu, labda aliona mbavu nene akaogopa kuendelea kunidai
 
Mpumbavu sana huyu jamaa alishawahi kuniletea huo ujinga nikiwa na wife, tukanywa Juice yake na hatukulipa kitu tukasepa Karume kununua mahitaji yetu.
 

Attachments

  • 20240319_123421.jpg
    20240319_123421.jpg
    826.1 KB · Views: 1
Mkuu kwani akijaza hata jagi ni lazima unywe?....mfano ukimshukuruvkisha ukamwambia nimeshiba atakumezesha ili uchangie?...tatizo hapo halipo kwa muuzaji.
 
kama unajielewa kuna vitu huwezi fanya.....
kwa akili za kawaida tu mtu anakukaribisha juice kwani unashindwa kusema asante?
jiulize hamjuani na hata kama uliishi nae kitaa kimoja kuna ulazima wa kunywa juice yake?

mji una mengi ila washamba ni wengi sana na wanakuja jf kuandika ili tuutanbue upumbavu wao...

tabia za kike kushobokea vitu bila kusema asante
 
Na tolori lake yule jamaa shenzi kabisa,eti "bado uko palepale?"
 
Alinikamata mara moja tena alinibananisha kuwa tunaishi wote maeneo ya Chanika,ila sikunywa juice huwa sipendelei juice za mitaani.
 
Kuna watu wazima mnatapeliwa na boya kama huyo.?! Otherwise wakuja au ww ni bwegw mtozeni.
 

Unatembea zako ghafla unaitwa,


Zinaanza stori "Vipi, bwana habar za siku nyingi, bado unaish pale pale au"... Mda huo huelewi chochote kombe linajazwa juice basi inadhani ni ukarimu

Mnaendelea na story unajua pengine labda mliishi eneo moja huku ukizidi kuvuta picha umkumbuke.

Mwisho wa siku anakwambia "Ahsante kwa kunichangia, hiyo buku tu"

Pia Soma - Jeshi la polisi limebariki huu wizi Kariakoo?
Nchi imefika pabaya sana hii, mtoto wa kiume. Mpaka unasimamishwa ukasimama hadi unapewa juisi unakunywa na kujiramba ukiwa haujielewi halafu unapotakiwa kulipa ndiyo unastuka???
Upo salama kweli wewe?
 
Back
Top Bottom