Wakazi wa Handeni - Tanga mje yapi ndo maji yenu kati ya haya?

Wakazi wa Handeni - Tanga mje yapi ndo maji yenu kati ya haya?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

Mvutano mkali wa kimtazamo umeibuka mtandaoni kati ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Bara John Heche, na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, kufuatia ubora wa huduma ya maji wilayani Handeni, mkoani Tanga.Mjadala huo umeibuka leo Agosti 11, 2026, baada ya Heche kusambaza video inayonyesha maji machafu sana yanayotiririka bombani huku akihoji uwajibikaji wa Serikali." Hapa ni Handeni Tanga. Hawa eti ndio wanasema tunachochea wananchi wawachukie!!! Kwa ujinga kama huu wananchi wanawezaje Kukupenda?" ameonya Heche

Muda mfupi baadaye, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alijibu mapigo kwa kuposti video tofauti ikionyesha maji safi na salama yanayofaa kwa matumizi, akisisitiza kuwa hayo ndiyo maji yanayotumiwa na wananchi wa Handeni."Maji ya Handeni haya hapa," alieleza Msigwa kwenye video hiyo.Ushindani huo wa video mbili zinazokinzana umezua maswali na mjadala mpana miongoni mwa wananchi kuhusu ni video gani inayosawazisha hali halisi ya huduma ya maji wilayani humo.

Ila hapo kwenye maji ya Msigwa kama vile wamesahau kuondoa matope chini hapo....
 
Mbona kila kona ni hayo , nilijua ya kisimani kumb bombani
 
Back
Top Bottom