A
Anonymous
Guest
Wakazi wa Kimara King'ongo tumekuwa tukiteseka kwa kukosa huduma ya maji. Tangu maji yalipotoka Juni Mosi baada ya kulalamika Makao Makuu, hayajatoka tena.
Hili si jambo la kwanza kutokea. Mara nyingi hatupati maji hadi tupige simu na kulalamika, kana kwamba huduma hiyo ni ya bure.
Cha kushangaza zaidi, hakuna hata tangazo la kutoa tahadhari au taarifa kuhusu tatizo hilo.
DAWASA Ubungo hawaonyeshi kujali wateja wao, na inaonekana hawatambui kuwa kwa kukosa kutoa huduma wanajinyima mapato kupitia bili. Mwishowe, wananchi wanaendelea kubambikiwa bili wakati hawajapata huduma ya maji.
Pia soma ~ DAWASA: Tumeingia mtaani kuboresha huduma ya maji Mtaa wa King'ongo - Kimara