Wakazi wa Madaba wampongeza Rais Samia kwa Tsh bilioni 1.5, Mbunge Mhagama awaonesha vijana njia

Wakazi wa Madaba wampongeza Rais Samia kwa Tsh bilioni 1.5, Mbunge Mhagama awaonesha vijana njia

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
204f2ab1-2c15-44bf-8ff8-f319f5683b35.jpg


Wananchi wa Jimbo la Madaba wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt. Joseph Mhagama wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupata tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu.

Pongezi hizo zimetolewa Juni 4,2022 wakati wa tamasha la kutambua vipaji kupitia sanaa na michezo jimboni humo.

“Huko nyuma bajeti yetu ilikuwa haizidi shilingi milioni 500 licha ya kuwa tuna kilometa zaidi ya 600 zinazohitaji ukarabati wa kila mwaka, bajeti ikawa inatosheleza asilimia 5 tu ya mahitaji ya njia zote za Madaba.

“Katika awamu hii tumepata shilingi bilioni 1.5 ambayo ni asilimia 15 ya mahitaji ya barabarta za vijijini, hilo ongezeko kwetu ni kubwa, limegusa sehemu nyingi ya mahitaji licha ya kuwa changamoto bado zipo.
4e659581-9daa-46dc-b30b-38eafe7d44eb.jpg

“Tunajua bado ana maeneo mengi ya kukuza uchumi,” anasema Mbunge Dkt. Joseph Mhagama na kuendelea:

“Pia tumelenga kuwawezesha vijana wa Madaba kutambua na kuelewa fursa za kutambua uchumi kisha kuzichukua. Tuna ufugaji na kilimo, tumewaonesha vijana wanachoweza kufanya katika maeneo hayo.

“Katika tamasha hilo la Jumamosi tulipeleka wataalam kutoka maeneo tofauti ili kuzungumza na vijana wetu kuhusu fursa mbalimbali.

“Tatu ilikuwa kuibua vipaji hasa michezo na muziki, tuliwaleta waliofanikiwa huko nyuma ili kuwahamasisha na kuwaonesha namba gani vipaji vinaweza kuwatoa.”

"Ukiwemo mchezo wa soka na netball ambapo zaidi ya timu hamsini kutoka katika vitongoji vya Jimbo la Madaba vinatarajia kushiriki katika ligi yenye lengo la kuibua vipaji."
 
Back
Top Bottom