Wakazi wa Madale wapatwa na taharuki baada ya kuvamiwa na Nyati wa Porini

Nimekula sana swala chinichini hapo,kuanzia pale baobab secondary hadi chini ya wazo hill palikuwa kichaka baadaye wakaja wahuni na kuanza kuchimba mchanga pale vikawe na pori likayeyuka,sijui pakoje sasa hivi?
Dah maeneo hayo yalikuwa pori yani hadi boko kulikuwa pori
 
Wanaume wa Dar mnakubali vipi mboga ilete taharuki namna hii?
Mkuu temea chini mwanawane, tembo ana nafuu!

Nyati huwa anaua kidhalilishaji sana kuliko unavyodhania wewe.

Hapo kwanza Mungu kawaepusha.

Maeneo ya mjini kama hayo mtu ataanza kushangaa shangaa kwamba hili zagamba la kizungu nani kaliachilia!

Ndiyo hapo madhara yanapoanza kujitokeza.
 
Wakazi wa Madale wa jijini Dar-es-salaam wakumbwa na taharuki na wngine kukimbia makazi yao baada ya kuvamiwa na nyati ambaye hajulikani alipotoka.

Nyati huyo amejeruhi watu na baadhi ya mifugo...Kikosi kazi cha Ant-robbery cha mabwepande wamefika haraka na kumuua nyati huyo.

Kiongozi wa kikosi amesema nyati huyo ni jike hivyo kuna uwezekano wa kuwa na nyati dume maeneo hayo ya madale.

View attachment 1546056

Kisa kama hiki kilipata kutokea huko Mazimbu Morogoro, nyati alitokea na alijeruhi watu waliokuwepo mashambani kabla hajauawa na mgambo aliyekuwa na Shot gun yenye risasi moja tu, watu huku wakimtia moyo mgambo; kwamba ampige hiyo risasi kichwani bila kumkosa, mwanaume akajipinda akampa ya kichwa, ngoma ikaenda chini, loo, watu hawakujali hatari ya nyati aliyepigwa risasi, haraka walivamia bila kuacha kitu hadi maliasili wanafika waliambulia kwato tu🤣🤣.
 
Wakazi wa Madale wa jijini Dar-es-salaam wakumbwa na taharuki na wngine kukimbia makazi yao baada ya kuvamiwa na nyati ambaye hajulikani alipotoka.

Nyati huyo amejeruhi watu na baadhi ya mifugo...Kikosi kazi cha Ant-robbery cha mabwepande wamefika haraka na kumuua nyati huyo.

Kiongozi wa kikosi amesema nyati huyo ni jike hivyo kuna uwezekano wa kuwa na nyati dume maeneo hayo ya madale.

View attachment 1546056
Labda katokea saadani
 
Inakuwaje Anti- robbery unit itumike? Mali asili walikuwa wapi? Huyo mnyama si jambazi na hakupaswa kupigwa risasi. Ni utaalamu wa Mali asili ungetumika na kumrudisha anakostahili. Hili ni doa jingine kubwa. Tunasomesha wataalamu wasiotumika wanapohitajika.

Well said wangempiga risasi yenye sindano ya usingizi wakamrudisha hifadhi ya wanyama
 
hadi wapate iyo sindano si atakua kajeruhi wengi hivi unajua nyati aki charge kichaa chake kinakuwaje wabongo bwana kila kitu mnafanya siasa hilo eneo lote lilikua mapito ya wanyama wala sio zamani sana ndio mana nazani mwaka juzi walionekana tembo mitaa ya mbezi temboni kwa mbele kule jamaa wa tanapa akaelezea vizuri kuwa binadamu wamejenga kwenye corridors za kupita wanyama
 
Huyo nyati ni mjumbe alitumwa na mamlaka za pori kuja kujifuunza kutoka kwetu binadamu namna tunavyoishi
 
hadi wapate iyo sindano si atakua kajeruhi wengi hivi unajua nyati aki charge kichaa chake kinakuwaje wabongo bwana kila kitu mnafanya siasa hilo eneo lote lilikua mapito ya wanyama wala sio zamani sana ndio mana nazani mwaka juzi walionekana tembo mitaa ya mbezi temboni kwa mbele kule jamaa wa tanapa akaelezea vizuri kuwa binadamu wamejenga kwenye corridors za kupita wanyama

Halafu huko Dar hivi kuna askari pori hadi wawe na huo utaalam na hizo bunduki za sindano za usingizi?
 
Kikosi cha Anti Robbery kinaendaje kuuwa nyati!!?
mbona wameingilia mamlaka zisizo zao!?
 
Inakuwaje Anti- robbery unit itumike? Mali asili walikuwa wapi? Huyo mnyama si jambazi na hakupaswa kupigwa risasi. Ni utaalamu wa Mali asili ungetumika na kumrudisha anakostahili. Hili ni doa jingine kubwa. Tunasomesha wataalamu wasiotumika wanapohitajika.
Asante mkuu kwa kuliona hilo, nadhangaa sana mnyama pori akionekana mjini kinachofuata ni kuuwawa kwa risasi ya SMG. Kwanini tuna idara za wanyama pori na wataalamu wa mifugo? Inashindikana vipi kucontain mnyama pori na kurudishwa porini kwenye makazi yake?
Alafu tunasema tuko vizuri mdomoni wakati ni hovyo tu kimatendo
 
Mkuu temea chini mwanawane, tembo ana nafuu!

Nyati huwa anaua kidhalilishaji sana kuliko unavyodhania wewe.

Hapo kwanza Mungu kawaepusha.

Maeneo ya mjini kama hayo mtu ataanza kushangaa shangaa kwamba hili zagamba la kizungu nani kaliachilia!

Ndiyo hapo madhara yanapoanza kujitokeza.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] zagamba
 
Back
Top Bottom