Wakazi wa Magamba Songwe wachoma mazao yao ya ufuta mashambani mwao kupinga agizo la Mkuu wa Wilaya ya kutaka wauze kwa mfumo wa stakabadhi ghalani

Wakazi wa Magamba Songwe wachoma mazao yao ya ufuta mashambani mwao kupinga agizo la Mkuu wa Wilaya ya kutaka wauze kwa mfumo wa stakabadhi ghalani

Soya inastakabadhi gharani kinachofanyika wanamkopa mkulima halafu wanamcheleweshea pesa, wakati wa kulima hauwaoni lakini kwenye kuuza wanaleta masharti hapo ndio hua naona ccm hawana akili
 
CCM hawajawahi kua na akili kuanzia wao hadi viongozi wao, wameua korosho, wameua soko la kahawa, wameua soko la mbaazi, wameua soko la ufuta, wanaleta porojo ya stakabadhi ghalani wakati hawana mtaji, yaani wamejigeuza madalari wapuuzi hawa
 
Hao wakazi ni wapumbavu sana,mfumo huo ndio wenye faida kwao kwani hakuna mtu wa kati,wanauza kwa bei ya soko moja kwa moja na pesa zao hulipwa ndani ya masaa 48 tokea kufanyika kwa mnada,narudia tena ni wapumbavu sana wataendelea kulanguliwa hadi mwisho wa dunia kmmzao
 
Uganda Kahawa haijawahi kuuzwa chini ya 4000 hadi 5000 lakini Tanzania bei ya kahawa inashuka kila siku,
 
Hao wakazi ni wapumbavu sana,mfumo huo ndio wenye faida kwao kwani hakuna mtu wa kati,wanauza kwa bei ya soko moja kwa moja na pesa zao hulipwa ndani ya masaa 48 tokea kufanyika kwa mnada,narudia tena ni wapumbavu sana wataendelea kulanguliwa hadi mwisho wa dunia kmmzao

Wewe acha porojo mfumo wa stakabadhi gharani nchi kama vietnam mkulima analopwa cash anaondoka habari za kumlipa kidogo halafu nyingine asubiri mara afhulumiwe nani anataka, kawaulize mtwara na lindi wakulima wa korosho kilichowatokea
 
kwahiyo na mwakanj watachoma tena!!!

akili za masikini sio za kuamini.
 
Mkuu wa mkoa siku zake zinahesabika mtakuja kuniambia.
Raisi anapigana kurudisha wawekezaji mkuu wa mkoa anafukuza wawekezaji.Hao wakulima ni kati ya wawekezaji ambao wataisaidia serikali kupata kodi yeye amesababisha serikali kukosa kodi, atafukuzwa kazi.
 
Ukizuia muhindi kuingiza pesa kununua, muhindi wa Tanzania anaenda kusema zao fulani la tanzania lipo juu na halina ubora kama korosho ilivokua wanunuzi wakubwa duniani wakaelekea ivorycost, korosho ya bongo ikabaki inaoza nadhani hadi leo mnafahamu bado wanayo maghalani
 
Back
Top Bottom