Wakazi: Wakati wasanii wanafight kwenda kimataifa Mimi huko ndiyo kwetu

Mafanikio hayatokani na ubora. Songa aliwahi kusema "unaweza ukawa bora hata usipo win"

Trust me Wakazi anaweza asiwe kwenye top ten zenu ila kichwa chake ni asset kubwa kwa sanaa yetu.
Sijakataa ndio maana nimesema anaweza kutumika vyema kwenye angle nyingine ya tasnia, sio kuimba/ku rap tu. kwa upande wangu kwenye kurap hayupo hata top 30 yangu
 
Cjui kwa nini watu hawampendi wakazi swagger bovu....

Mimi ni mpenzi wa hip-hop... Miaka kama nane iliyopita nilijiunga na group la hiphop lilikua linaitwa "RAP BATTLES". Kwenye hilo group members walikua ni Wasouth Africa na west Africans km Nigeria, Ghana na kwingineko pia kulikua na members wengine kutoka ulaya....

Kwenye hilo group ilikua na battle za kutosha.... Kulikua na mashindano ya kuchana balaa.... Pia watu walikua wanapost ngoma mbali mbali kali za hip-hop.... Kuna ngoma moja ya rap kali sana Ili postiwa members wengi waliipenda wamefanya rappers wengi wa Africa, ni ngoma kali sana, flowz na michano hatari... Wakazi pia yupo kwenye hiyo ngoma kaua sana kwenye michano.... Nashangaa watu wanadai wakazi sio lolote kitu ambacho sio kweli.
 
Jamaa anaishi kwenye ulimwengu wa imagination tu huyu. Ha hit local wala internationally
 
Wakazi ni mjuaji na anafikiri tunaposema kutoboa kimataifa tuna maanisha kuishi au kufika Marekani…lah asha…Wakazi anatakiwa kujua kuwa kuna wasanii wanaishi marekani lakini hawajatoboa kimataifa and their still local artist…. Na hata yeye uko marekani bado hajafikia level ya kuitwa local artist kabisa na sidhani kama kuna anayejua kama anaimba!

Tunaposema international artist ni kutoboa nje ya mipaka yako ukiwa tayari umetoboa kwako halafu internatinal ni zaidi ya marekani kuna kusikika Ulaya,Asia na Africa!

Wakazi alifikiri akijua kingereza ingetosha kutoboa kuwa international artist au kuwa best artist lakini sivyo ndio maana alidhani akirudi Tanzania akaanza kuimba basi itakuwa rahisi kwake kutoboa na kusikika kimziki hadi nje ya Tanzania ikimaanisha Africa,europe and America….
Lakini imekuwa tofauti kwani Wakazi hata soko la nchini ameshindwa kupenya vilivyo sasa atapenya vipi kusikika America,Africa and Europe?

Wakazi ni muongeaji sana lakini ukweli ni kwamba swala la muziki limemshinda kwani toka mwanzo alishindwa kutofautisha kuwa mwanamziki bora na kujua kingereza au kujua kingereza na kuwa mwanamuziki wa kimataifa!
 
Weka link
 
Ujuaji mwiñgi... Alichokijenga hapa bongo ni kipi sasa?
 
Sijakataa ndio maana nimesema anaweza kutumika vyema kwenye angle nyingine ya tasnia, sio kuimba/ku rap tu. kwa upande wangu kwenye kurap hayupo hata top 30 yangu
Mi mwenyewe sijawahi kumkubali kwenye rap

Ila niulize kuhusu live performance hususani akitumia bendi

Kwenye ngoma hizi hizi ambazo Wakazi simuelewi lakini linapokuja swala la live band jamaa ni gwiji
 
Isije kuwa ww ndiye wakazi mwenyewe 🙌😂😂😂
 
Hivi ni kabila gan?? ...sijawasema wahaya [emoji23]
 
Uko sahihi Mkuu [emoji23]
 
Wakuu tuache masihara jamaa kwenye muziki ana Net Loss kubwa + Muda
Anyway anaforce anachokipenda sio mbaya😆😆
 
Mi mwenyewe sijawahi kumkubali kwenye rap

Ila niulize kuhusu live performance hususani akitumia bendi

Kwenye ngoma hizi hizi ambazo Wakazi simuelewi lakini linapokuja swala la live band jamaa ni gwiji
Ok, vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…