Wake wa Marais wetu na Mambo yao

Wake wa Marais wetu na Mambo yao

Walimu na wafanykazi angalieni vigezo na maneno haya na mjifunze muache UNAFIKI!
Na kama kuna mwananchi atakayeipigia kura ccm kama mambo yatabakia hivi...Basi na mimi nitakata tamaa rasmi.
Nawaachia wananchi KESI.

Wananchi wa mjini na wasomi ndio wanatakiwa kuelimishwa ,sio walimu na wananchi wa kijijini.

Walio na machungu ni walimu/wafanyakazi na wananchi wa vijijini .Hawa wa mjini na wasomi wengi ni wanafanya uhuni kwa maneno ya kejeli eti tukawaelimishe vijijini.Wanakijiji wanaelewa siasa vizuri kuliko watu wa mijini na wasomi.

Angalia statistics za wabunge tangu vyama vingi vilipoanza.Utagundua watu wa vijijini wamejaribu sana kubadili wabunge na vyama vya upinzani tofauti na wamjini na wasomi.
wamjini na wasomi chama chao ni CCM maana hawajawahi badili ama kama waliwahi basi ni kwa makosa.

Lakini hawa wa mjini na wasomi wamekua wakitoa kejeli kuwaelimisha watu wa vijini ni kwa vile tu wao wana uwezo wa kuvifikia vyombo vya habari na kwa hilo kurusha li-rungu la kejeli kwa wasiovifikia vyombo hivyo vya habari.
 
Mbunge ambaye alilivalia njuga suala la TICTS, Godfrey Zambi, wa Mbozi Mashariki kupitia CCM, amesema mke wa Rais Msataafu Benjamin Mkapa, Anna Mkapa, anaendesha vitendo vya wizi kupitia kampuni anayoiongoza ya BayPort Financial Services.

Hivi hawa watu wana kampuni ngapi jamani? Kila kukicha jina la kampuni yao mpya, hii nayo ilikuwa wapi mbona hatujaisikia hii? Damn!

Yaaani wana hii halafu pia na ANABEN au? duh!
 
Hivi hawa watu wana kampuni ngapi jamani? Kila kukicha jina la kampuni yao mpya, hii nayo ilikuwa wapi mbona hatujaisikia hii? Damn!

Yaaani wana hii halafu pia na ANABEN au? duh!

Hiki kipato cha familia Mkapa hakuki consider aliposema anaishi na pensheni. Ni kama hakusema ukweli.

Angekuwa nchi za watu kuna mwana media angesha mrushia swali barabarani, sio mpaka aje ukumbi wa Maelezo. Kama yule questioner wa Mugabe kwenye hallway, na alikuwa kazungukwa na wapambe. Naona sasa nifikirie seriously kuhusu kuanzisha ki BBC changu Bongo, japo sijasomea hayo mambo.
 
Kuhani... huhitaji kuanzisha Bongo.. hata hapo ulipo unaweza ndugu yangu. Natafuta mapatner... nikupe contacts uwahoji unachotaka kuwahoji halafu uturushie, ili na wengine tujifunze? Itakuwa msaada mkubwa sana.
 
Mbunge ambaye alilivalia njuga suala la TICTS, Godfrey Zambi, wa Mbozi Mashariki kupitia CCM, amesema mke wa Rais Msataafu Benjamin Mkapa, Anna Mkapa, anaendesha vitendo vya wizi kupitia kampuni anayoiongoza ya BayPort Financial Services.

Kauli ya Zambi, itaibuka kesho kwenye magazeti kwa kuwa wanayoyasema bungeni yanakuwa na kinga. Alisema ndani ya Bunge jana usiku, wakipitisha bajeti ya WIzara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Waziri MAghembe hakuweza kutoa majibu mwafaka kiasi cha wabunge kuguna kuonyesha kutoridhishwa na majibu yake ya kubabaisha.

Mbunge huyo amesema kampuni ya Mama Mkapa na wenzake inawatoza riba ya karibu asilimia 200 watumishi wa kipato cha chini wakiwamo waalimu, kitendo ambacho alisema ni sawa na wizi wa wazi.

Zambi alisema: “Kampuni hii inakopesha watumishi na hususani walimu kwa sababu ndiyo walioleta malalamiko kwangu kule Mbozi, Mwalimu akikopa milioni moja anatudisha milioni tatu, sasa hii ni mikopo ya wapi kama siyo wizi wa waziwazi kwa walimu, na mimi nina mifano Waziri akitaka naweza nikampa hizi taarifa"


Kumbe mwizi kama Anna Che-nkapa aitwe vipi? Kibaka!
 
Hiki kipato cha familia Mkapa hakuki consider aliposema anaishi na pensheni. Ni kama hakusema ukweli.

Angekuwa nchi za watu kuna mwana media angesha mrushia swali barabarani, sio mpaka aje ukumbi wa Maelezo. Kama yule questioner wa Mugabe kwenye hallway, na alikuwa kazungukwa na wapambe. Naona sasa nifikirie seriously kuhusu kuanzisha ki BBC changu Bongo, japo sijasomea hayo mambo.

Fisadi Mkapa atwambie ukweli kwamba mbali ya kuishi kwa pensheni pia yeye na fisadi mkewe wanakupua toka kwa walimu na pia wanakupua toka kwa Watanzania kupitia mkataba wa 'kampuni yao ya Kiwira' na TANESCO ambao unawalipa shilingi 146 millioni kwa siku.

Jamani watu wengine wana ulafi wa hali ya juu! Hawawaonei huruma hata Watanzania wenzao pamoja na kuwa wana vipato vidogo. Unamkopesha mtu millioni halafu akulipe milioni 3! Huu ni wizi na pia ni unyang'au!! Huyu mama ashinikizwe awarudishie hao walimu hela zote za ziada alizowaibia hao walimu kwa kuwatoza riba kubwa isiyostahili.

Kuhani kuna gazeti kama sikosei THIS DAY lilishaandika maswali kwenye article moja ambayo yalikuwa yameelekezwa kwa Fisadi Mkapa, lakini ububu ndiyo staili yake siku hizi lakini na sisi hatutasita kumsakama kila kona ya dunia hii.
 
Anna Mkapa ameitumia IKULU kwa asilimia 100, mfuko wa Fursa sawa ulikuwa kwa ajili ya wachagga na familia yake ilikuwa chombo cha kuwatapeli mabalozi na mashirika mbalimbali.
 
Jamani hizi financial institution zingine zinatia kichefu chefu maana zinakuja kwa mgongo wa kumkomboa mfanyakazi au mfanya biashara au mkulima, simply kwa nia ya kumuibia.
Watu wengi hapa Tanzania nimegundua when they just get seduced to take loans hawajiulizi maswali zaidi ya kukimbia kuchukua. That's where the problem arises.
Unaona kwa ripoti ile kampuni hiyo imeweka wazi kwamba wanalipisha riba ya 70% to 90% kwa mwaka na mkopo unakwenda hadi miaka 3 hii ni riba kubwa sana!
Kama walivyoshauri wengi kwa riba hiyo na hasa kama ni compound interest inaweza kuwa mwisho wa mkataba mkopaji karipa 200% hii si ajabu.
Kinachoumiza mioyo ya watu wengi ni kwamba Mama Mkapa akijua wazi kwamba hili linafanyika kwa kutumia kampuni yake huku akiaminiwa kama mke wa kiongozi safi aliwaingiza walimu mkenge bila kuwambia ukweli.
Na wanaowalaumu walimu wanawalaumu bila sababu maana walimu si wataalam wa financial deals, bali kwa shida zao wanatafuta kila anayeweza kuwasaidia wamalize shida walizo nazo kama elimu kwa wana wao, afya kwa matibabu ghali ya Tanzania na kununua mahitaji ya muhimu kwa ajili ya familia zao.
Hapa ndipo tu mama huyu anastahili kulaumiwa. Otherwise ni fisadi kama mafisadi wengine.
By the way mbona hawamu mbili zilizopita ma first lady wamekuwa mabingwa wa ufisadi?
Mama JMK b careful nawe usije ukatufisadi basi!

Kwikwikwi... hivi hujui ndugu yangu??

Naye kaisha anzisha ka kwake kanaitwa WAMA ( wanawake na Maendeleo) kama kawaida kaisha chotewa bilions toka japan, USA na kwingineko.. siyo kwamba atakuwa fisadi tayali ni..., na huko kwao kaisha shusha bonge la school kwa hela hiyo hiyo..

Kinacho nikera hiyo mifuko wanaifanyia umatonya kwa kutumia kigezo cha watanzania masikini wakati wanaishia kujazia mifuko yao!
 
Yaani ulafi mwingine bana!Haka kamama hakajashiba kweli mihela yote hiyo kaliyo kwapua sasa kamehamia kwa walalahoi wa mwisho kabisa kimshahara serikalini.
 
Yaani ulafi mwingine bana!Haka kamama hakajashiba kweli mihela yote hiyo kaliyo kwapua sasa kamehamia kwa walalahoi wa mwisho kabisa kimshahara serikalini.

sheikh binadamu anashiba chakula...lakini hakuna binadamu anayeshiba pesa, hiyo ndiyo historia inavyosema toka enzi ya kaisari.
 
Mh! Tunahukumu mapema mno. Au nasi humu JF tuna KINGA kama ile ya ndani ya BUNGE?
 
sheikh binadamu anashiba chakula...lakini hakuna binadamu anayeshiba pesa, hiyo ndiyo historia inavyosema toka enzi ya kaisari.

kwi kwi kwi lakini tamaa nyingine yakhee zimezidi mpaka kwa walimu duh! walimu mshahara wanao lipwa ni kiduchu sana ukilinganisha na gharama za maisha.
 
with an interest rate btw 70-90 % sishangai kuona baada ya miaka 3 tu analipa milioni 3 kutoka deni la milioni 1. it makes perfect sense

nafikiri mbunge alitakiwa kulalamika kuwa interest rate ni kubwa mno, na sio kumwita mama mkapa mwizi moja kwa moja.

wakimfikisha mahakamani .....watamumbua mbunge wetu!
 
Wananchi wa mjini na wasomi ndio wanatakiwa kuelimishwa ,sio walimu na wananchi wa kijijini.

Walio na machungu ni walimu/wafanyakazi na wananchi wa vijijini .Hawa wa mjini na wasomi wengi ni wanafanya uhuni kwa maneno ya kejeli eti tukawaelimishe vijijini.Wanakijiji wanaelewa siasa vizuri kuliko watu wa mijini na wasomi.

Angalia statistics za wabunge tangu vyama vingi vilipoanza.Utagundua watu wa vijijini wamejaribu sana kubadili wabunge na vyama vya upinzani tofauti na wamjini na wasomi.
wamjini na wasomi chama chao ni CCM maana hawajawahi badili ama kama waliwahi basi ni kwa makosa.

Lakini hawa wa mjini na wasomi wamekua wakitoa kejeli kuwaelimisha watu wa vijini ni kwa vile tu wao wana uwezo wa kuvifikia vyombo vya habari na kwa hilo kurusha li-rungu la kejeli kwa wasiovifikia vyombo hivyo vya habari.

Ninachosubiri hapa bado ni vigezo vya credit evaluation process.
CREDIT EVALUTION METHODS TO BE MORE SPECIFIC.
Wakijibu hili tutajuwa kama walimu walitendewa haki ama la.
Zaidi ya hapo ni porojo tu.
 
Leo ndio anajua hilo?Tena ni mwizi aliyebobea hao ndugu zake aliwowajaza TRA si ni wizi huo?

Sidhani kama ni hivyo mkuu, ni suala la wakati tu. The time has come to call spade a spade!
 
Ndugu zangu kwa sasa hatuna njia mbadala wa kupambana na hawa mafisadi na wezi isipokuwa kuwashikia bango tu bila kuwaonea haya. Na wale wote wanaojaribu kuwatetea ama kwa makusudi au kwa kutokujua, kazi ni mtindo moja - tuwasute kwa nguvu zote. Pamoja na kwamba ndio wenye nyumba, tuhakikishe hawalali kwa kuzidi kupaza sauti hata ikibidi tutumia tarumbeta.

Na hii ifanyike kote tu iwe misikitini, makanisani, majumba ya starehe, kwenye burudani, kwenye misiba au harusi na popote pale tutakapokutana nao. Kwa mara ya kwanza machungu ambayo wametusababishia tuyaanike kila tukipata mwanya iwe magazetini, kwenye blog, radioni hata safarini iwe kwenye anga, nchi kavu na majini. Pote tutakapokusanyika gumzo liwe moja tu - kuwakoma hawa bila huruma.

Pia tusiwaonee haya ndugu zao, jamaa zao, rafiki zao na wanaonufaika kwa nama moja au nyingine na ufisadi wao. Kuendelea kusubiri sheria ichukue mkondo wake ni kuwapalilia njia za kutuzuga zaidi. Wakati ni HUU.
 
Ninachosubiri hapa bado ni vigezo vya credit evaluation process.
CREDIT EVALUTION METHODS TO BE MORE SPECIFIC.
Wakijibu hili tutajuwa kama walimu walitendewa haki ama la.
Zaidi ya hapo ni porojo tu.

Hiyo 70-90% interest ni kubwa mno! Lakini kumbuka kuwa hii rate inaweza kuwa kubwa kiasi hiki ku-reflect kiasi cha RISK mkopeshaji anayochukua kukopesha walimu. Ina maana, kuna uwezekano mkubwa walimu kushindwa kurudisha hizo hela na pengine kuingia mitini sub-prime style....However, they are still blood sucking machines.
 
Ndugu zangu kwa sasa hatuna njia mbadala wa kupambana na hawa mafisadi na wezi isipokuwa kuwashikia bango tu bila kuwaonea haya. Na wale wote wanaojaribu kuwatetea ama kwa makusudi au kwa kutokujua, kazi ni mtindo moja - tuwasute kwa nguvu zote. Pamoja na kwamba ndio wenye nyumba, tuhakikishe hawalali kwa kuzidi kupaza sauti hata ikibidi tutumia tarumbeta.

Na hii ifanyike kote tu iwe misikitini, makanisani, majumba ya starehe, kwenye burudani, kwenye misiba au harusi na popote pale tutakapokutana nao. Kwa mara ya kwanza machungu ambayo wametusababishia tuyaanike kila tukipata mwanya iwe magazetini, kwenye blog, radioni hata safarini iwe kwenye anga, nchi kavu na majini. Pote tutakapokusanyika gumzo liwe moja tu - kuwakoma hawa bila huruma.

Pia tusiwaonee haya ndugu zao, jamaa zao, rafiki zao na wanaonufaika kwa nama moja au nyingine na ufisadi wao. Kuendelea kusubiri sheria ichukue mkondo wake ni kuwapalilia njia za kutuzuga zaidi. Wakati ni HUU.

Sasa tunaanza kuwaaibisha, kuwazomea, kunyanyua mabango kila waendako...Wakuu mikoani na nje ya nchi inabidi tuanze juhudi za ku-print mabango na kuanza harakati. Kuna jamaa kadhaa wanaharati niliko wako tayari.
 
Date::7/17/2008
Anna Mkapa ana hisa chache katika kampuni ya Bayport
Na James Magai

WAKATI Kampuni ya Bayport Financial Services imethibitisha kwamba viwango vya riba wanazokata wateja wanaokopa fedha ni kikubwa zaidi ya kinachokatwa na mabenki nchini, pia imeeleza kwamba Mama Anna Mkapa ana hisa kwenye kampuni hiyo.


Meneja wa Tawi la Bayport nchini, Robert Washokera, akizungumza na Mwananchi jana, alisema kwamba ingawa viwango vyao viko juu lakini havizidi asilimia 50 kama serikali ilivyoagiza.


Alisema wanatoza viwango hivyo tofauti na benki kwa kuwa wao hawana ankaunti yoyote na wateja kama ilivyo kwa benki, ambapo kutokana na wateja kuwa na ankauti katika benki hizo kuna makato ambayo benki zinapata zikiwezo gharama za huduma mbali ya kiwango cha riba kwa mkopo.


Hata hivyo, Washokera alipotakiwa kutaja viwango vya riba wanavyotoza, hakuwa tayari kwa madai kwamba si vema kibiashara kutaja viwango hivyo kwenye vyombo vya habari.


''Unajua biashara ni ushindani, sasa si vema kutaja viwango hivyo kwenye media (vyombo vya habari) kwa sababu ni sawa na kumpa adui yako mbinu unazotumia. Lakini kama nilivyosema viwango vyetu haviko nje na tamko la serikali na mtu yeyote akija tunampa na yeye ndiye anachagua kiwango atakachoridhika nacho,'' alisisitiza Washokera.


Kadhalika, msemaji huyo alisema kwamba madai yaliyotolewa na Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM), Godfrey Zambi bungeni wiki hii kwamba Mama Anna Mkapa ndiye mmiliki wa kampuni hiyo si sahihi, kwa sababu anamiliki kiwango kidogo cha hisa.


''Mama Anna Mkapa na Kaduma si wamiliki wa kampuni hii bali wao ni wanahisa tu. Wao ni miongomi mwa Wakurugenzi tu kwa sababu wamenunua hisa katika kampuni hii na hisa zao ni ndogo mno,'' alisema Washokera.


Washokera alisema ingawa Mama Anna Mkapa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ibrahim Kaduma ni miongoni wa Wakurugenzi wa kampuni hiyo kutokana na kuwa na hisa, hawahusiki na wala hawajui shughuli zozote za utoaji mikopo katika kampuni hiyo.


?Wao ni sawa mtu yeyote aliyenunua hisa TBL (Kampuni ya Bia nchini), yeye anachojua ni gawio lake tu kwa hiyo haiwezekani TBL ikiuza mazao yenye hitilafu, umtaje huyu mwenye hisa mmoja tu kuwa ndiye anahusika,? alisema Washokera.


Maelezo ya Washokera yanafuatia kauli ya Zambi bungeni wakati wa mjadala wa kupitisha makadirio ya matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwamba Bayport inayomilikiwa na Mama Mkapa na Kaduma, inawaibia walimu kwa kukata fedha nyingi kutokana na mikopo kidogo.


''Kuna kampuni ya Bayport inamilikiwa na mke wa Rais Mstaafu, Anna Mkapa. Lakini wapo wengine wazito walioitumikia nchi hii, kama Kaduma. Mwalimu akikopa Sh1 milioni analipa Sh3milioni. Hii imetoka wapi kama si wizi?'' alihoji Zambi bila kueleza muda wa ulipaji wa mkopo ulitolewa na kampuni hiyo.


Washokera alidai kwamba kauli ya mbunge huyo kuwa Mama Anna ndiye mmiliki wa kampuni hiyo ililenga kumchafua jina pengine kutokana na baadhi ya tuhuma ambazo zimewahi kuibuliwa zikimuhusisha na mumewe, Rais Mstaafu Benjamini Mkapa.


''Kama alipata taarifa hizi kwa wananchi wake, hatujui ni kwa nini yeye alishindwa kuwahoji zaidi ili wampe taarifa za kina na sahihi. Lakini pia tunashangaa ni kwa nini alishindwa kwenda walau halmashauri tu akapata historia ya kampuni maana huko kuna nyaraka zinaonyesha na majina ya wakurugenzi wote,'' alihoji Washokera.


Washokera pia alisema kampuni hiyo ambayo imeanza kufanya shughuli zake hapa nchini mwaka 2006 ni ya Afrika Kusini na kwamba kwa sasa ina matawi katika nchi tano katika Afrika.


Alizitaja nchi hizo mbali na Afrika Kusini kwenye makao makuu kuwa ni Tanzania, Uganda, Ghana, Zambia na Mauritius.


Kuhusu tuhuma za kuwaibia wateja wao, Washokera alisema madai hayo hayana msingi kwa kuwa kampuni hiyo inaendesha shughuli zake kwa taratibu za wazi na kwa mujibu wa kanuni na taratibu za nchi.


Alisema kila mtu anayehitaji mkopo kwanza huelezwa masharti na taratibu za mikopo ikiwa ni pamoja na kiwango cha makato na riba na muda wa kurejesha mkopo, ambao huanzia mwezi mmoja hadi miaka mitano na iwapo ataridhika ndipo anapewa fomu ambazo atazijaza na kisha kusaini.


Alisema kiwango cha makato hutegemeana na muda wa kurejesha mkopo na kwamba ikiwa kipindi cha kurejesha mkopo ni kirefu basi kiwango cha makato kinakuwa ni kidogo, lakini riba yake inakuwa ni kubwa kidogo tofauti na mkopo unaorejeshwa katika kipindi cha muda mfupi ambapo kiwango cha makato huwa kikubwa, lakini riba yake inakuwa ni ndogo.


Akizungumzia madai ya kuwakata viwango vikubwa wateja wao, Washokera alisema malalamiko hayo yamekuwapo na wamekuwa wakiyapokea ofisini kwao kutoka kwa wateja, lakini akasema kuwa hayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya wateja ambao mwisho wa mwezi kujikuta hawana salio baada ya makato.


''Hii inatokea kwa sababu kuna watu wengine ambao wamekopa sehemu mbalimbali sasa inapofika mwisho wa mwezi wanajikuta hawana kitu ndio wanakuja hapa na kuanza kulalamika kuwa tunawakata viwango vikubwa licha ya kwamba walikubaliana na viwango vyetu,'' alisema Washokera na kuongeza:


''Kuna mama mmoja alikuja hapa akiwa ana shida ya shule ya mtoto, tulipoangalia akiba yake alikuwa habaki na kitu, kumbe alikuwa amekopa katika taasisi tatu tofauti, ikiwemo NMB, Baclays na Nufaika.''


Alisisitiza kuwa hadi sasa wamekwishatoa mikopo kwa watumishi wengi wakiwemo wafanyakazi wa wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na katika manispaa nyingi lakini hawajawahi kusikia malalamiko yoyote kutoka kwao.


Alisema kabla mteja hajapewa mkopo kuna fomu ambazo anazijaza baada ya kuzisoma na kukubaliana na masharti na taratibu zao.


''Haiwezi kuingia akilini kuwa mtu amesaini kitu asichokielewa kwani kuna mambo ya msingi ambayo kwanza mteja inabidi ayaelewe. Anapaswa kufahamu kiasi cha mkopo muda wa kurudisha mkopo, kiwango cha riba atakachokatwa,'' alisema.


?Wapo wengine ambao wameomba kuongeza (mkopo) hata kabla hawajamaliza kulipa mkopo wa kwanza na wale ambao ulipaji wao hauna matatizo tunawakubalia.


''Hivi juzi kuna wengine nao walikuja hapa kutoka Kilwa wakiwa na mbunge wao wa zamani wakilalamika kuwa tunawakata kiwango kikubwa, lakini tulipokaa nao na kuwaeleza matokeo yake ni kwamba wote waliomba kuongeza mkopo na mbunge wao huyo akabaki anashangaa.''


''Kuna mteja mwingine kutoka Kibaha alifika ofisini kwetu kulalamika kuwa tunamkata kiwango kikubwa kiasi kwamba habaki na kitu. Baada ya kugundua kuwa tatizo lake ni kwamba alikuwa habakii na akiba yoyote tulimpa njia za kumsaidia na tukamtaka achague, matokeo yake alichagua kuongeza mkopo tena na tukampa Sh600,000 kwa kiwango kile kile cha makato,'' alisema Washokera.


Alisema kuna watumishi wengine wanakuwa wakiomba mkopo na kuomba wakatwe hata zaidi ya nusu ya mshahara wao kwa mwezi, lakini wamekuwa wakikataa kwa kuwa hilo ni nje ya utaratibu wa serikali na badala yake wanajaribu kuwapa ushauri mwingine namna ya kufanya.


"Kuna mama mmoja alikuja hapa akihitaji mkopo lakini tulipoangalia 'balance' yake ilikuwa ni sifuri, alikuwa amechukua mkopo NMB, Barclays na Nufaika,'' alisema Washokera na kuongeza:


''Kwa kuwa alilia sana tulichokifanya ni kuangalia ni wapi alikuwa anakaribia kumaliza deni hivyo tulikwenda NMB wakatuthibitishia kuwa alikuwa anatarajia kumaliza deni mwezi uliokuwa unafuata, hivyo tulikubali tukampa mkopo wa jinsi hii wapo wengi wanaokuja hapa.''


Washokera alisema kwa sasa kampuni hiyo ina matawi manne jijini Dar es Salaam na mikoani hadi sasa wana matawi tisa na kwamba kwa hali hiyo jinsi walivyojizatiti si rahisi kufanya upateli kama huo.


Tuma maoni kwa Mhariri
 
Mwandishi Wetu
Daily News; Thursday,July 17, 2008 @19:01


Kampuni ya Huduma za Fedha ya Bayport iliyolalamikiwa bungeni majuzi kuwa inawatoza walimu riba kubwa baada ya kuwakopesha, imesema mke wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Anna, ni mmoja wa wakurugenzi wake, lakini hana hisa binafsi anazomiliki kwenye kampuni hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Bayport, Etienne Coetzer, alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosambazwa Dar es Salaam leo kuwa Anna Mkapa anawakilisha taasisi ya Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) ambayo inamiliki asilimia moja ya hisa za kampuni hiyo.

Kampuni hiyo pia imesema Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ibrahim Kaduma ni mmoja wa wakurugenzi kupitia kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL) ambayo nayo inamiliki sehemu ya hisa katika Bayport. Haikuelezwa kiasi cha hisa zinazomilikiwa na NICOL.

"Mama Mkapa na Kaduma wameteuliwa na taasisi hizo mbili kuziwakilisha kwenye bodi ya wakurugenzi ya Bayport," ilifafanua taarifa hiyo. Bayport imetoa ufafanuzi huo baada ya Mbunge wa Mbozi Mashariki Godfrey Zambi (CCM) kutoa tuhuma nzito bungeni na kukaririwa na magazeti kadhaa leo, kwamba watu hao wawili kuwa wanamiliki kampuni ya Bayport ambayo alidai inawaibia walimu kwa kuwatoza riba ya juu.

Mbunge huyo alifafanua kuwa kampuni hiyo imekuwa inawakopesha walimu lakini inawatoza riba kubwa inayofikia asilimia kati ya 167 na 200. Alitoa mfano kuwa mwalimu anayekopa Sh milioni moja amejikuta analipa Sh milioni 3, jambo alilodai ni wizi kwa watumishi hao wenye kipato kidogo.

Wakati Zambi anawasilisha hoja yake bungeni, hakuwasilisha nyaraka zozote zinazothibitisha kuwa Anna Mkapa na Kaduma ni wamiliki wa Bayport. Lakini hata hivyo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Jumanne Maghembe alimwahidi kuwa atafuatilia malalamiko hayo ya walimu.

Taarifa ya leo ya Bayport imewataja wanahisa wengine mbali na EOTF na NICOL kuwa ni Africa Yetu na Bayport Management Ltd. Kaduma ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ni mwanahisa katika kampuni ya NICOL na Anna Mkapa ni Mwenyekiti wa EOTF.

Kuhusu riba, kampuni hiyo ilisema inatoza riba inayotokana na gharama halisi za mkopo. "Bayport inatoza riba yenye ushindani katika sekta ya masoko na siyo kwamba sisi riba yetu ni ya juu." Hata hivyo haikutaja kiasi cha riba inayotozwa. Coetzer alisema kampuni imeshtushwa na habari za Mbunge huyo alizozitoa, wakati Bunge limekaa kama kamati ya matumizi na akihitaji ufafanuzi kutoka kwa waziri sababu ya kampuni hiyo kutoza riba kubwa kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom