Yapo mambo mengi tu Mkuu lakini kwanza kabisa KATIBA,sheria mama ya nchi, tuna katiba kama ya kikoloni koloni hivi,au kibabe, katiba tuliyonayo sasa inafaa zaidi katika mfumo wa chama kimoja kuliko wa vyama vingi,na ndo maana inaonekana kama katiba inayoegemea chama tawala. Ntakupa mfano wa katiba ya Zanzibar ambayo naifahamu vizuri,katika tafsiri ya maneno tu, neno "serikali" linamaanisha "serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" au neno "rais" linaamaanisha "rais wa zanzibar na Mw'kiti wa baraza la mapinduzi". haya ni makosa ya kitafisiri tu lakini athari yake ni kubwa katika mfumo siasa za kisikuhizi,vp katika mfumo wa vyama vingi uwe na serikali ya kimapinduzi? au baraza la mapinduzi? n.k na hata katiba ya muungano ina kasoro kadhaa za namna kama hiyo na zaidi.
Suala jingine la kurekebishwa ni sheria kandamizi, rejea taarifa ya tume ya Jaji Nyalali, ametaja sheria nyingi kandamizi, zinazotakiwa kufutwa au kurekebishwa.Utaona kama mambo madogo tu lakini yanalitafuna taifa vibaya sana, leo tunashindwa kumrudi mtu tuliyemkabidhi dhamana za uongozi akatuibia kwa sheria hizi hizi mbovu mbovu,wakati wenzetu kama Malawi,Zambia n.k wameweza!
Kero za Muungano mfano, tunarejea pale pale kuwa tatizo ni katiba, same conlusion give by Aboud Jumbe and other founders of Union.