NASA should go to court so as to petition these amendments. Uhuru is preparing clauses in the law that will enable him rig the election. He is doing everything to remain in office, so NASA be careful.
Hamna cha kuiga mkuu viongozi wa Afrika baba mmoja mama mmoja.Siasa za kenya wakati mwingine zinafundisha na kuwa mfano wa kuigwa lakini wakati mwingine zinasikitisha sana
Nakubaliana na wewe mkuu yaani katiba inawa favor wanasiasa badala ya wananchi. Kwaiyo ukiingia kiundani wananchi wanachezeshwa shere tu mkuu.Usianze kujishuku na kujihami mapema, mimi nimeuliza maswali ungenijibu badala ya kunishutumu. Sijasema hakuna mambo mazuri yaliyopatikana, ila nimesema mengi mazuri yanawalenga watu wakubwa na wanasiasa, na nimekua very specific kuainisha maeneo ambayo yanawagusa wananchi, hivi kweli bila aibu unasema ukabila Kenya umepungua, kweli unasema maneno hayo wewe bila aibu hata chembe? 2) Hivi kweli rushwa imepungua Kenya?, mwaka jana imeshika namba tatu duniani, 3) Hivi unataka kusema usalama wa raia wa Kenya umeimarika wakati Kenya imekua kinara Afrika katika extra judicial killings 2016, 4) Hivi unasema pengo la masikini na tajiri Kenya linapungua?. 5) Unataka kusema malalamiko ya ardhi yaliyofanyiwa kazi na tume ya wako yamefanyiwa kazi?, 6)Unataka tuamini kiwango cha unemployment kinashuka au kinaongezeka?. Kama unasema katiba mpya umeyapatia ufumbuzi hayo na ukatupa na ushahidi, basi kweli ni katiba nzuri, vinginevyo ni nyie wachache wanasiasa na watu wa hali nzuri ndiyo mnaouona huo uzuri
Umeongea facts kabisa mkuu.Mimi ninaamini katiba nzuri ni ile inayoleta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi walio wengi, ambao ni masikini, sio inayotoa ufumbuzi wa matatizo ya wanasiasa, ukisikiliza kwa makini sana huo unaoitwa uzuri katika katiba hiyo ya Kenya, mengi sana yanawalenga wanasiasa na viongozi wa juu, sio wananchi, mambo kama haya ya kupinga matokeo, kumpunguzia rais madaka na kadhalika, karibu yote yanawagusa wanasiasa au watu wa tabaka la juu. Kuna matatizo ya msingi yanawakabili wakenya tangu wapate uhuru 1963, tujiulize tangu katiba nzuri ipatikane, je kuna unafuu gani uliopatikana katika;
1) Kupunguza ukabila unaohatarisha nchi kugawanyika vipande vipande
2)Rushwa inayozidi kuongezeka na kuzidisha ugumu wa maisha
3) Kupunguza pengo la umasikini kati ya tajiri na masikini
4) Kushughulikia dhuluma iliyosababisha wachache matajiri na wanasia kujiridhisha ardhi ya wananchi wanyonge walioporwa na wakoloni kama ilivyopendekezwa katika The wako report
5) kuimarisha usalama ambao unazidi kuzorota
6) kuongeza ajira kwa vijana
7)Upatikanaji wa chakula cha uhakika(Food security)
Kama katiba haiwezi kuwapatia wakenya majibu katika hayo, basi huo uzuri wa katiba kwao hawatouona zaidi ya kuhudhuria mikutano ya wanasiasa ambao ndiyo wanufaika wakubwa wa hii katiba nzuri.
Nawakilisha
Lakini ki msingi sio siasa za Kenya mbovu sababu sheria,mikakati ,kupunguzwa uwezo wa offisi ya rais ,tume kadhaa zilizopo - hizi zote ni ishara kwamba siyo siasa mbovu .Sema kile kibovu ni ubinafsi wa wanasiasa ndio unaharibu.Ndiyo ninawasngaa, nilianza kwa kusema siasa za Kenya ukizifuatilia unaweza kuwa chizi, nikamalizia kwa kusema "likiisha hili linakuja lingine, kwanini lakini?", wakitoka NASA, wanakuja Jubilee, hakuna hata wakumuamini.
Kwani siasa maana yake ninini?, siasa haimaanishi katiba tu, au sheria tu, hapana, ni mchanganyiko wa yote hayo na muhimu zaidi ni kwa jinsi gani watu au viongozi wanavyoishi au kuongoza kwa kufuata sheria na taratibu mlizojiwekea, inawezekana msiwe hata na katiba, lakini viongozi wakawa wanaongoza vizuri kwa kufuata misingi ya jamii husikaLakini ki msingi sio siasa za Kenya mbovu sababu sheria,mikakati ,kupunguzwa uwezo wa offisi ya rais ,tume kadhaa zilizopo - hizi zote ni ishara kwamba siyo siasa mbovu .Sema kile kibovu ni ubinafsi wa wanasiasa ndio unaharibu.
Baada ya kuiga Eurobond na SGR money unategemea nn?NASA should go to court so as to petition these amendments. Uhuru is preparing clauses in the law that will enable him rig the election. He is doing everything to remain in office, so NASA be careful.
Ruto alikuwa against Katiba hii..Pitia vizuri utaona alifanya na kampeni nchi nzima kuipinga.Siasa za Kenya ukizifuatilia sana unaweza kuwa chizi, hawa hawa Uhuru na Rutto walipambana sana kupata katiba mpya, baadae wakawa wanapita kuisifia na kuiaminisha dunia kwamba katiba ya Kenya is the best, hata vumbi halijafutika tayari imeonekana na dosari... wanasemaga siku ya kufa nyani, miti yote aliyozoea kuiparamia siku zote inaanza kuteleza...wakenya chokochoko hii, kuna kitu mnakitafuta, Mungu hajaribiwi, ukibeep yeye anapiga...chondechonde..kila siku mnakuja na jipya..kwanini lakini?
Majority rule inayopingana na Katiba. Wewe punga kweluKwani hao wawili wantofautiana vipi na hawa NASA jameni? Wanasiasa wa NASA walifurahia sana majority ruling kule supreme court sasa iweje ati majority vote bungeni nayo sasa ni kitu kibaya?
NASA should go to court so as to petition these amendments. Uhuru is preparing clauses in the law that will enable him rig the election. He is doing everything to remain in office, so NASA be careful.
Aisee usimkufuru Mungu nyie mna raisi bora kabisa katika afrikawakati mwingine huwa natamani uongozi wa Magu kidogo....yaani hapa Kenya imekuwa ni sarakasi za kipumbavu for the last 6 months...vuta nikuvute ujinga mtupu...siasa za kijinga kwel kwel...wakati nchi kama ethiopia na tanzania ziko zinakimbia kwa haraka, Kenya ni IEBc, sijui Supreme court, sijui Nasa, sijui Jubilee, sijui election date imeahirishwa, sijui Chiloba, sijui maandamano, sijui matusi...smh
Acha kutuingiza choo cha kike wewe, taarifa zote zinaonyesha hayo niliyokutajia yanaongezeka mwaka had
Acha kutuingiza choo cha kike wewe, taarifa zote zinaonyesha hayo niliyokutajia yanaongezeka mwaka hadi mwaka leo unasema yanapungua, acha maneno weka muziki, ajenda kubwa kwenye uchaguzi mwaka huu ilikuwa ni rushwa, security, unemployment na hali ngumu ya maisha, insecurity Kenya inaongoza Africa kwa sasa, google uone hali ilivyo, unemployment inakaribia 48%, haijawahi kutokea tangu Kenya ipate uhuru wake, rushwa ndiyo usisema, rais mwenyewe amesalimu amri haiwezi, wewe unatuletea filimbi hapa, inflation is the highest hapa EAC, achana na Burundi na SS, acha maneno ya kienyeji wewe, Kenya kwa sasa ipo kwenye very bad shape than any time before.
Mmh! With all the smear campaigns preached on unga crisis and rampant corruption in the country, still NASA can't win? If that is the case, why Uhuru is becoming so ferocious and losing democratic direction? Since he is still in power Uhuru was expected to maintain calmness, humility and keep on waiting for the people of Kenya to decide. But now he seems to be making an attempt to divert the democratic channels forcing his way back to state house.NASA know that if ballots are counted physically even by Angels will never win elections for the coming 100 years
Gatuzi nininiKawaida ya Watanzania haswa nyie wa mlengo wa CCM mnapoijadili katiba ya Kenya huwa ni kama mumekaririshwa, yaani hayo yote umeandika hapo yameshughulkiwa pakubwa na katiba yetu mpya. Huwa mnajaribu kutumia huko kukaririshwa ili kuwaonyesha Watanzania kwamba hamna umuhimu wa wao kufuata katiba mpya. Huwa mnatumia nguvu nyingi sana.
Kwa ajili ya katiba mpya
- Maendeleo yameenea kwenye gatuzi zote hata maeneo ambayo yalikua yametelekezwa maiaka yote
- Maskini wa chini wameanza kuona haki ikitendeka
- Ukabila unapungua pakubwa maana watu walikua wameaminishwa raslimali zote zinaishia kati au Nairobi, leo hii mikoa na gatuzi zote zimepata fursa ya kutumia raslimali zao vizuri. Ni kama watu wa Mtwara waanze kuona umuhimu wa gesi.
Kuna vitu vingi sana ambavyo naweza kuandika, na kuna mada na hoja tulichangia sana humu, lakini kwa sababu upo kwa ajili ya kutafuta makosa hutaona chochote kizuri. Utatumia nguvu nyingi sana kupata wapi pa kukosoa ili uwatamaushe Watanzania wenzio wanaotamani kuwa na katiba mpya.
Hivi wewe uelewa wako ukoje?, huko shule ulienda kufuata nini?, mimi sijazungumzia wala kulinganisha na Tanzania, mimi nimezungumzia katiba ya Kenya, nikawa ninasema katiba nzuri lazima ijubu na kutafutia kero za wananchi, acha kulinganisha na Tanzania kwanza, tukimaliza hapa ndiyo tulinganishe maendeleo yanayotokea Kenya na Tanzania, ninaamini utakimbia au kurusha matusi. Mimi nilikutajia mambo saba ambayo niliyatafsiri kama shida za msingi zinazowakabili wananchi walio wengi Kenya, nikakuuliza vipi hii katiba mpya imejibu matatizo hayo?Naona unazungukia pale pale bila kupiga hatu yoyote na kunipotezea muda.
Hayo unayotaja hapo ni changamoto za kiuchumi ambazo zinakumba mataifa yote. Tanzania hapo enzi za Jakaya ilikua kwa asilimia 7.2, leo hii mumerudi nyuma hadi 6.9
Kwa kifupi ukizingatia wakati tulikua na katiba mbovu kama ya kwenu, kuna mambo mengi sana yameboreshwa
- Wakati wa katiba mbovu, uchumi wa nchi yetu ulikua kwa asilimia 3, leo hii unakua kwa zaidi ya asilimia 5
- Wakati ule Kenya ilikua inaorodheshwa kwenye nchi maskini kama Tanzania, leo hii ni uchumi wa kati
- Tulizoea vita vya kikabila, kuchomeana nyumba kila wakati wa uchaguzi, leo hii tunaona maamuzi yanafanywa na mahakama huru. Sio kama kwenu rais anatangazwa moja kwa moja bila jinsi ya kulalamika.
- Maendeleo tunaona yanafikia maeneo ya mbali ambayo yalitelekezwa
- Tunaona mawaziri wanachaguliwa kwa kuzingatia sifa, wanapitia bunge na taasisi kadhaa kabla ya kukubalika, awali ilkua kama Tanzania ambapo sifa za waziri ilmradi anajua kusoma na kuandika tu.
kama nilivyokuambia nikiamua kuandika manufaa ya katiba mpya, hapa naweza kuorodhesha zaidi ya elfu moja, lakini haitakua na umuhimu wowote maana wewe hapo ulishakaririshwa. Hivyo kwaheri....
Gatuzi ninini