Wakenya walinunua hisa za Safaricom hadi wakapitiliza, WaTz wanabembelezwa na Vodacom wanunue

And still we're greater than you. You're just a bitter Bongo lala. With all our problems we continue to prosper.
Na by the way, DSE cannot even come close to NSE.
Hapa Nairobi twanunua hisa zote bila kubagua.
sababu nyingine ni za kihistoria, toka dunia iumbwe nyie mlikuwa mabepari na mabwanyenye na makabaila. on the other side sie tulianza na ujamaa na sasa tuko half ubepari even I hv not mentioned harakati zetu za kusaidia waafrika wenzetu. mdogomdogo mbona tutawapita Pamoja na kutangulia kwenu. tuko smart hatukurupuki.
 
Si kweli 95% came from Kenyans
 
Kuna vitu viwili hapa vya kuzingatia.
1. Ununuzi wa hisa huangalia projection kama unaweza kupata faida kwa muda fulani. Sasa kuna taarifa za Vodacom kuwa na hali ya kusuasua(au tuseme hali sio nzuri) kibiashara kiasi cha kupunguza wafanyakazi. Nani anapenda kuwekeza ktk biashara yenye uelekeo wa kushuka hisa zake au kupata hasara?
2. Hali ya mzunguko wa pesa imekuwa ni changamoto kwa watu wengi kuanzia wafanyabiashara wakubwa hadi wadogo au wa kati kutokana na mabafiliko makubwa ya utekelezaji wa sera za uchumi wa awamu hii ya Mh.Magufuli. Watu wamekosa mtaji wa kununua hisa. Sekta binafsi zimeyumba na watumishi wa umma nao marurupu mengi nje ya salary yamesitishwa.
HITIMISHO: Pamoja unaweza kuwa upo sahihi kuhusu mtazamo wa watanzania lakini ni kwa kiasi kidogo sana. Miaka ya karibuni tumeona muamko mkubwa sana wa watanzania kununua hisa. Mtazamo au imani kubwa ya watanzania wengi ni kuwa makampuni ya simu yanaingiza faida kubwa sana kiasi watu wengi walitamani kuajiriwa nayo. Hivyo kwa mtazamo huo wasingeogopa kuwekeza mahali wanapohisi watatengeneza faida kubwa, sasa basi tuhitimishe kwa kuhisi tatizo kubwa watanzania wengi sasa wameyumba kiuchumi.
 
Then this IPO ni 100% for Tanzanians,by seeing 20% is allocated for foreigners i guess wananchi wakajua hii ishu ni hot cake! Ni mtazamo wangu tu.
 
ww umenunua hizo hisa unapiga domo tu....

na nataka uje na zaidi ya asilimia 20 tu za faida ya hao watu walio wekeza hisa safaricom

nimegundua nyie wakenya ni wapumbavu sana katika mnapenda mpate mali kirahisi rahisi .....
 
Tutajie gawiwo (dividend) ya Safaricom ni ksh. ngapi?
Nijipime laki mbili yangu nikiiwekeza huko italipa kuliko nikilima heka kumi za nyanya.

(najua kwenyu hamko na ardhi)
hajibu huyo maana yeye mwenyew hajawekeza kwenye hiyo hisa anayoisema na swali ulilomuuliza mpaka aka google ndyo atakujibu..
 
acha kujidanganya wew huku vodacom wateja wengi wapo vijijini huku vodacom si mtandao unaotamba kama ufikiriavyo.....vodacom haina wateja wengi kama tigo na airtel na sasa hivi kuna halotel

unapoongea uchunguze kama kwenu mtandao unaoongoza ni safaricom basi huku vodacom ni mtandao wakawaida sana una wababe wake
 
hilo nilikenya
 
@leadersofleaders huko kwao hawana choice innovation kwao ni Mpesa tu bila kuangalia the overall product that a phone company offers Tigo wanaweza mchezo. Hata Halotel ni tishio kwenye data.
Bongo unajichagulia upendacho
Leo Halotel kwenya Data hata polini full kasi
 
Sasa mkuu utanunuaje hisa hauna uhakika wa kula jioni?

Pia tuliowengi huu mfumo wa hisa hatuujui, unapataje faida, unadaije Mali zako....kwa kifupi kwa 90% ya wabongo hatujui hisa ni nn

Wangeanza kwanza kutuelewesha huenda tungeamka
 
wakenya mimi huwaga nawaitaga mataila wa dunia hawatupagi shida sababu tushawajua....
Ni watu wa ku-exxagerate mambo...hamna kampuni itakayoipa shida Halotel in the region kwenye data! So far is the fastest growing as the newest entrant na niko sure in 2 years time itakuwa na market share ya double digits i.e. over 10% considering the massive infrastructure they r constructing.
 
@lusematic huyu @leaderofleaders huko kwao hawana choice innovation kwao ni Mpesa tu bila kuangalia the overall product that a phone company offers Tigo wanaweza mchezo. Hata Halotel ni tishio kwenye data.

We have many choices. Orange na Airtel wako na much better voice and internet packages than Safaricom.
There was a time YU was offering free calls.. Literally ZERO charges all round.
Airtel money nayo ni free kutransact, ilhali Mpesa inalipisha.

Lakini bado Wakenya wamekatalia Safaricom. It's not out of lack of choices, but rather because of convinience. We've reached a stage where calling and texting is so cheap that even if the other guy offers it for free, it's not worth your time getting up to buy another sim card.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…