Wakenya wanajua kuitumia ardhi kwa manufaa zaidi kuwazidi Watanzania?

Wakenya wanajua kuitumia ardhi kwa manufaa zaidi kuwazidi Watanzania?

Siku chache zilizopita, nilimtembelea mkulima mmoja wa matunda nchini Kenya. Taswira ya shambani kwake ilinipa ujumbe kuwa ni mkulima mwenye mafanikio mazuri.

Japo hana na eneo kubwa sana, analitumia kikamilifu eneo lililopo. Sidhani kama shamba lake lote linazidi ekari tano!

Aliniambia kuwa kwa kawaida, robo ekari humwingizia shilingi milioni moja hela ya Kenya kwa mwaka

Milioni moja ya Kenya ni kama milioni kumi na sita hela ya Tanzania.

Sitilii mashaka maelezo yake, ila najiuliza kama kuna Watanzania wanaopata mafanikio kama hayo kupitia kazi za shamba.

Na kwa kuwa bado sijamsikia Mtanzania mwenye mafanikio kama hayo, nimebaki najiuliza: Wakenya wenye uhaba wa ardhi wanajua namna bora ya kutumia ardhi kwa kilimo chenye tija kuwazidi Watanzania wenye ardhi bwerere?
Siku ukitembea dunia utagundua hamna mwaafrika amefika level ya kucheka mwenzake. There is a reason tunaitwa Third world. Ukiona mashamba ya Corporations ndio utanielewa.
 
Angalia mitandao ya kijamii za Tanzania sasa hivi, watu wako busy kubishana mambo ya vita vya Russia Vs Ukraine na Israel Vs Hamas utafikiri wanaopigana huko ni waluguru na wazigua mpaka watu wanatukanana matusi ya nguoni.

Sasa ingia kwenye mitandao ya kijamii za Kenya utaona wananchi wanavyoisakama serikali kuhusu hali mbaya ya uchumi na mambo ya ufisadi na wanaona vita vinavyopiganwa nje ya Kenya haviwahusu.

Kuna kipindi hapo majuzi wakati UN ilipoiomba serikali ya Kenya kupeleka polisi kulinda amani nchini Haiti wananchi wa Kenya walienda mahakamani kupinga na kudai kwamba polisi wameshindwa kuwalinda wakenya sasa wataendaje kuwalinda wahaiti..??😛😛😛

Hili ktk Tanzania kamwe haliwezi kutokea na sana sana watamwagia mama sifa kwa jinsi UN ilivyo na imani na jeshi lake la polisi.

Comparing the mentality of Tanzanians and Kenyans is an exercise that will always be in futility as the people of the two countries have less to share in common but much to contrast in general.
 
Analima nini? Na kilimo eidha greenhouse, nimesaidia kueleźea.
Analima DRAGON FRUITS na APPLE, pia anauza mbegu/ miche ya apple na dragon fruits.

Hana green house, ila amefunga mfumo wa umwagiliaji.

Na kwa sababu eneo hilo lina asili ya jangwa, amechimba kisima kwa hiyo ana uhakika wa maji majira yote ya mwaka.
 
Hata Tanzania walioelimika ni wengi mno ila system imeshikiliwa na waswahili. Siku mfumo ukishikiliwa na mtu alienyooka mabadiliko ni ndani ya miaka michache mno.
Niliwahi kujaribu kuulizia jinsi ya kununua kahawa bongo na kuuza nje, nilichoka na hiyo milolongo iliyopo katika utaratibu wake katika ununuzi , haukuwa na tofauti kati ya mtu anayetaka kununu dhahabu bongo na kuuza nje
 
Niliwahi kujaribu kuulizia jinsi ya kununua kahawa bongo na kuuza nje, nilichoka na hiyo milolongo iliyopo katika utaratibu wake katika ununuzi , haukuwa na tofauti kati ya mtu anayetaka kununu dhahabu bongo na kuuza nje
Hiyo bureaucracy nafikiri ipo pia kwenye ununuzi wa korosho na pamba. Inafanyika hivyo kwa manufaa ya nani?
 
Mfumo, sababu serikali wangeweka senta za kuuzia km vile maziwa wanavyopeleka watu center. Wanalipwa naona kila mtu angelima na kupata pesa. Lakini aaaahh dalali akuzingue na kukuibia juuu aiseee.
Mabadiliko huanzia kwa mtu mmoja. Inawezekana wewe si mkulima lakini bado unaweza Ukafanya kitu kitakacholeta mabadiliko ya kudumu. Una mpango gani kwa ajili ya kuibadilisha hali hiyo?
 
Kenya kuwa na kiwango kikubwa cha elimu kimewasaidia sana kupunguza kuwa na tabia za kiswahili ambazo ni very common among the people of Tanzania.

Na hii kwa kiasi kikubwa ndio inasababisha Tanzania kuwa na uchumi mdogo tofauti na Kenya pamoja na kuwa na rasilimali nyingi zaidi kuishinda Kenya.
Huu ni ukweli mchungu ambao Wabongo hatutaki kuambiwa

Sent from my TECNO BF7 using JamiiForums mobile app
 
Mkenya ana masoko ya uhakika baada ya kuvuna tukianzia nchini kwao pamoja na nchi za nje. Wabongo wanategemea dalali.
Hivi ni visingizio tu ili usilime.

Moja ya kanuni za mkulima bora ni pamoja na kutokulima kwa kulenga soko. Sisemi kwamba usiuze isipokuwa, mtu anatakiwa alime kwa kupenda yaani kilimo ukipende kwanza, halafu ukishapenda ndipo utapata mazao mazuri ambayo utayauza kutokana na ubora wake.

Si kweli kwamba kila mkulima hupata soko la uhakika kila wakati. Kwa hiyo kilimo unatakiwa ukipende katika shida na raha. Vinginevyo huwezi kuwa mkulima.
 
Back
Top Bottom