John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Tatizo siyo ukubwa wa ardhi, tatizo ni ubora wa AKILI walizonazo hao watu wenye ardhi. Akili yako ikiwa mbovu, hata uwe na ardhi au rasilimali zingine nyingi au kubwa kiasi gani, bado ardhi au rasilimali hizo hazitakusaidia wala hazitakunufaisha.Siku chache zilizopita, nilimtembelea mkulima mmoja wa matunda nchini Kenya. Taswira ya shambani kwake ilinipa ujumbe kuwa ni mkulima mwenye mafanikio mazuri.
Japo hana na eneo kubwa sana, analitumia kikamilifu eneo lililopo. Sidhani kama shamba lake lote linazidi ekari tano!
Aliniambia kuwa kwa kawaida, robo ekari humwingizia shilingi milioni moja hela ya Kenya kwa mwaka
Milioni moja ya Kenya ni kama milioni kumi na sita hela ya Tanzania.
Sitilii mashaka maelezo yake, ila najiuliza kama kuna Watanzania wanaopata mafanikio kama hayo kupitia kazi za shamba.
Na kwa kuwa bado sijamsikia Mtanzania mwenye mafanikio kama hayo, nimebaki najiuliza: Wakenya wenye uhaba wa ardhi wanajua namna bora ya kutumia ardhi kwa kilimo chenye tija kuwazidi Watanzania wenye ardhi bwerere?