SSEKK The Literally
JF-Expert Member
- Sep 5, 2023
- 1,134
- 1,905
Kuna wakulima wa mpunga huko Ifakara wanapata mpaka million 70 baada ya mavuno au hyo ni pesa ndogo mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nafikiri. Yote yanapendelea mazingira ya joto.Hayo matunda yanaweza kustawi kwenye maeneo ya joto kama bagamoyo?
☑️☑️☑️Unaweza kutupa link za YouTube kwa manufaa ya wengi
Utunzaji na umuhimu wa kitu chochote una mashina mawili makubwa.Mkenya ana masoko ya uhakika baada ya kuvuna tukianzia nchini kwao pamoja na nchi za nje. Wabongo wanategemea dalali.
Hoja imeungwa mkono kwa kura zote.Utunzaji na umuhimu wa kitu chochote una mashina mawili makubwa.
1) Kwanza ni Elimu na Discipline ya Matumizi mazuri. Iwe ya Ardhi, gari, fedha, elimu, mahusiano nk. Haya yanaweza kutokana na mfumo mzuri wa elimu, au mazingira yanawasukuma kufanya matumizi sahihi halafu Matokeo yake subconsciously mnajengwa kuwa watu wenye utaratibu wa kuwa watumiaji wazuri wa vitu. Kwenye mfano wa Ardhi hapa unakutana na Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa. Ambao jiografia imewafunza kutumia Ardhi vyema kwa sababu ya scarcity especially kwenye vizazi.vilivyotangulia. hii pia imewashape wakenya... Lakini zaidi ni post colonial land laws and policies ambazo zimeendelea kujifanya.ardhi kuwa haba zaidi Matokeo yake imekuwa ya thamani.. tofauti na kwetu hapa kuipata bure bure na mifumo kushindwa kulinda Milki ukijumlisha na sera yetu ya kukodi Ardhi yetu inakosa kuwa ya thamani sana hivyo kushindwa kuvutia uwekezaji mkubwa kwa ngazi zote za kipato.
2) Ili kitu kiwe muhimu pia lazima kiwe na uwezo wa kuwa na faida au kutatua changamoto mbali mbali kwa mmiliki wake. Hapa tukozumzia Ardhi Kenya wamefanikiwa sana kuwasaidia watumiaji wa Ardhi katika nyaja zote ikiwemo kilimo, ufugaji, madini, na ujenzi kujipatia kipato kikubwa. Hiyo inamvutia kila mtu anayepata nafasi japo haba ya kupata rasilimali Ardhi kuiwekea mipango kabambe inayosaidiwa na.mifumo.mozuro ya kisheria na kiuchumi kufikia.malengo. tofauti na hapa kwetu wakulima matajiri ni wachache sana..na matajiri wakulima wa kizazi.mpaka kizazi ni kama hakuna kabisa.
Tunahitaji kuyazungumza haya kwa upana sana.
Wakenya wanalangua matunda na mbogamboga wanapeleka kwao kufanya package na kuuza nje ,mkuu kuuza mboga na matunda nje ya nchi sio kwamba unaamka tu na unajiamlia kuna utaratibu maalumu na makubaliano ambayo serikali ya nchi husika lazima ifanye na nchi unayoenda kuuza hizo bidhaa .
Sisi balozi zetu zimelala hazifungui masoko na kuingia mikataba ya kibiashara ya kumnufaisha mkulima directly ,sasa hilo ni tatizo .
Huwezi leo hii ukasema umelima zako Matango ,tikiti , spinach organic fresh kwenye greenhouses zako halafu unataka ukayauze UK bila pre agreement na vibali maalumu , haipo hiyo .Bidhaa yako yenye package na mambo ya Tanzania toka Tanzania haiwezi ingia UK bila makubaliano ya Tanzania na UK na vibali maalumu vya ukaguzi kuhusiana na hiyo bidhaa unayopelekea .
Hii haifanywi na raia ,ni kazi ya serikali kufungua hizi fursa
sawa mkuu ila kamaa alivyo comment EXTROVET uwe na passion ya shamba mi ni mkulima mdogo ninaepanukaPole sana mkuu. Ugua pole.
Mimi nayamudu mazingira yote:
1. Kukaa kwenye hoteli ya nyota tano
2. Kulala shambani kwenye banda la majani ambalo mlango wako ni kipande cha gunia
3. Kutumia usafiri wa ndege
4. Kutembea kwa miguu kwa masaa mengi bila kupumzika, hata zaidi ya masaa kumi, ikibidi.
5. Kuvaa kinadhifu
6. Kuvaa ",kishamba", ikibidi, na kutembea peku
7. Kulima muda mrefu kwa jembe la mkono, muhimu tu nisiwe na njaa. Naweza nikakaa shambani Asubuhi hadi Usiku
Kwa kifupi, ninayaweza mambo yote...
Pole sana mkuu. Ugua pole.
Mimi nayamudu mazingira yote:
1. Kukaa kwenye hoteli ya nyota tano
2. Kulala shambani kwenye banda la majani ambalo mlango wako ni kipande cha gunia
3. Kutumia usafiri wa ndege
4. Kutembea kwa miguu kwa masaa mengi bila kupumzika, hata zaidi ya masaa kumi, ikibidi.
5. Kuvaa kinadhifu
6. Kuvaa ",kishamba", ikibidi, na kutembea peku
7. Kulima muda mrefu kwa jembe la mkono, muhimu tu nisiwe na njaa. Naweza nikakaa shambani Asubuhi hadi Usiku
Kwa kifupi, ninayaweza mambo yote...
Sawa sasa hivi angalau tunaweza kusema tuna wasomi lakini utakubaliana na mimi kwamba wengi wa wasomi wa kitanzania utawajua tu kwani wengi wao ni watu wanafiki na hawawezi kujenga hoja na kuitetea ni watu wasiojiamini kabisa tofauti na wasomi wa Kenya.Sema wametangulia kuwa na exposure,kwani huku huku hakuba wasomi?
Si vibaya ukashare nasi huo mfumo unakuwa si rafiki katika hatua ipi ya mnyororo wa thamani?Mimi nimezaliwa Kagera ,nakupa uhalisia huo sasa , kama wewe hauamini ,its up to you kufanya uchunguzi wako binafsi na kujiridhisha nilichokwambia .
Mfumo sio rafiki kabisa nchi hii kwa mkulima
Watuwekea limiti ili wao viongozi wao wapush hayo madel imagine kwenye open market wewe na waziri mna compete sehemu moja ya biashara,.kwaiyo lazima waziri atumie uwazir wake kuku push down ili yeye ndio hiyo deal aipate, kuna miradi mingi bongo huwa behind the scenes ni viongozi na ndio hao hao wanotunga sheria za wake wenza kulipwa mafaoHiyo bureaucracy nafikiri ipo pia kwenye ununuzi wa korosho na pamba. Inafanyika hivyo kwa manufaa ya nani?
Nimekusoma mkuu🙏sawa mkuu ila kamaa alivyo comment EXTROVET uwe na passion ya shamba mi ni mkulima mdogo ninaepanuka
sawa mkuu ila kama alivyo comment EXTROVET uwe na passion ya shamba mi ni mkulima mdogo ninaepanuka shamba kadiri ya muda napenda pilipili mbuzi , papai na pesheni soko ni DAR, hakuna cha ajbu mpaka upoteze muda kuja huko na pia mtibabu yana nisumbua ccbrt
mazao yangu hayo nni kwamba ukipanda utavuna kupata hela mara kadhaa bila kupanda tena yaani unachuma unauza na shambni unasubiri tena yaive , natumia umwagiliaji wa matone kwenye pilipili.. Hivyo nimepata shamba ambalo linakubali mazao hayo matatu na mahindi alizeti na ufuta. na nyanya bamia na mbogo mboga zote na matunda., mazao yanayokaribiana pH, sina maarifa kwenye mahindi n mpunga sabbu mimi sipendi mazoo ya kuvuna halafu unapanda tena
kinachonisiadia ni kuwa na maji wakati wote na kumwagiiia eneo kubwa kwa urahisi, hivyo hakuna cha ajabu kama nivyosema mimi ni mkulima mdogo ninaechipukia. Ila ukianza kulima aa kuvuna mtandao wko unakuwa.
mkuu sio kiwango cha elimu,usiwe mfata mkumbo.Kenya kuwa na kiwango kikubwa cha elimu kimewasaidia sana kupunguza kuwa na tabia za kiswahili ambazo ni very common among the people of Tanzania.
Na hii kwa kiasi kikubwa ndio inasababisha Tanzania kuwa na uchumi mdogo tofauti na Kenya pamoja na kuwa na rasilimali nyingi zaidi kuishinda Kenya.
hakuna exposure kama hakutakuwa na mtu anayefanya mnamuona kwa macho.Nini kifanyike ili wakulima wa Kitanzania nao wapate exposure kama wenzao wa Kenya?
na kwa sasa 2023 dunia iko kwenye mfumo tofauti sana.Kilimo kulipa ni masoko, mchawi yuko hapo. Kama utalima kwa million 20 halafu upate soko kwa million 15 huoni kama balaa ni zito. Asilimia 80% ya wabongo tunalima ila hatujui tutamuuzia nani at the end.
😀Nimekuelewa, kina msoga au sio?! Maana naye amekuwa king/queen maker.
Nazani walofuatana wote huenda anahusika including wa sasa top?!
sio elimu ndogo tu Bali mtaala mbovu usiomtengeneza mhitimu kuyamudu mazingira yake,yaani elimu isiyotoa maarifa tambuzi(self awareness/consciousness)Nakumbuka wakati tunasoma shule za msingi kwenye miaka ya sabini, wakati Tanzania ilikua na shule za sekondari chini ya mia mbili nchi nzima Kenya walikuwa na sekondari zaidi ya 600 nchi nzima wakati tukiwa na idadi ya watu kwenye milioni 12 huku Kenya wakiwa na watu milioni 8 hivi.
Elimu ndogo miongoni mwa watanzania wengi imechangia sana kwa jamii ya watanzania kuwa subjective society badala ya objective society tofauti na Kenya na hii hali ndio imewapa ccm unafuu wa kuitawala nchi hii kwa muda mrefu zaidisio
Nini kifanyike mkuu?Wakulima wakenya ni madoni huko Bei za mazao zimechangamka Sanaa, na Wana uhakika wa masoko, huku Bongo anayefaidika ni dalali, mkulima lake ni jua na mvua
🙏hakuna exposure kama hakutakuwa na mtu anayefanya mnamuona kwa macho.
kenya inaongoza kwa kilimo cha maua,unadhani waliamka wameshiba wakaamua kuanza kulima maua na kuuza nje!!!
ni wazungu walioingia kenya na kuanza biashara hiyo,wazawa nao wakaingia ktk field baada ya kuona kumbe inafanywa hivi.