Swala la permit Raisi Magufuli hatakiwi kukubali, mimi nilipata nafasi ya kufanya kazi Kenya zaidi ya miaka mitano, Kenya wanasema wanatoa kibali cha kufanya kazi ( work permit) kwa wananchi wa jumuia ya afrika mashariki kumbe sio, ukiwa katika kampuni yeyote Kenya utapewa documents zote za ku apply work permit, baade utazipeleka uhamiaji pale nyayo ,kinachofanyika maafisa wa uhamiaji watapokea zile documents zako na kuzitunza au kuzitupa kabisa, utakaa unasubiri work permit hata miaka miwili hautapata permit, hii ilinitokea mimi kwa kujifanya kuwa ni member of east Africa, nilisubmit documents zangu zikaa zaidi ya mwaka mmoja bila kupata permit, ndipo nikaulizia dada mmoja ambae ana deal na visa/permits katika kampuni niliokuwa nafanya kazi akaniambia ndugu ( Kenya wanatumia sana hili neno wanapoongea na wtz) bila pesa hutapata permit hata kama wew umetoka katika jumuia hii ya afrika mashariki, akaniambia permit Kenya kuna watu /staff wa immigration wanao control the whole process na wanakampuni zao nje ( Agents) bila kupitia kwao huwezi pata permit, na hao huamua nani apate permit nani asipate hivyo ikawa imekula kwangu.
Niliendelea kuongea nae huyo mdada akaniambia andaa 90k Kenyan shillings equivalent to mil 1na laki 8 ya tz ,ujaze form then nipatie documents zako nikusaidie kupata permit, nikamuuliza hiyo 90k ya nini akaniambia hii napatiana agent na watu wa immigration uweze kupata then nitakupatia receipt uweze to claim back ur money to the company, ila akaniambia kabisa katika 90k hii, 10k inakwenda kwa government iliyobaki ni mlungula kwa agent na wahusika wakuu ndani. Kweli nilifanya vile na nikakaa ndani ya miezi miwili au mitatu nikapata permit ya miaka miwili. Kwa hiyo nilikuwa nafanya hivyo pindi nikiwa Kenya kwa zaidi ya miaka sita kwa interval ya two yrs two yrs, wengine wtz ambao hawakuwa na 90k hadi leo sijui kama waliweza kupata permit Kenya, hiyo kampuni tulikuwepo wtz lakini ni mimi pekee ndo nilipata permit kwa njia ya kutoa pesa wenzangu waliotegemea free permit kwa watu wa EAC walisota miaka yote bila kupata permit, hivyo uhuru kama anataka kuleta usawa na anapigania sana permit kwa wananchi wake Tanzania basi kwanza aende pale Kenya immigration awaambie maafisa wake mchezo wanaoucheza kwa wananchi wa EAC, aweke dawati/help desk kwa ajiri ya wananchi wa EAC kupata huduma za business visa/work permit bila kupitia kwa agents na bila kulipa 90k,akifanikiwa hili basi ahamasishe viongozi wa EAC kufuta permit katika nchi husika.
Business visa, ukienda Kenya kufanya kazi ndani ya miezi mitatu hadi sita kabla hujapata permit kuna utapewa kibali cha muda cha kufanya kazi ( business visa) ,hii business visa bila kujali wew umetoka EAC unalipa 5K Ksh, na unapewa miezi mitau, ikiisha unapewa tena business visa ya miezi mitatu kwa kulipa tena 5K ksh, ikifika miezi mitatu hupati unaambiwa apply for permit, hapo ndo shida inaanza, hivyo utaona kuwa Kenyan permit ni ngumu sana kupata kuliko nchi yeyote wanachama wa EAC, kama kuna mtanzania yeyote au mganda au Rwandese amepata permit Kenya bila pesa aseme hapa, sio swala la mchezo kupata permit Kenya , kwa hiyo magufuli awaambie kabisa wao wabadilike, na watoe permit bure kwanza ndani ya miaka mitatu kwa wananchi wa EAC then baadae nchi zingine zifuate, au la sivyo tuendelee hivi hivi kwa Wtz na nchi nyingine kulipa 90k na wao waendelee kulipa gharama za permit nchini tz au kwingineko, wahusika wa magufuli mfikishieni mheshimiwa hii taarifa.