Tetesi: Wakenya wanataka waruhusiwe kufanya kazi Tanzania bila Vibali, rais asikubali

We hakuna unachojua Mfatilie trump analalamikia nini kuhusu Mexico

Ule ukuta alioaidi trump kuujenga mpakani mwa Mexico ili wasiingie ni wakina nani na ni kwa nini?

Na ni RAIA kutoka nchi gani ......

Tatizo ufatilii mambo.........
Inawezekana unafuatilia mambo lakini hauelewi, watu wengi wanaotoka Mexico ni illegal migrants (HAWANA VIBALI) na wamejaa Texas kwa kupitia njia za panya na kilaza Trump anadhani ukuta utawazuia.

Na sioni akikubali hilo ombi.
 
Fatilia mkuu acha kuwa mvivu....

Wa Mexico wanaishije USA?
Unafatilia mijadala ya Trump kweli wewe,,,,anasema wageni ndo wanaziba nafasi za wazawa kwenye ajira kwaiyo atalikomesha hilo swala akiingia madarakani ndo ujue hata marekani wanateseka na kuajiri raia wageni nchini mwao
 
Mim sioni kama ni tatzo as long as na wao wataruhusu na sisi tuende kufanya kaz huko bila kibali
Kupata kazi kule sahau kaka...wao wenyewe wanapeana kikabila utakuta ofisi flani imejaa kina kimanthi na Wangai...ofisi nyingine wamejaa kina onyango na odhiambo...hatari sana kule kaka...
 
Swala la permit Raisi Magufuli hatakiwi kukubali, mimi nilipata nafasi ya kufanya kazi Kenya zaidi ya miaka mitano, Kenya wanasema wanatoa kibali cha kufanya kazi ( work permit) kwa wananchi wa jumuia ya afrika mashariki kumbe sio, ukiwa katika kampuni yeyote Kenya utapewa documents zote za ku apply work permit, baade utazipeleka uhamiaji pale nyayo ,kinachofanyika maafisa wa uhamiaji watapokea zile documents zako na kuzitunza au kuzitupa kabisa, utakaa unasubiri work permit hata miaka miwili hautapata permit, hii ilinitokea mimi kwa kujifanya kuwa ni member of east Africa, nilisubmit documents zangu zikaa zaidi ya mwaka mmoja bila kupata permit, ndipo nikaulizia dada mmoja ambae ana deal na visa/permits katika kampuni niliokuwa nafanya kazi akaniambia ndugu ( Kenya wanatumia sana hili neno wanapoongea na wtz) bila pesa hutapata permit hata kama wew umetoka katika jumuia hii ya afrika mashariki, akaniambia permit Kenya kuna watu /staff wa immigration wanao control the whole process na wanakampuni zao nje ( Agents) bila kupitia kwao huwezi pata permit, na hao huamua nani apate permit nani asipate hivyo ikawa imekula kwangu.

Niliendelea kuongea nae huyo mdada akaniambia andaa 90k Kenyan shillings equivalent to mil 1na laki 8 ya tz ,ujaze form then nipatie documents zako nikusaidie kupata permit, nikamuuliza hiyo 90k ya nini akaniambia hii napatiana agent na watu wa immigration uweze kupata then nitakupatia receipt uweze to claim back ur money to the company, ila akaniambia kabisa katika 90k hii, 10k inakwenda kwa government iliyobaki ni mlungula kwa agent na wahusika wakuu ndani. Kweli nilifanya vile na nikakaa ndani ya miezi miwili au mitatu nikapata permit ya miaka miwili. Kwa hiyo nilikuwa nafanya hivyo pindi nikiwa Kenya kwa zaidi ya miaka sita kwa interval ya two yrs two yrs, wengine wtz ambao hawakuwa na 90k hadi leo sijui kama waliweza kupata permit Kenya, hiyo kampuni tulikuwepo wtz lakini ni mimi pekee ndo nilipata permit kwa njia ya kutoa pesa wenzangu waliotegemea free permit kwa watu wa EAC walisota miaka yote bila kupata permit, hivyo uhuru kama anataka kuleta usawa na anapigania sana permit kwa wananchi wake Tanzania basi kwanza aende pale Kenya immigration awaambie maafisa wake mchezo wanaoucheza kwa wananchi wa EAC, aweke dawati/help desk kwa ajiri ya wananchi wa EAC kupata huduma za business visa/work permit bila kupitia kwa agents na bila kulipa 90k,akifanikiwa hili basi ahamasishe viongozi wa EAC kufuta permit katika nchi husika.

Business visa, ukienda Kenya kufanya kazi ndani ya miezi mitatu hadi sita kabla hujapata permit kuna utapewa kibali cha muda cha kufanya kazi ( business visa) ,hii business visa bila kujali wew umetoka EAC unalipa 5K Ksh, na unapewa miezi mitau, ikiisha unapewa tena business visa ya miezi mitatu kwa kulipa tena 5K ksh, ikifika miezi mitatu hupati unaambiwa apply for permit, hapo ndo shida inaanza, hivyo utaona kuwa Kenyan permit ni ngumu sana kupata kuliko nchi yeyote wanachama wa EAC, kama kuna mtanzania yeyote au mganda au Rwandese amepata permit Kenya bila pesa aseme hapa, sio swala la mchezo kupata permit Kenya , kwa hiyo magufuli awaambie kabisa wao wabadilike, na watoe permit bure kwanza ndani ya miaka mitatu kwa wananchi wa EAC then baadae nchi zingine zifuate, au la sivyo tuendelee hivi hivi kwa Wtz na nchi nyingine kulipa 90k na wao waendelee kulipa gharama za permit nchini tz au kwingineko, wahusika wa magufuli mfikishieni mheshimiwa hii taarifa.
 
host, President Uhuru Kenyatta, is also expected to lobby for a clear stand on work permits for Kenyans living and working in Tanzania.
Soma hizo quote uone kilichoandikwa, inaonekana hukumuelewa mleta mada.
Ambassador Mohamed was set to address a news conference to formally announce her bid on Friday, but postponed it to a later date.

President Magufuli, will be in the country for a two day State Visit, that will see him affirm his country’s position on the candidature of Foreign Secretary, Ambassador Amina Mohamed for the African Union Commission Chair.
 
Protectionism ni moja ya falsafa inayotumika na mataifa makubwa pia kabla hujaandika upuuzi wako kaa chini na uje na arguement ilioenda shule..otherwise acha kudhihirisha upeo wako mdogo(low IQ)
Ficha upumbavu wako", K*** wewe. Mlaumu mzazi wako kwa kushindwa kukusomesha, na sio kutuonesha upumbavu wako hapa. Tunawataka wakenya tupambane nao on employment & development.
 
Tufikirieni sawa kama mnasema waje powa tu ila background zao zitolewe isije ikawa kama UK waliingia eeu ilikuwa tabu ma killers kibao wakaingia hakuna background sasa wamejuta Blair kuwafungulia geti. Mimi sijali msinielewe vibaya ila wachekiwe.mmm nimesahau africa hongo kwa kwenda mbele wataingia tu haa
 
Kupata kazi kule sahau kaka...wao wenyewe wanapeana kikabila utakuta ofisi flani imejaa kina kimanthi na Wangai...ofisi nyingine wamejaa kina onyango na odhiambo...hatari sana kule kaka...
Mwenzangu niliishigi Kenya balaaa.miaka mingi iliyopita ..tribalism kule noma.ukiingia ofisi hii ni wakamba ile nyingine wakikuyu
 
Mkuu nakuambia kama kuna watu wana Roho mbaya East Africa basi ni KENYA. Mwaka juzi niliajiriwa na NGO flan duty station NAIROBI. Ngoma ikaanza niliporipoti pale,

Yaani niliambiwa na country manager kuwa inabidi ashughulikie work permit kwanza, sasa kimbembe, ili upewe permit ni lazima kazi hiyo iwe imetangazwa Kenya na wamekosa mtu mtu huko, ikaonekana mambo hayaeleweki.

Nimekaa miezi mitatu sioni kinachoendelea ikabidi niwasiliane tena na NGO President SWEEDEN, alipowapigia pale wakasema nimekosa work permit, baada ya mwezi uliofuata nikawa sina jinsi nikabeba begi langu kurudi Bongo land.

KENYANS ARE FOOLS KWAKWELI
 
Sioni kama kuna ubaya ikiwa watafanya kazi kwa vibali, mbona utaratibu wa aina hiyo unafuatwa na nchi nyingi, wa wageni kufanya kazi kwa vibali, ni nafasi nzuri ya sisi kujifunza toka kwao na wao toka kwetu.
 
Bro lugha uliyotumia si ya kistarabu, umejieleza vizuri, ila ilikuwa haina haja ku generalise kuandika mwisho " KENYANS ARE FOOLS" nimeona aibu hata kurudia ulichoandika.
 
Bro lugha uliyotumia si ya kistarabu, umejieleza vizuri, ila ilikuwa haina haja kuandika mwisho " KENYANS ARE FOOLS" nimeona aibu hata kurudia ulichoandika.
Hujui shida nilizopata mkuu, nadhani unyamaze tu. Nakuhakikishia huwa nikiona mkenya natamani kumkata panga.

Waone hivi hivi, wakenya siyo watu kama unavyodhani.
 
Hapo kwenye maamuzi ya papo kwa papo ndipo kwenye utata.

All in all sioni ubaya wa Wakenya kuja kupiga kazi humu ndani kama wanafuata sheria.

ni kweli waje, ila work permit lazima walipie na walipe kodi mapato yao angalau kwa 30%, wezetu ulaya wagen wanalipa kodi kubwa zaid.
 

unania zuri, ila acha woga, waache waje wafanye kazi ila walipie work permit na walipe kodi mapato yao. tena kodi iwe juu zaid kwa wageni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…