DECEPTION GAME PLAN YA CHADEMA SO FAR ,"INAWORK"OUT???
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 9,2023.
Wakati maridhiano kati ya Chama changu cha Mapinduzi na Chadema yanaendelea,mwanzoni mwa mwaka huu,2023,nilionya Chama changu kuwa makini na Chadema kwani hawakuwa na nia njema katika kutekeleza maridhiano yale dhidi ya Chama cha Mapinduzi.
Miezi minne mitano mbele,Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe mmoja ya washiriki "kinara"kwenye maridhiano yale ndio akawa mtu wa kwanza "kuyavunja" kwa mdomo wake mwenyewe kwa kusema hivi".....Rais Samia na Wazanzibar wenzake wanauza Tanganyika...."Mh Mbowe alinukuliwa akiwa barani Ulaya.
Mh Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti wa Chadema kwa sasa ndio anaongoza "genge" la matusi dhidi ya Mh Rais kwa kutamka hadharani kwamba "..Rais Samia ni Rais wa ajabu kuwahi kutokea kwenye Taifa hili,...hivi huyu Mama kapatwa na nini..."
So far "Deception Game Plan" ya Chadema dhidi ya "Nia Njema"ya CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kama tayari imeshakuwa "sucessfully executed".Niliwahi kuonya kwamba Chama changu kilikuwa kinaingizwa kwenye mtego mkali ndani ya eneo la adui Chadema kwa ajili ya Siasa za mwaka 2024 na 2025.
Kosa la.kwanza kubwa ambalo tulilifanya ni kukosa nafasi ya "kuingia kwenye akili" ya Chadema na kujua wanawaza nini kuhusu Siasa za mbele dhidi ya nia njema ya CCM na Rais wake.That was the first mistake we commited,strategists wa CCM hatukuweza kufanya "recce" ya kutosha katika executuon ya mpango ule.
Deception ni nini?kwa lugha rahisi deception ni uwezo wa upande mmoja(vikosi) kumdanganya adui(vikosi vingine)katika uwanja wa medani kwa lengo la kumuwin adui yako na kuweza kummaliza kirahisi.Moja ya njia kuu ya kutekeleza mpango wa deception ni pamoja na (I)kumfanya adui hakuone dhaifu kwa vikosi vyako kufanya mambo ya kawaida kawaida hivyo kuweza (ii)kumuaminisha na kumfanya adui yako awe "at easy".
Deception utekelezwa katika hatua kadha na moja wapo ni(I) kwa kumficha adui yako mipango yako yote ya siri(secrecy & security)ya kivita na pili (ii) ni kwa kuhakikisha unajua kila hatua ambayo adui yako.anafanya hivyo kuweza kuandaa kitu kinaitwa(Maneuver Plan)dhidi ya miapngo yake.The next and most important aspect ya deception ni (iii) attacking the enemy by suprise.
Ni wazi kuwa Chadema walikuwa anangojea muda sahihi na opportunity sahihi kwa ajili ya "kumsuprise"adui yao CCM na kweli kwa sasa wanashambulia kila kona dhaifu ya adui wao.Mpango huo wa Chadema kupitia Social.Media ambao umebatizwa jina la "Keep Placing the Botton..".unaonekana umeanza kutufanya CCM tusiwe confortable sana.
Tactics kubwa ambayo inatumiwa na Chademe ni ile ya "disinformation & misinformation " dhidi ya Mkataba wa Uwekezaji wa Bandari na DP Wprld ya Dubai.Bahati mbaya sana Counter- Strategy ya CCM yangu imekuwa dhaifu sana kuanzia Serikali na hata ndani ya Chama changu,sababu ya udhaifu huu sijui ni kwa nini.
Chadema pia wanacheza na principle nyingine ya War Execution ni ile ya Concetration of Force kwa maana ya kumpiga adui yako kwa silaha zote na kwa nguvu zako.zote pale unapoingia kwenye "target" yako.This time planners/strategist wa CDM wamekuwa accurate sana katika mpango huu.Ajenda ya Uwekezaji wa Bandari imeongezewa na mbinu ya kuwajaza "upepo"Watanganyika dhidi ya wenzao wa Zanzibar kitu ambacho hawakuwa na wasingeweza kukitamka waziwazi wakati wa Komandant John Pombe Magufuli.Thubutu.
Ajenda hizi kuu tatu zinahitaji ufundi wa viwango vya juu kuweza kuzipindua(Uwekezaji wa DP World,Udini na ajenda ya Muungano )na Chama changu cha Mapinduzi kinahitaji kuleta watu wapya kwa sasa ndani ya uwanja wa medani wa kuweza kucheza na Siasa hizi hatarishi kwa Usalama Taifa langu la Tanzania.
NINI CCM TUFANYE HARAKA HARAKA WA SASA ANGALAU KUWEZA KUWAPUNGUZA SPIDI HAWA JAMAA?
I.Tactical withdraw kwa sasa ni muhimu sana kwetu kwani kuendelea kuwajibu bila kufanya "Political Appreciation "itakuwa ni kuendelea kujiingiza kwenye "King" hivyo kuendelea kupoteza ushawishi wetu mkubwa kwa wananchi wetu.Zoezi la tactical withdraw lisizidi wiki.mbili.tatu kabla ya kuja upya kwenye uwanja medani.
II.Hatua ya pili ni kufanya tactical "re-organization & re-recruitment" kwa.maana lazima tuwasake vijana wa CCM walio.nje wenye uwezo wa kucheza na Vijana wa Chadema iwe Majukwani na Mitandaoni na kwenye main Stream Media haraka sana.Vijana hao tunao wengi tu na huu sio wakati wa utengano tena bali huu ni wakati wa kufuta tifauti zetu ndani yetu kwa ajili ya Maslahi mapana ya kuendelea kushika Dola.
Vijana hao tunawajua na wapo available muda wowote kwa maslahi mapana ya Chama.
III.Serikali yangu ya awamu ya Sita ifahamu kwamba hauwezi kufanya Siasa na wakina Tundu Lissu na Vijana wao wakina Mdude, Martin ,Mwaipaja na wengine wengi bila angalau kupractice "The Culture of Supression & Intimidation".Nadhani Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni kashaona hilo,lazima.sheria ziwe execited bila.kuangalia.sura kama kweli tunataka kulinda Usalama.Taifa pamoja na Muungano wetu.
Nadhani imetosha kwa leo.
+255746726484.
Sent from my Infinix X6511B using
JamiiForums mobile app