Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Nani hajui kwamba Uwakili wa Poti Mwabukusi ni "cover "tu lakini yeye aliwahi kugombea ubunge pale Rungwe kwa tiketi ya Chama fulani cha Upinzani,suala la Bandari ni "siasa "ya Kumbomoa Samia Suluhu Hassan tu,hakuna umaslahi ya Tanganyika wala Zanzibar.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Jibu hoja zake, usilete porojo hapa, yeye kugombea ubunge kupitia chama chochote cha siasa ni haki yake, hajavunja sheria yoyote ya nchi, kama nyie mlivyozivunja sheria nyingi mkiwapa waarabu bandari zetu zote milele wazisimamie, kama vile mmetuona sisi na vizazi vijavyo ni manyani, hamna adabu kabisa nyie.
 
wewe inaonekana hata ukitishiwa na manati tayari unakumbatia ukuta na kusomwa jicho ki urahiiisi kabisa madai yako usije tolewa nundu na jiwe la manati. Mambo yenu ya ki bwabwa pelekeni huko kwa wajomba zenu wanaotaka kubeba bandar yetu
sawa . ila mda ni mwalimu mzuri. mtakuja humu kulialia kuhusu huyo jamaa yenu. hii nchi chezea vyote usichezee misingi yake. yaani mjinga mmoja tu alete taharuki za kijinga who is he? hata huko ulaya mnaposema kuna democrasia kuna kipindi lazima wa eliminate wanaotaka kuvunja misingi ya taifa.
 
Alikuwepo ila kapokea malipo unadhani hizi kelele anapiga sababu mzalendo sana? pesa bwana hakuna asiyejuwa anafanya kazi aliyolipwa kama mzalendo ndio leo? siku za watu wenye roho wasiokuwa na uhuruma walikuwa wapi? Mama Samia huu upole utamponza nchi haiendi hivyo JPM alijuwa kuwanyosha hawa.

Wewe unadhani Boni ni Dalali kama Kitenge?

Then alivyowanyoosha ikaishia wapi? Wapiganaji hawafi bali wana-mutliply strength in numbers!
 
Watanganyika wapo na ardhi ya Tanganyika bado ipo. Hata hivyo ulipaswa kushambulia hoja na si mtu. Tatizo lenu watetezi wa mkataba hamna hoja zaidi ya vitisho na matusi! Watanganyika wameamka.
kame wameamka ingia barabarani sasa
 
viva mwambukusi, viva tanganyika
Ali Karume kasema Hussein Mwinyi mtanganyika anauza mali ya Zanzibar. Kwa habari za mitandao wanasema yupo chini ya ulinzi Msasani
Mambo yao ya Zanzibar wamalizane huko hoko hatutaki upumbuvu huku Tanganyika tunazidai Bandari zetu. Kwa nini aletwe Tanganyika wakati wanaserikali yao huko Zanzibar? Iwe mvua iwe jua hizo Bandari wanazo piga mnada kwa mahawala zao watazinyaa.
 
Wakili Mwabukusi hapo amezidisha ukali wa maneno na matamshi yake, tena sana. Mpaka roho imenistuka dah!!!

Hata viongozi wa vyama vya upinzani kina Tundu Lissu, Freeman Mbowe, Zitto Zuberi Kabwe, Yuda Iskarioti (Prof Lipumba) hawajawahi kutoa matamshi makali kiasi hicho!

Sisi wengine kila kukicha tunaitoa kasoro Serikali, Mawaziri na CCM kwa maamuzi wanayofanya, tokea enzi za mwendazake. Kila siku tunavurugana nao mitandaoni... Ila hatujawahi kuthubutu kufikia kutoa maneno makali na yenye ukakasi kiasi hicho!

Mungu iongoze Tanzania, Mungu Ilinde Tanzania. #TanzaGiza!
Ukishindwa kusikilizwa kwa lugha ya staha tumia sauti wanayoitaka wao.
 
sawa . ila mda ni mwalimu mzuri. mtakuja humu kulialia kuhusu huyo jamaa yenu. hii nchi chezea vyote usichezee misingi yake. yaani mjinga mmoja tu alete taharuki za kijinga who is he? hata huko ulaya mnaposema kuna democrasia kuna kipindi lazima wa eliminate wanaotaka kuvunja misingi ya taifa.
Misingi ya nchi Tanganyika kuuzwa na wazanzabar?
 
huyo mbwa kuna kitu kinamwasha siku si nyingi atapata anachokitafuta. Ameshindwa kupata umaarufu huko mahakamani kwasababu ni kilaza. Amekula pesa za mafisadi wanaofikiri wanaweza kuikwamisha serikali hii, atakwama yeye ngedere. Lengo la hao mambwa ni kuikwamisha serikali na wanatumika na mafisadi wa bandari. Mnafiki mkubwa eti Tanganyika yetu, anaijua Tanganyika huyo fala? Hii nchi haigawanyiki watagawanyika wao.

Dada acha hasira, mrembo andika kwa kutulia
 
WAKILI BONIFACE MWABUKUSI;KAMA HAMTATUSIKILIZA,TUTAZUNGUMZA LUGHA MTAKAYOTUSIKILIZA,HATUTARUHUSU MZANZIBARI KUFANYA MAMBO YA HOVYO KWENYE MALI ZA TANGANYIKA.

"Wazee wangu wa Mbeya nipo hapa kuwahakikishia Tanganyika hailiwi tena,tutafuatilia hatua kwa hatua kwenye mikataba ya Mali zote za Tanganyika" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba unatakiwa ujisimamie na ujitetee,ila watu wanautetea bila "baseline" za data na facts kwenye mkataba huo,hakuna research wala data, mkataba hauna data ambazo ni measured kisayansi watu wanacheza na maneno tu ambayo hayapo kwenye mkataba" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba wa bandari ni batili, chochote kilichofanywa nje ya sheria na nje ya katiba kirekebishwe" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar,hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Tanganyika,kama ambavyo Mtanganyika hawezi kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Ndoa ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ndoa ya utotoni sasa tumekua tunataka tuongee tukubaliane Mali za Tanganyika ziwe chini ya Mtanganyika na Mali za Zanzibar ziwe chini ya Mzanzibari" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu alitudanganya kuhusu kifo cha Hayati Rais John Pombe Magufuli na hajawahi kuomba radhi,na leo anatudanganya kuhusu mkataba wa bandari,akae pembeni kumsaidia Rais" Wakili Boniface Mwabukusi

"Waziri Mkuu atujibu,sheria sura 449 na sheria sura 450 kuhusu Ulinzi wa rasilimali za nchi na kuhusu ushughulikiwaji wa vifungu vyenye utata walizifuata,je vipengele vya mkataba wa bandari vinaoana na vipengele hivi vya sheria yetu" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu atujibu,kwa nini bunge linataka kubadili sheria sasa hivi ziendane na mkataba huu wa bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tuliibinafsisha Tanesco kwa Net Solution tulipata faida gani na leo Tanesco ya nani? Tulileta watu TRL wakaishia kubeba vichwa vya treni kurudi navyo India,tulifanya hivyo hivyo kwa NBC kuuzwa bei ya kutupwa,na leo mnatuambia mna muujiza kwenye kuibinafsisha bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Kama mkataba ni sahihi,Waziri Mkuu anatuambiaje tukusanye maoni,nani anakusanya maoni,yaende wapi,ya nini? kama mkataba tayari umeshapita" Wakili Boniface Mwabukusi

"Wakati nchi yetu ina Kiongozi mwenye element za Uzalendo watu fulani hawakuonekana kabisa,sasa hivi wamerudi wanatukana hadi Mahakama, Watanzania angalieni walioko nyuma ya huu mkataba"Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kila uovu juu ya Tanganyika tutaukabili kwa jina lake na kila muovu tutamkabili kwa jinsi anavyokuja,hii ni nchi yetu hatutamuchia mtu mwingine aitetee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mabadiliko ya sheria yanayokwenda kufanyika ni matusi kwa Tanganyika,narudia tena Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tunatoa onyo kwa Kiongozi mwingine kudhani anaweza kuingia mikataba ya kuuza nchi akabaki salama,wasituchezee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tunawaomba Watanzania wa dini zote,Waislamu, Wakristo,Wachungaji na Mashehe na WA jadi,tufunge tarehe 14,15,16 kuomba mapenzi ya Mungu yakafanyike kwa Tanganyika na Tanzania,ahsanteni sana"Wakili Boniface Mwabukusi
Kongole sana wakili msomi. Tuko nyuma yako sisi watanganyika wote. Huyu mama wa kambo arudi kwao na asituuze kwa waarabu.
 
Wewe unadhani Boni ni Dalali kama Kitenge?

Then alivyowanyoosha ikaishia wapi? Wapiganaji hawafi bali wana-mutliply strength in numbers!
Kwenye mitandao kweli lakini huku mitaani hata hamjulikani kumepoaa. Mwenyekiti aliwekwa ndani mkaweka matako yenu chini kimyaaa. Wale sijui covid 19 tu CCM wamewaamulia tu umeufyataaa. Ila kwenye mitandao utasema kuna nchi nyingine ndio maana wanawapuuza tu.
 
Wakili Mwabukusi hapo amezidisha ukali wa maneno na matamshi yake, tena sana. Mpaka roho imenistuka dah!!!

Hata viongozi wa vyama vya upinzani kina Tundu Lissu, Freeman Mbowe, Zitto Zuberi Kabwe, Yuda Iskarioti (Prof Lipumba) hawajawahi kutoa matamshi makali kiasi hicho!

Sisi wengine kila kukicha tunaitoa kasoro Serikali, Mawaziri na CCM kwa maamuzi wanayofanya, tokea enzi za mwendazake. Kila siku tunavurugana nao mitandaoni... Ila hatujawahi kuthubutu kufikia kutoa maneno makali na yenye ukakasi kiasi hicho!

Mungu iongoze Tanzania, Mungu Ilinde Tanzania. #TanzaGiza!
Wakili Boniphace Mwabukusi amekuja kwa ghafla. Huyu ndiye man of the moment. Anaongea kwa mode ya kiuchungaji kwa kufoka anapojenga hoja zake.

Anyway ngoja tuone hatma yake japo kazidisha matusi na dharau
 
Back
Top Bottom