TANZIA Wakili Geofrey Noah afariki dunia kwa tatizo la Nimonia

TANZIA Wakili Geofrey Noah afariki dunia kwa tatizo la Nimonia

Kwani hao waliopona hapo juu inathibitisha kuwa punguani walikuwa sahihi kudai kuwa Corona ni mafua kama mafua mengine?
Inathibitisha kuwa watu wanaumwa na kupona kwa wingi sana tu na kwamba hivyo vifo vinavyotangazwa humu si kwamba ndio picha halisi. Kuhusu mafua ni ugonjwa unaowaua sana wenzetu huko na sasa corona pia imewauwa sana sasa sijui ni vp hapo.
 
Aisee balaa gonjwa halichagui masikini wala tajiri likikufuma ni linapita na wewe moja kwa zote.
Hawa ni baadhi ya watu waliyowahi kuugua Covid-19 na wakapona.



Anna Mghwila.

Mwana FA.

Salam SK.(meneja wa Diamond?)

Mtoto wa Magufuli.

Mtoto wa Mbowe.




Na sasa Maalim seifu amejitangaza kuumwa Covid-19, tunaimani atapona pia
 
Mkuu

Wakili Msomi nadhani ni direct tafsiri kutoka ile ya Kingereza inayotumika mahakamani ya "Learned Brother"

Sasa hiyo "Learned" basi Wabongo kwavile tunapenda mteremko watu wakatafsiri directly "Msomi" au "Aliesoma",etc
Mkuu uko sawa, ila nashangaa tu hawa jamaa wakihitimu masomo yao wanajiona wako juu sana kujipa hilo jina.
Wengine vibonde tu
 
Ajabu haiwapati wanaobanana kwenye msongamano kwenye daladala nk iinawawinda self drive!!! High profiles!!! wanao keep social distancing na kuepuka misongamano!

Hivyo vifo sio Corona ni maradhi mengine tu.
Wanaobanana siyo watu maarufu hivyo vifo vyao havijulikani na kutangazwa kwenye mitandao. Hawa wanaotangazwa wengi ni viongozi, wasomi na wafanya biashara wakubwa hivyo wanajulikana sana.
 
Ila tuchukue tahadhari, hali si nzuri. Tupunguze mikusanyiko na kusali kwa bidii. Naunga mkono sana msimamo wa mh Rais wetu lakini kuna kazi kubwa ya ku create awareness ili kupunguza vifo.
Msimamo gani unaoungunga mkono? Kwa nini magonjwa mengine husemi watu wasali kwa bidii?
 
Unaunga mkono ujinga na uongo kwamba Tanzania hakuna corona? We vipi!? 😳
Huyo jamaa ni kaputi mmoja hivi aliumizwa Dr Slaa alipompisha Lowassa kugombea nafasi ya urais 2015. Huenda ni ID ya mke wake dr. Siku hizi amejitoa ufahamu na Magufuli hata atembee uchi yeye ni kuunga mkono tu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Unajua walalahoi wana advantage maana Muda wote wako kwenye pilika pilika. Sasa hawa wasomi wanaotembelea makalio wako kwenye hatari zaid kwa sababu Muda mwingi miili Yao hawaishughulishi tangu anaamka asubuhi adi anarudi kulala, utakuta hajatoka hata tone la jasho, mwanzo mwisho ni kukaa tu. Na hapo ukute ana liugonjwa lake uko kishkaji, Mapresha wooii..covid ikimfika inakuwa hatunaye tena.
Na wewe unaamini hakuna walalahoi wanaokufa? Wapo wengi tu ila hawatangazwi kwa sababu hawajulikani. Habari zao huishia mitaani kwao tu. Unategemea eg muuza mkaa apostiwe hapa?
 
Hii pneumonia ya Tanzania ni tofauti na ya mataifa mengine?
Ndugu yangu umeuliza swali la msingi sana lakini halitakuwa na jibu na watu wanaonekana wanaishi kama mambo yako sawa tu! Tatizo serikali haifanyi chochote hivyo ni vigumu hata kujua kama ni virus wame-mutate na kuwa wakali zaidi. Kuna kitu hakipo sawa kwani wanafariki watu walio kwenye umri mdogo.
 
Hao kajambanani kama wewe wakidedi hawatangazwi. Wanazikwa fasta tu. Mbona hili halihitaji shule kulielewa?
Ndugu yangu wengine wanafikiri kwa kutumia viungo tofauti labda. Anategemea muuza genge atangazwe hapa? N
 
Yaaani sio mchezo kabisa .... hii mikoa hali sio nzuri
RIP
Hii akili yenu etu wakili msomi sijui mnatoa wapi,.

Kuna wakili asisome? Huyo atakua katibu kata.

Mawakili wengi wao wanapewa hiyo calliber kutokana na vyeo vya baba zao.

Kakae nao kwenye vyungu wanatoka na pneumonia.

RIP Wakili msomi, yuko mwenzio kaoa mke field Marshall wa vyungu Gwajima.
Mkuu sio kila kitu lazima uchangie waachie fani yao waitane hivyo
 
Kabisa Mkuu katika watu wasio na misimamo hapa jamvini huyo ni mmoja wao. Alikuwa Chadema damu damu mara tu akabadilika na kuwa mtu wa Lumumba.
Huyo jamaa ni kaputi mmoja hivi aliumizwa Dr Slaa alipompisha Lowassa kugombea nafasi ya urais 2015. Huenda ni ID ya mke wake dr. Siku hizi amejitoa ufahamu na Magufuli hata atembee uchi yeye ni kuunga mkono tu.
 
Katika hao uliowataja, ni wachache wanaweza kumudu hizo gharama za hospitali ambazo zinaweza kuwapunguzia maumivu ya kushindwa kupumua. Wengi hufia majumbani mwao na taarifa ni nadra kufikia umma.
Hii nakataa bana hatujafikia huko labda unambie uko nchi gani
 
Ajabu haiwapati wanaobanana kwenye msongamano kwenye daladala nk iinawawinda self drive!!! High profiles!!! wanao keep social distancing na kuepuka misongamano!

Hivyo vifo sio Corona ni maradhi mengine tu.
Low profile people inawapata sema uwa hawatangazwi
 
Back
Top Bottom