Wakili Ishabakaki: Idris Sultan anahojiwa kwa kuicheka picha ya Rais

Mwisho wa siku watamuwekea madawa ya kulevya nyumbani kwake.
 
Elewa wewe si lazima uwe na mwanasheria. Unaweza jiwakilisha mwenyewe kwa mujibu wa sheria. Nilikuuliza mwanasheria ndo nani baada ya wewe kutaka kuconclude kuwa mwanasheria kasema. Swala hapa si mwanasheria bali ni proof beyond reasonable daught! Hii ndo mahakama ungalia ili kumweka mtu hatiani katika upande wa makosa ya jinai. Siyo a mere say by an advocate to the public relied on medias. Kama unahitaji tuingie kisheria itakuwa vizuri. Pia nami naweza matusi sana. Ila ni nzuri kum.. ignore mtu atukanae, automatically tusi umrejea yeye mwenyewe. U pumbavu wa atukanae ujidhania yeye ni mjanja kumbe ujanja wake waweza kuwa ushenzi wa kutoelewa mambo.
 
Hiyo picha nimeiona ila sijaona apo mtu ambae ni Rais mkuu..maana Mh.Magufuli amekua Rais wetu kuanzia 2015.
Sasa ni picha yake. Hoja hapo kinachoongelewa ni nafsi yake, hata ingengelikuwa ya utotoni ni yake.

Ndiyo maana mtu anaweza akafanya makosa let say akiwa na umri wa miaka 20, lakini akaja kupatikana na hatia baada ya miaka 30 mbele huko.

Je Kwa kuwa atakuwa ni mtu mzima, ataiepuka adhabu kwa kuwa kavua umri ule na kuvaa umri mwingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwenye hiyo picha kuna Rais wa mwaka gani?
Je,kucheka si maana mtu amefurai au siku hizi kucheka sio furaha tena?
 
Mkuu kwenye hiyo picha kuna Rais wa mwaka gani?
Je,kucheka si maana mtu amefurai au siku hizi kucheka sio furaha tena?
Point yangu hapo ni kujibu picha ya nani.

Hsyo mengine kuhusu kuchekesha ama kuhuzunisha inategemeana na mtu anavyoichakata hiyo picha kwenye ubongo wake.

Kwa mfano mimi nilipoiona ni kastaajabu kitu gani cha kuchekesha hapo?

Kama ni hizo suti za six button na masuruali mapana yalivaliwa sana enzi za utawala wa Mkapa, ilikuwa ni fashion pendwa, kila mwenye uwezo alitamani kushona.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Seriously! Yaani ni kosa kumcheka Rais? Tena picha ya mtu aliekuja kuwa Rais!!! Seriously?
Tena kaamua mwenyewe kuvaa oversize?mbona wenzake wa umri ule walikuwa wanatokelezea kimaridadi tu!
 

I honestly don’t think you’re being serious. I think you’re being facetious.

I don’t see how Magufuli can invoke intentional infliction of emotional distress here.

He is the president. He wanted to be president. He asked people to vote for him so he could be one.

He is the foremost public figure in the country.

It comes with the territory. If he can’t handle being in the limelight, he should quit and go live a private life somewhere.

He works for us. Not the other way around. Remember that.
 

Hakuna lolote. Dogo hajatenda kosa lolote.

Kucheka si kosa.

Na ndo maana hamna hata kifungu cha sheria mnachoweza kukitaja kusema kuwa kakivunja na hivyo kustahili kukamatwa na kuwekwa ndani.

Mabavu tu yametumika. Na huo ni unyanyasaji.

Kucheka kamwe haliwezi kuwa kosa. Hivyo hakuna heshima aliyovunjiwa Magufuli.
 

Kwani ukicheka halafu urushe kwenye social media ndo inakuwaje?

Magufuli aache kunyanyasa watu.

Urais aliutaka mwenyewe. Urais unakuja na mambo mengi sana.

Rais anapaswa kuwa mvumilivu sana kushinda watu wengine. Magu anapaswa awe na ngozi nene.

Why is he so sensitive?

Idris hana kosa hapo.

The laugh was innocuous.
 
Kuna kitu huwa kinanishangaza sana. Hivi inawezekana vipi mfano unagandamizwa, kunyimwa haki, democrasia, uhuru wa kujieleza na kadhalika then ukawa tena unaunga mkono ugandamizaji huo dhidi yako?! Haya nayaona sana hapa Tanzania. Inasababishwa na nini?
 
Marekani, nchi ya makazi yangu, nchi iliyoendelea kiuchumi kwa kupitia figisu nyingi sana na kuweka misingi ya sheria, imejiwekea sheria hivi.

Mimi Kiranga, raia, nikitaka kuchukua picha yako Nyani Ngabu, raia mwenzangu usiye na cheo, halafu niiweke picha ike kwenye T-Shirt. Labda tuseme wewe Nyani Ngabu ni firefighter uneokoa watu, nikiweka picha yako kwenye T-Shirt, ama kwa kuuza ama kwa kuvaa mimi mwenyewe, ama kwa kukusifu, ama kwa kukutukana, wewe una uhuru wa kunishitaki na kunishinda mahakamani nisiweke picha yako. Ukashinda kesi, mimi nifungwe au nilipe faini, na nikatazwe kutumia picha yako.

Kwa nini? Kwa sababu wewe ni private citizen. Una privacy rights kubwa sana.

On the same token.

Nikiamua kuchukua picha ya Donald Trump. Niziweke kwenye T-Shirt. Ama kwa kumsifu, ama kwa kumtukana. Donald Trump na serikali yake hawana haki ya kisheria ya kunukataza.

Nina ruhusa za kuchapisha T-Shirt za kumtukana Donald Trump, nikaweka picha yake na maneno "Donald J. Trump is a douchebag".

Kisheria, hiyo ni sehemu ya free speech tu. Hakuna sheria itakayonikataza.

Raia wa kawaida anatetewa na sheria kuliko rais katika hili.

Kwa sababu, rais alikuwa na uchaguzi, awe raia wa kawaida aachiwe maisha yake yawe private bila figisu na maneno mengi, au atake uongozi, kwa kujua "ukubwa gunia la chawa", pamoja na figisu zote zinazokuja na uongozi.

Akachagua figisu. Hakuchagua privacy.

Sasa keo watu wamemcheka suti msulupwete tu?

Sasa akitukanwa kikwelikweli serikali itaweza kuvumilia?

Tuna umasikini kwa sababu nyingi sana.

Na serikali yenyewe ina ji undermine. Haijui kula na kipofu usimshike mkono.

Sasa wanaendesha serikali kisiri na kujuwekea mazingira ya kuiba mabilioni, watu hawahoji.

Unapoanza kukamata watu wanaomcheka rais kwa sababu ya suti msulupwete, hapo ndipi unaanza kumgusa mkono kipofu unayekula naye.

Wanaiba kura, wanaiba hela, hata kuwaachia uhuru wa msingi tu watu wacheke wasahau machungu wanashindwa?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Ujinga na umasikini. Ukijitambua huwezi kuwa na akili za kishamba hivo.
Yaani kumcheka kiongozi ni kosa. Wallahi tunapo elekea ni shimoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafuatilia sana habari za migawanyiko ya kisiasa. Nilitaka kujua kwa kiasi gani migawanyiko hii ni ya kimazingira, na kwa kiasi gani ni ya kibaiolojia.

Nilikuwa nashangazwa sana inawezekanaje watu fulani wakaamini habari fulani ambazo mimi naona upumbavu wa wazi kabisa.

Nikauliza rafiki zangu swali hili. Rafiki yangu mmoja aka recommend kitabu kinachojadili mambo haya. Nakisoma hicho kitabu sasa hivi.

Nasoma kitabu hiki kinaitwa "Our Political Nature: The Evolutionary Origins of What Divides Us" cha Avi Tuschman.

Kitabu kizuri, kimejaa usomi na mifano hai. Ana argue a lot of this divide has evolutionary origins.

Haya mambo si Tanzania tu.

Kuna mtu aliandika kitabu kingine kinaitwa "What's The Matter With Kansas: How Conservatives Won The Heart of America" cha Thomas Frank.

Jamaa anaelezea habari kama uliyoulizia, katika Marekani. Demicrats wanakuja na sera nzuri tu za kusaidia watu masikini, kama vike kuwapa universal health care, halafu hao hao watu masikini wanakataa Democrats kwa conspiracy theories jwamba hao Demicrats wanataka big governments zitakazowaua bibi zenu!

Huko Tanzania kuna watu wanapenda hero worship tu, kwa hiyo ukiwa rais gangwe, mgandamizaji, ndiyo unaonekana unajua kazi, unakomesha watu, wakiwamo hata hao wanaokusifia.

Yani it is like some form if political sado masochism. Watu wanapendwa kupigwa, usipowapiga watakuita dhaifu.

Tanzania watu wengi wanaomsifia Magufuli ni wanaoumia kutokana na sera za Magufuli.

Halafu wanajazwa ujunga wa "mabeberu wanatuandama". Evolutiinary herd thinking za kuchagua kundi zina kick in. Watu wanachagua "my country, my president".

Wanazidi kupigwa na huyo huyo rais wao.

A lot of this is evolutionary.

Kama hujasoma hivyo vitabu, vitafute usome utaona mambo yote yameelezwa humo.


Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…