Pre GE2025 Wakili Jebra Kambole: Jinsi ilivyo ngumu kumnadi Mbowe; sasa mpitisheni muone itakavyokuwa ngumu kuwanadi wagombea 2025. Mtapita kama mnaaga maiti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mnataka kutushawishi kuwa CHADEMA bila Mbowe haiwezi kuwepo? Ameongoza kwa miaka 20+ na amepewa ushirikiano wa kutosha kwa nini inakuwa vigumu na yeye kuwapisha wengine na awape ushirikiano na yeye atoe ushirikiano kuipeleka mbele CHADEMA?

Nini bado hajatimiza pale au mnataka CCM wapate kuthibitisha hoja yao kuwa hii ni SACCOS ya Mbowe?
 
Wakili Jebra Kambole,wewe sio mpiga kura! Jukumu la kuchagua Mwenyekiti wa Cha Chadema,waaachie wajumbe,ambao ndio wapiga kura.
Ikifikia kumchagua Rais wa TLS, nasi tutawaachia mfanye mambo yenu!
Hapo umejibu hoja yake au umeamua kumjadili mtoa hoja?

Je CHADEMA haistahili kuongozwa na mtu mwingine zaidi ya Mbowe?

Au wanasheria hawaruhusiwi kuwa wanachama wa CHADEMA?
 
Huyu mwanasheria wa mchongo ni kichaa
 
Unajua toka 2012 sijaona lugha ya kifedhuli kutoka kwa Pascal, tuachie siye tuliochanganyikiwa na siasa za Tanzania, nawachukiaga CCM lakini si Pascal Mayalla na uccm wake
Nisamehe sana,nimekuwa provoked sana kwasababu nilimshauri Mhe。 Mbowe apumzike toka 2010 CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
P
 
Wewe mzee wa hovyo wa CCM inakuwaje kada mtetea wezi wenzio wa CCM mkawa na maslahi ghafla ya CHADEMA?

Pili kwa nini makada wa CCM hadi mama Abdul na Abdul hamumtaki Tundu Lissu? Nyie chini ya Mbowe mmepora utajiri wake kakaa kimya.
Mkamfungulia kesi ya uhaini ambayo adhabu yake ni kifo au kiungo cha maisha kakaa kimya.
Mkamdanganya mazungumzo ya maridhiano mwaka mzima kisha mkakataa yote mkaenda kuiba uchaguzi wa serikali za mitaa kakaa kimya.

Vipi baada ya Tundu Lissu kukataa hela za mama Abdul mmeona huyu hamuwezi kumuinamisha kichwa kama kondoo kwa jinsi mlivyomfanyia Mbowe mmejiunga kumpiga madongo Lissu?

Nini maslahi yenu nyinyi CCM kwa Mbowe?
 
Wakili Jebra Kambole amesema Jinsi ilivyongumu leo kumnadi Mbowe kwenye nafasi ya Uenyekiti hata mara baada ya kumpitisha watakutana na ugumu huo huo kwa Wananchi katika kuwanadi wagombea wote katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 chini ya MBOWE.
Hata wagombea hawatapatikana. Kwasabb chini ya Mbowe hakutakuwa na wanachama wa chadema, wengi wataondoka.
 
Mkuu Mbangaizaji wa Taifa ,kama ni USAJIRI, basi huo upande imepata MSHAMBULIAJI HATARI SANA!
Umejiunga hapa JF 25/12/2025, yaani juzi, na nafikiri ni baada ya KUVIMBIWA PILAU LA KRISMASI. Lakini, umesha anzisha thread KUMI za kuuponda upande wa pili usiouunga mkono! Toka usajiri hii "akaunti mpya", haujawahi kuandika chochote tofauti na kuinanga ile timu usiyoipenda!
Nyuzi zako 10 hizii….

1
Mchungaji asema Mbowe ni tapeli hawezi kupigania Katiba mpya itakayoleta ukomo wa uongozi wakati yeye miaka 20 na hana mpango wa kuachia uongozi.

2
GEORGE KABADI: Siasa zinabadilika sana. Leo kumnadi Freeman Mbowe imekuwa ngumu, hii ni sawa na kunadi nyama ya kitimoto visiwani Zanzibar mchana.

3
Wakili Zebra Kambole: Jinsi ilivyo ngumu kumnadi Mbowe; Sasa mpitisheni muone itakavyokuwa ngumu kuwanadi wagombea 2025. Mtapita kama mnaaga maiti.

4
ARUSHA: Wananchi wamzomea Mgombea Uenyekiti Taifa Odera Charles Odera wakidai yeye na Mbowe ni mapandikizi ya CCM.

5
CHADEMA tupate wapi mtu kama huyu anayependwa hivi?

6
Wakili Edward Heche atangaza kumuunga mkono Tundu Lissu, asema ni mtu pekee anayechukia rushwa kwa moyo na roho yake yote.

7
VIDEO: Baada ya kumsikiliza huyu mjumbe wa CHADEMA, nimebubujikwa na machozi.

8
Askofu Benson Bagonza: Viongozi wana nguvu sana katika vyama kuliko wanachama. Dola inatumika kuingilia chaguzi ndani za vyama vya siasa.

9
Ibrahim Ngogo: Ametoa wito kwa wajumbe wa chama hicho, kumpigia kura Tundu Lissu.

10
TUNDU LISSU. Ni kweli CHADEMA kimepoteza mvuto hasa kwa vijana na walalahoi.

--Kama ni usajiri mpya unaolipa, basi ni huu. Muda wote upo kwenye goli la mpinzani!
 
Hapo umejibu hoja yake au umeamua kumjadili mtoa hoja?

Je CHADEMA haistahili kuongozwa na mtu mwingine zaidi ya Mbowe?

Au wanasheria hawaruhusiwi kuwa wanachama wa CHADEMA?
Punguza maneno,tuonane siku ya uchaguzi!
Ila mkubali matokeo!
 
Mbowe kafanya kosa kugombania tena uenyekiti? Ilitakiwa Wakili Naomi TL agombanie mwenyewe?! Mashabiki wa hawa mamba miwili wameleta matatizo sana. CCM washazoea hizi mbanga
 
Gentleman,
si ujikite kwenye hoja mahususi mezani bila mawenge na mihemko kwa yasiyo husu hoja mezani,

nadhani wew, huyo alietajwa kwenye hoja na kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi mmepoteza uelekeo kabisaa, mnatapatapa na kuweweseka vizuri sana,

itabidi mzoee sasa maana hakuna namna nyingine 🐒
 
Mbowe hana mvuto, sasa ni wakati wa Lissu
 
Big up Wakili Kambole umeongea ukweli.
 
duh! Hii kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…