Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Mwanasheria maarufu, Aloyce Komba ametoa maoni yake kuhusu maswali ya dodoso yaliyofanywa na mawakili wa Serikali wakuu, akiwamo Wakili Nassoro Katuga. Haya ndio maelezo yake:
1. Ilidhalilisha taaluma ya sheria kwani ilikusanya maswali mengi ya umbea wa kisiasa na maisha binafsi ya shahidi ambayo hayahusiani na hati ya mashitaka ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu.
2. Ilimfanya Heche naye ajibu kisasa na kwa self defence of status.
3. Iliwachosha majaji kuandika vitu ambavyo sijui wataviunganisha vipi na ushahidi wa mashahidi wa awali wa utetezi.
4. Ilionyesha kwamba hata kama ktk cross exam wakili unaweza kuuliza chochote lakini ni muhimu kihusiane na kesi ya msingi au ushahidi wa awali wa shahidi yaani his testimony in examination in chief.
5. Ilikuwa si mfano mzuri wa kufundishia law school au kwa pupillage ya wanafunzi wa uwakili in our law firms.
Nikawakumbuka majaji hawa waliokuwa na tabia ya kutoandika na kufanya vitu vingine iwapo wakili unahoji kwa maswali yasiyoeleweka wakati wa cross exam: Mapigano, J. (Kusoma gazeti), Ndyansobera, J. (Kupanga karatasi na statutes), Rugazia, J. (Kutafuna pen na kuangalia pembeni), Ruhangisa, J. (Kuchora tu cartoon), Mgeta (John), J. (Kujifanya amesinzia).🤣⚖️🤣
Tumsome vizuri yule wakili wa Uingereza (Queen's Counsel) mtunzi wa textbook iliyoandikwa kama notes za kufundishia kiitwacho “A devil's advocate" (Ian Morley) anavyotutahadharisha kuhusu cross examination.
AAK Jnr, SC, Esq.
15th Sept. 2026
Soma pia: Kutoka Mahakamani - 15 Septemba, 2026: John Heche aendelea kutoa ushahidi