"Hata kwenye Sheria yetu ya Kanuni ya adhabu imeeleza kwamba Mwanamke ni nani?, ili kueleza kwa nini tunasema Mwanaume ndiye anayeweza kubaka na sio Mwanamke, japo siku hizi kuna Kampeni nyingi, Wanaume nao wanasema na wao wanabakwa wasikilizwe, lakini sababu kubwa ndio hiyo kuwa kuna mwenye 'kibakio' na mwenye 'kibakwa' ni hivyo" -Wakili Getrude
"Haiwezekani mwenye 'kibakio' akabakwa kwa sababu kinachotumika kubaka anacho yeye kwahiyo huyo hana, Kwahiyo hawezi kumbaka, naona kama Jamii inatafuta sehemu ya kujifichia" -Wakili Getrude
Wakili Getrude Dyabene kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) amezungumza hayo leo, Jumanne Januari 16.2024 wakati akifanya mahojiano maalumu na Clouds FM kupitia Kipindi cha Power Breakfast