Wakili Madeleka: Rais Samia nakusihi, Futa huu Mkataba wa Bandari

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 12, 2023, Wakili Peter Madeleka amesema watu wengi wanaomchukia hawamwambii ukweli Rais Samia zaidi wanaishia kumsifia hata anapokosea. Amesema Rais Samia anatakiwa kukaa na kutafakari kusudi la Mungu wake kumfanya awe Rais kwasababu hakupigiwa kura na Wananchi bali aliwekwa kwa lengo la kuweka mambo sawa.

Akiongelea kuhusu sakata la Mkataba wa Bandari amesema, Rais ana mambo mawili ya kufanya ili akumbukwe na Watanzania mambo ambayo ni kuwapa Katiba Mpya pamoja na kufuta Mkataba

Pia soma: Mkutano wa Dkt. Slaa, Askofu Mwamakula, Wakili Mwabukusi na Madeleka
 
Bado wanabweka tu!!..tulipoamua DP world aje kuwekeza tulifanya hivyo baada ya tafakuri jadidi,hatutayumbishwa na watu wanaomchukia mwarabu,mkataba tutasaini soon
Acha kuonesha kiwango cha akili yako
Hadharani.watanzania wamekaa huu mkataba na hakuna aliyemkubwa kuliko Tanzania na waliyoonesha kuwa wao ni wakubwa kuliko Tanzania wamepotea.
 
Bado wanabweka tu!!..tulipoamua DP world aje kuwekeza tulifanya hivyo baada ya tafakuri jadidi,hatutayumbishwa na watu wanaomchukia mwarabu,mkataba tutasaini soon
Mwarabu ni mjomba wako? Eventually ataondolewa tu. Just a matter of time.
 
Bado wanabweka tu!!..tulipoamua DP world aje kuwekeza tulifanya hivyo baada ya tafakuri jadidi,hatutayumbishwa na watu wanaomchukia mwarabu,mkataba tutasaini soon

Unaona kabisa umeongea point, na unaweza kujiona una akili timamu maskini ya mungu
 
Kuendelea kukumbatia mkataba wa hovyo ni ujinga uliopitiliza, kushindwa kujiheshimu mwenyewe, na kuwaheshimu wale unaowatumikia.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 12, 2023, Wakili Peter Madeleka amesema watu wengi wanaomchukia hawamwambii ukweli Rais Samia zaidi wanaishia kumsifia hata anapokosea. Amesema Rais Samia anatakiwa kukaa na kutafakari kusudi la Mungu wake kumfanya awe Rais kwasababu hakupigiwa kura na Wananchi bali aliwekwa kwa lengo la kuweka mambo sawa.

Akiongelea kuhusu sakata la Mkataba wa Bandari amesema, Rais ana mambo mawili ya kufanya ili akumbukwe na Watanzania mambo ambayo ni kuwapa Katiba Mpya pamoja na kufuta Mkataba
View attachment 2685806

Pia soma: Mkutano wa Dkt. Slaa, Askofu Mwamakula, Wakili Mwabukusi na Madeleka
Mbona anasahau kumwambia aufute huu uvamizi uitwao muungano ulioiangamiza Zanzibar tokea 1964

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 12, 2023, Wakili Peter Madeleka amesema watu wengi wanaomchukia hawamwambii ukweli Rais Samia zaidi wanaishia kumsifia hata anapokosea. Amesema Rais Samia anatakiwa kukaa na kutafakari kusudi la Mungu wake kumfanya awe Rais kwasababu hakupigiwa kura na Wananchi bali aliwekwa kwa lengo la kuweka mambo sawa.

Akiongelea kuhusu sakata la Mkataba wa Bandari amesema, Rais ana mambo mawili ya kufanya ili akumbukwe na Watanzania mambo ambayo ni kuwapa Katiba Mpya pamoja na kufuta Mkataba
View attachment 2685806

Pia soma: Mkutano wa Dkt. Slaa, Askofu Mwamakula, Wakili Mwabukusi na Madeleka
Hayo mambwa yamehongwa yapindue serikali, huo mkataba unatumika tu km geresha. Walitaka kuanzisha chama wakitumia picha ya Magufuli km mtaji. Kwa ninavyoifahamu nchi yangu na vyombo vyake vya ulinzi na usalama wataishia kubwabwaja tu, hata miaka 100 ijayo hayo malengo yao hayatafanikiwa kamwe. Ngedere tu hao.
 
Naunga mkono hoja ya kuufuta huu mkataba.
 
Mimi sikubaliani na mkataba na naona bora uvunjwe.

Lakini wakili Peter Madeleka amepotosha kwamba Dubai haiwezi kuingia IGA na Tanzania, kwa sababu si nchi.

Wanasheria wetu hata hawa tunaowaona nguli bado wanapwaya sana.

TLS walikuwa wajanja sana wakakubali kwamba hawana taarifa kamili katika jambo hili na wanahitaji mtu anayeelewa mambo ya Dubai zaidi, that was prudent and truthful.

Madeleka anapotosha katika hili.

Nuance please.
 
Back
Top Bottom