DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Wakili Shabaan Marijani amesema watu wote waliyotajwa katika zuio la Mahakama la kutokushiriki shughuli zozote za kisiasa katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hawaruhusiwi hata kuzungumza na vyombo vya habari.
Aidha, amesema wakitaka kuzungumza na vyombo hivyo wasizungumze masuala ya chama, waeleze mambo mengine ambayo hayaingiliani na amri ya zuio hilo lililotolewa Juni 10,2025 na Jaji Hamidu Mwanga.
Wakili Marijani amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na upotoshaji uliyokuwa ukiendelea kuhusiana na zuio lililotokana na shauri dogo namba 8960/2025 katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
"Hawatakiwi hata kuzungumza na waandishi wa habari kwa sababu tayari Mahakama ilishatoa amri ya zuio hapo wanakuwa wamekiuka amri hiyo," Amesema Wakili Marijani
Kwa upande wake, Wakili Gizo Simfukwe amesema Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imetoa ufafanuzi wa wahusika 10 wa zuio hilo kutokana na baadhi ya watu kujiondoa kwamba hawahusiki.
"Kutokanana na upotoshaji huu na sisi kama wanasheria tunawawakilisha wateja wetu waliyofungua hii kesi tulimuandikia Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam barua kuomba ufafanuzi wa kisheria kwamba Je! lile zuio lililotolewa linawahusu wakina nani," Amesema Wakili Simfukwe
Amesema kuwa wamepokea barua ya majibu kutoka kwa Msajili ya Julai 14,225 ambayo hata wenzao wa upande wa pili wa kesi hiyo na wao wamepewa nakala yake, ambapo baadhi ya watu walisema zuio ni la Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu.