Wakili Mgongolwa: Katiba inamruhusu Rais kumuongezea muda Jaji Mkuu

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Kupitia kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kupitia Clouds FM, Mwanasheria wa kujitegemea Alex Mgongolwa ameeleza kuwa Rais anayo Mamlaka na hajavunja Katiba kwa kumuongezea muda wa kuhudumu Jaji Mkuu wa Tanzania

Msikilize hapa, kisha tujadili nini maoni yako?

Pia soma > Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuwa Jaji Mkuu, Rais Samia anavunja Katiba ya JMT?

--
Mwanasheria wa kujitegemea Alex Mgongolwa ambaye amekuja kutuweka sawa kuhusu nafasi na uwezo wa Mhe Rais katika kumuongezea muda Jaji Mkuu, ikiwa ni baada ya sintofahamu iliyoibuka ikihoji kuhusu kupitiliza kwa muda wa utumishi wa Jaji Mkuu! Katiba inasemaje!?

Mahakama.png
 
Wakili wetu msomi Pascal Mayalla
Naye anasemaje kuhusu hii

Ova
Japo mimi ni wakili, ila mimi sio wakili msomi, mimi ni wakili mtangazaji.

Katiba yetu iko wazi kabisa kwa teuzi zote za rais, akiletewa majina, akaona wote hawatoshi, ana mamlaka ya kumuongezea muda aliyepo kisha kutafuta wa kutosha. Hili limekuwa likifanyika siku zote na hakuna tatizo lolote!.

Ila kwenye kumuongezea muda wakuu wa mihimili, Rais, Spika, Jaji Mkuu na wale the 5 constitution officers, CAG, Chair wa NEC, Msajili wa Vyama, Chair wa Tume ya Maadili, kuna kipengele kimewazuia kuongezewa muda baada ya kustaafu, hivyo Wakili Alex Mgongolwa amechemka big time alipomtetea rais Samia kuwa hajavunja katiba, kwasababu japo Jaji Mkuu ni Jaji Rufani, na Rais ana mamlaka ya kumuongezea muda Jaji Rufani, lakini Jaji Rufani aliyekuwa Jaji Mkuu, hawezi kuongezwa muda cha Ujaji Rufani kwasababu katiba imezuia maofisa hao kuteuliwa nafasi yoyote ya kiutendaji baada ya kustaafu nafasi zao!.
Hili nomelifungulia uzi Jaji Mugasha Apewe Maua Yake Kupinga Uvunjifu wa Katiba Ukomo wa CJ, ila Mbona Hili ni Dogo Tuu, Kubwa ni Katiba Yetu Imenajisiwa! Why Wako Kimya?!.
P
 
Japo mimi ni wakili, ila mimi sio wakili msomi, mimi ni wakili mtangazaji.

Katiba yetu iko wazi kabisa kwa teuzi zote za rais, akiletewa majina, akaona wote hawatoshi, ana mamlaka ya kumuongezea muda aliyepo kisha kutafuta wa kutosha. Hili limekuwa likifanyika siku zote na hakuna tatizo lolote!.
P
Kwa hiyo alichokiandika Mh Jaji ni sahihi au sio sahihi?
Naomba unisaidie kama hutajali.....natanguliza shukrani.
 
Japo mimi ni wakili, ila mimi sio wakili msomi, mimi ni wakili mtangazaji.

Katiba yetu iko wazi kabisa kwa teuzi zote za rais, akiletewa majina, akaona wote hawatoshi, ana mamlaka ya kumuongezea muda aliyepo kisha kutafuta wa kutosha. Hili limekuwa likifanyika siku zote na hakuna tatizo lolote!.
P
Je, Umesoma vizuri na kuielewa barua ya Jaji Mugasha???
 
Kupitia kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kupitia Clouds FM, Mwanasheria wa kujitegemea Alex Mgongolwa ameeleza kuwa Rais anayo Mamlaka na hajavunja Katiba kwa kumuongezea muda wa kuhudumu Jaji Mkuu wa Tanzania

Msikilize hapa, kisha tujadili nini maoni yako?

Wagalatia ndio wameanzisha izo chokochoko
 
Kupitia kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kupitia Clouds FM, Mwanasheria wa kujitegemea Alex Mgongolwa ameeleza kuwa Rais anayo Mamlaka na hajavunja Katiba kwa kumuongezea muda wa kuhudumu Jaji Mkuu wa Tanzania

Msikilize hapa, kisha tujadili nini maoni yako?

wabishane mawakili na majaji sababu ni fani zenu.mara zote huwa nasema shida ya masomo ya art huwa hayana uhalisia kama hesabu ndo maana kuna kona kona nyingi.ingekuwa hesabu tungeenda na facts.
 
Nasindikiza na sehemu ya ibara.View attachment 2671841
Huo ni uteuzi wa Jaji wa Mahakama ya Rufani (JR), siyo uteuzi wa Jaji Mkuu (CJ). Usichanganye haya mambo mawili kwani JR na CJ ni vitu viwili tofauti.

Rejea kusoma tena vizuri na kwa kina barua ya Jaji Mugasha, barua ya AG aliyonukuu Jaji Mugasha, Katiba ya nchi pamoja na Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayohusika na suala hili. Usikurupuke.
"No research no right to speak".
 
Japo mimi ni wakili, ila mimi sio wakili msomi, mimi ni wakili mtangazaji.

Katiba yetu iko wazi kabisa kwa teuzi zote za rais, akiletewa majina, akaona wote hawatoshi, ana mamlaka ya kumuongezea muda aliyepo kisha kutafuta wa kutosha. Hili limekuwa likifanyika siku zote na hakuna tatizo lolote!.
P
Ni kifungu cha katiba kinachompa Rais ya kumuongezea muda Jaji Mkuu?
 
Kupitia kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kupitia Clouds FM, Mwanasheria wa kujitegemea Alex Mgongolwa ameeleza kuwa Rais anayo Mamlaka na hajavunja Katiba kwa kumuongezea muda wa kuhudumu Jaji Mkuu wa Tanzania

Msikilize hapa, kisha tujadili nini maoni yako?

Pia soma > Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuwa Jaji Mkuu, Rais Samia anavunja Katiba ya JMT?

--
Mwanasheria wa kujitegemea Alex Mgongolwa ambaye amekuja kutuweka sawa kuhusu nafasi na uwezo wa Mhe Rais katika kumuongezea muda Jaji Mkuu, ikiwa ni baada ya sintofahamu iliyoibuka ikihoji kuhusu kupitiliza kwa muda wa utumishi wa Jaji Mkuu! Katiba inasemaje!?

ila hapa msomi kajielekeza vibaya, ibara nukuliwa inazungumzia jaji wa mahakama ya rufaa, na sio jaji mkuu. kumbuka Profesa Juma ana nafasi mbili; yaani ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa na Jaji Mkuu. Katiba imeweka ukomo wa Jaji Mkuu, na Umeacha upenyo wa Jaji wa Mahakama ya Rufaa,

hivyo Rais kwa Mujibu wa Katiba ibara 120 (3) imempa mamlaka ya kuongeza muda wa jaji wa mahakama ya rufaa, na si jaji wa mahakama kuu.

kwa hiyo Rais anawajibika kuteua Jaji Mkuu, kwa mjibu wa katiba na endapo anaitaji huduma ya Profesa Juma kama Jaji wa Mahakama ya Rufaa, basi anaweza kumwongezea Muda wa kuhudumu katika nafasi hiyo na si kama jaji muda
 
Back
Top Bottom