Mjina Mrefu
JF-Expert Member
- Dec 6, 2016
- 3,045
- 3,389
Wakuu,
Ni kuhusu huyu wanayemwita wakili msomi.. Yaani Peter Kibatala. Kila siku nasikia Kibatala, Kibatala. Tujuzane wakuu.
CV yake
Kashinda kesi ngapi?
Kashindwa kesi ngapi?
Tujuzane tumjue huyu wakili anayeitwa msomi
======
Ni kuhusu huyu wanayemwita wakili msomi.. Yaani Peter Kibatala. Kila siku nasikia Kibatala, Kibatala. Tujuzane wakuu.
CV yake
Kashinda kesi ngapi?
Kashindwa kesi ngapi?
Tujuzane tumjue huyu wakili anayeitwa msomi
======
Peter Kibatala said:Nimewahi kuwa Makamu wa Rais wa TLS;2012-2014.
Nimewahi kuwa voted kama Most Influential Young Tanzanian upande wa Law.
Nimeendesha cases za watu maarufu wafuatao:
1. Wakili wa kwanza kupangua mashtaka ya Ugaidi Nchini katika cases za Ugaidi za Wilfred Lwakatare na mwenzake [Mahakama Kuu Kanda ya Dar 2013] na Henry Kilewo na wenzake [Mahakama Kuu, Tabora 2013].
2. Case ya Elizabeth Michael Kimemeta @ Lulu.
3. Case ya Uchaguzi ya Fred Mpendazoe pamoja na case nyingi za Uchaguzi kama vile Halima Mdee na Suzan Kiwanga.
4. Cases zote za Uchochezi za Tundu Lissu ambazo ama alishinda au zilifutwa.
5. Cases za kufutiwa Uwakili Fatma Karume [ambapo baada ya kufutiwa Uwakili alishinda mbele ya Jopo la 3 Judges Mahakama Kuu na AG anakata Rufaa].
6. Case ya Kajala Mahakama Kuu.
7. Case ya Wema Sepetu [kabla Msando hajaichukua].
8. Case ya kina Mbowe ya Maandamano yaliyopelekea Akwilina kuuawa [walishinda Rufaa Mahakama Kuu na kuamriwa warudishiwe fines zao].
9. Case ya Ugaidi ya Mbowe ambayo ilifutwa na DPP hatimaye.
10. Cases mbalimbali za Halima Mdee za maandamano ya BAWACHA [ilifutwa na Mahakama].
11. Cases za Gwajima [ya kupatikana na silaha na ya kumtukana Pengo na zote alishinda].
12. Case ya jinai ya Mbunge wa zamani Mtwara Mjini Hasnain Murji ya kupinga gas kutolewa Mtwara [alishinda].
13. Cases za Uchochezi za Yericko Nyerere [alishinda mbili Kisutu, na moja Rufaa Mahakama Kuu Dar].
14. Case ya Uchochezi ya Sugu [alishinda Rufaa Mahakama Kuu Mbeya na rekodi kufutwa].
15. Sasa naendesha case ya Mauaji ya mke wa "Bilionea" Msuya.
16. Case ya kupinga uenyekiti Augustin Mrema TLP [alishinda].
17. Case ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Air Tanzania David Mattaka [aliachiwa huru na kupigwa fine ndogo].
18. Case ya kupinga kauli ya Waziri Mkuu wa zamani Mizengo Pinda kusema "wanaondamana wapigwe tu" [Mahakama Kuu ilisema Wabunge hawana kinga isiyo na mipaka kwa kauli wanazotoa Bungeni, principle ambayo ni ya muhimu sana].
Naendesha case ya kudai haki ya Uraia Pacha kwa niaba ya watu wa Diaspora