Kweli huijui sheria, na hata vipengele vya kisheria kwenye mikataba huvijui pia maana yake.
Hapo suala sio lazima mpaka viongozi wa Yanga SC wakae na Azam ndio waongee biashara, muhimu ni kama umeweka kipengele kwenye mkataba wa mchezaji wako kinachomruhusu kuondoka aki deposit kiasi fulani cha pesa, basi hapo umejibana mwenyewe.
Mchezaji ataondoka wakati wowote akiamua, muhimu aweke pesa mliyotaka kwenye akaunti yenu, hapa suala la Yanga SC kuongea na Azam linakuwa halina maana tena, halipo, kwasababu mchezaji ameshavunja mkataba na Yanga SC kwa kuweka mzigo kwenye akaunti, huyu sasa ni sawa na mchezaji huru.