Wakili Msomi: Yanga wamefanya uzembe kwa Feisal

Wakili Msomi: Yanga wamefanya uzembe kwa Feisal

Neymar alienda PSG bila makubaliano kati ya psg na barca.
Alichofanya neymar ni kuvunja mkataba 250 million euro. Then akawa free agent akaenda zake PSG. Yaani hata FFP haikuwa na nguvu yoyote hapa..
Hujui kitu , Neymar hakulipa pesa yeye kihuni bali PSG waliwalipa Barca hiyo pesa na akawa mchezaji wa PSG .
 
Hi I unajua kuna tofauti ya signing fee na release clause? Neymar aliwalipa Barca signing fee au release clause?
Hujui unachoandika, unadandia dandia maneno ya wanasheria uchwara wa vijiwe vya kahawa...hebu tufafanulie hiyo signing fee na release clause then tuambie ina apply vp kwa Fei. Tatizo la Fei ni udhaifu wa mkataba
 
Mikataba ya football haipo hivyo inafuata msimu hauvunji tu kama taraka ya ndoa
Mikataba ipi hiyo ya football isiyoweza kuvunjika?
Mikataba yote, dunia nzima, muda wowote inaweza kuvunjwa. Mikataba inaweza kuvunjwa ndani ya utaratibu uliowekwa au nje ya utaratibu. Mkataba ukivunjwa nje ya utaratibu fulani uliowekwa, mhusika anawajibika kulipa fidia kulingana na sheria za huo mkataba.

Yanga haiwezi kulazimisha Feisal kubakia Yanga, Feisal ameamua kuachana na Yanga, hivyo amelipa fidia ya mkataba wake kuvunjwa, na sasa yuko huru.
 
Hapo sijui Sheria is kuna raia ni vilaza sana kwenye soka,umeona wapi mchezaji mwenye mkataba na timu anasajiliwa na timu nyingine bila hizo timu kukubaliana? Yaani Leo Jude Bellingham apokee pesa kutoka Man City akailipe Dortmund then awe mchezaji wa Man City bila City na Dortmund kukubaliana?
Basi wachezaji wengi sana wangesepa Kwa namna hiyo.
Bro ayo ni maoni yako, lakini kwani huonagi wachezaji wengi wakivunja mkataba na timu zao na kubaki wachezaji huru. Klabu inabidi iwe na ustadi wa kumbana mchezaji kwa kutokumpa uwezo wa kuuvunja mkataba kitu ambacho yanga wameshindwa kufanya. Mbona Dejan kavunja mkataba na simba akawa free agent saiv yuko tim nyngne. Ndomana yanga wanaitwa utopolo, hawana hata ustadi wa kutengeneza vizuri mikataba. Lakini shida hio sio kwa yanga tu hata tim nyngne bongo. Shida ni Elimuu!!!
 
Rejea ya Neymar utanielewa, mlijichanganya kuweka kipengele cha kuvunja mkataba endapo mchezaji ataweka dau (kununua mkataba wake) Fei kaweka mzigo now yuko free.
Ishu ya Neymar ni tofauti ile iliwekwa kama Dau kama timu ikitaka kumsajili na sio yeye akitaka kuvunjwa mkataba kumbuka mkataba mpk kuvunjwa lazima kuwa na sababu za msingi .Neymar yeye hakulipa PSG bali PSG ndio waliilipa Barca
IMG_20221225_094142.jpg
 
Hapo sijui Sheria is kuna raia ni vilaza sana kwenye soka,umeona wapi mchezaji mwenye mkataba na timu anasajiliwa na timu nyingine bila hizo timu kukubaliana? Yaani Leo Jude Bellingham apokee pesa kutoka Man City akailipe Dortmund then awe mchezaji wa Man City bila City na Dortmund kukubaliana?
Basi wachezaji wengi sana wangesepa Kwa namna hiyo.
Kama mkataba unaruhusu hivyo inawezekana. Rejea sakata la Neymar na barcelona wakati anaenda PSG
 
Bro ayo ni maoni yako, lakini kwani huonagi wachezaji wengi wakivunja mkataba na timu zao na kubaki wachezaji huru. Klabu inabidi iwe na ustadi wa kumbana mchezaji kwa kutokumpa uwezo wa kuuvunja mkataba kitu ambacho yanga wameshindwa kufanya. Mbona Dejan kavunja mkataba na simba akawa free agent saiv yuko tim nyngne. Ndomana yanga wanaitwa utopolo, hawana hata ustadi wa kutengeneza vizuri mikataba.
Kuvunja mkataba mtu haamui tu from no where ingekuwa hivyo ingekuwa rahisi sana ,hata Dejan yeye aliweka sababu .
 
Wakili na mwanamichezo mzoefu nchini, Aloyce Komba ametoa ufafanuzi juu ya dili la Fei Toto kutua Azam akisema:
.
“Yanga wamefanya uzembe wenyewe na wasije wakathubutu kukimbilia Fifa kama walivyofanya kwa Bernard Morrison itakula kwao. Waangalie vizuri mkataba wa mchezaji unaeleza nini, watapoteza muda zaidi.”
.
“Ninachokiona Yanga walimpa mkataba Fei ambao hauna faida kwao. Unawekaje kiasi hicho cha pesa kuvunja mkataba wake wakati unaona kabisa kiwango cha mchezaji kilivyo. mchezaji hawezi kuacha pesa hasa kama mkataba wake unaruhusu kuununua ama kuuvunja.”
.
“Sioni kama Azam wamekosea na ni timu ambayo inazingatia sana masuala ya kisheria katika kuvunja mikataba ya wachezaji wao ama wanaposajili mchezaji. Azam siyo wajinga kiasi hicho wakurupuke tu kumsajili Fei Toto pasipo kuzingatia taratibu za kimkataba.
.
“Wanachotakiwa kukifanya Yanga ni kuulezea umma ama wanachama na mashabiki juu ya hilo, lakini mengine ni kuleta siasa tu kwenye mpira.”

My Take
Nawakumbusha tu Yanga kuitwa Utopolo ni maono ya ndani sana. Hii ndio maana halisi ya Utopolo
Uto ni hamnazo wanakimbilia CAS wataenda kupigwa za uso
 
Utaratibu wa kuvunja mkataba haupo upande mmoja pia sheria za FIFA zinaruhusu kuvunja msimu ukiwa umeisha sio kati kati ya msimu hii kitu wasipo kaa kuongea Feisal hatacheza mpaka mwisho wa msimu
Ndugu umeisoma hiyo sheria ya Fifa vizuri na kuilewa?

Embu waza tu, ikiwa Feisali ameamua kuachana kabisa na soka kwa sababu zake binafsi (Kama kifamilia, kiimani), ni vipi sheria inampa haki yake ya kufanya hivyo, ikiwa kweli sheria za soka zinatamka 'mchezaji hawezi kuvunja mkataba na klabu yake kstika ya msimu'?
 
Kumekucha..ngoja tuone kama jioni atachezea Yanga
 
Kama mkataba unaruhusu hivyo inawezekana. Rejea sakata la Neymar na barcelona wakati anaenda PSG
Sakata la Neymar ni tofauti wabongo jifunze kufuatilia mambo Psg walitoa mpunga kwa Barca na Barca kipengele chao lilikuwa kinasema ikiwa club itamtaka basi dau lake ni kiasi hiki na sio player mwenyewe kujiamulia .

Kwa hiyo unataka kusema Neymar alienda Psg kama mchezaji huru?
IMG_20221225_094142.jpg
 
Kuvunja mkataba mtu haamui tu from no where ingekuwa hivyo ingekuwa rahisi sana ,hata Dejan yeye aliweka sababu .
Nakuambia hapa hapa JF, kuvunja mkataba unaweza kuamua 'from no where' na ukavunja vizuri tu, tena kisheria. Suala sio sababu unayotumia kuvunjia mkataba, suala ni kulipa gharama unayotakiwa kuilipa kama fidia ya kuuvunja huo mkataba.
 
Hapo sijui Sheria is kuna raia ni vilaza sana kwenye soka,umeona wapi mchezaji mwenye mkataba na timu anasajiliwa na timu nyingine bila hizo timu kukubaliana? Yaani Leo Jude Bellingham apokee pesa kutoka Man City akailipe Dortmund then awe mchezaji wa Man City bila City na Dortmund kukubaliana?
Basi wachezaji wengi sana wangesepa Kwa namna hiyo.
Hujawahi sikia kitu kinaitwa buy out clause na unadhani mikataba yao ni miepesi kama huu wa kuvunjwa kwa dola 48K? Hakuna sheria yoyote ya soka inazuia mchezaji kuvunja mkataba na club
 
Hapo sijui Sheria is kuna raia ni vilaza sana kwenye soka,umeona wapi mchezaji mwenye mkataba na timu anasajiliwa na timu nyingine bila hizo timu kukubaliana? Yaani Leo Jude Bellingham apokee pesa kutoka Man City akailipe Dortmund then awe mchezaji wa Man City bila City na Dortmund kukubaliana?
Basi wachezaji wengi sana wangesepa Kwa namna hiyo.
Thomas Partey alinyakuliwa AM kwa style hiyo, this is not new young boy
 
Wakili na mwanamichezo mzoefu nchini, Aloyce Komba ametoa ufafanuzi juu ya dili la Fei Toto kutua Azam akisema:
.
“Yanga wamefanya uzembe wenyewe na wasije wakathubutu kukimbilia Fifa kama walivyofanya kwa Bernard Morrison itakula kwao. Waangalie vizuri mkataba wa mchezaji unaeleza nini, watapoteza muda zaidi.”
.
“Ninachokiona Yanga walimpa mkataba Fei ambao hauna faida kwao. Unawekaje kiasi hicho cha pesa kuvunja mkataba wake wakati unaona kabisa kiwango cha mchezaji kilivyo. mchezaji hawezi kuacha pesa hasa kama mkataba wake unaruhusu kuununua ama kuuvunja.”
.
“Sioni kama Azam wamekosea na ni timu ambayo inazingatia sana masuala ya kisheria katika kuvunja mikataba ya wachezaji wao ama wanaposajili mchezaji. Azam siyo wajinga kiasi hicho wakurupuke tu kumsajili Fei Toto pasipo kuzingatia taratibu za kimkataba.
.
“Wanachotakiwa kukifanya Yanga ni kuulezea umma ama wanachama na mashabiki juu ya hilo, lakini mengine ni kuleta siasa tu kwenye mpira.”

My Take
Nawakumbusha tu Yanga kuitwa Utopolo ni maono ya ndani sana. Hii ndio maana halisi ya Utopolo
Nawakumbusha tu Yanga kuitwa Utopolo ni maono ya ndani sana. Hii ndio maana halisi ya Utopolo[emoji818][emoji817]
20221225_080258.jpg
 
Back
Top Bottom